Watu walio wengi wanaamini kuwa mwanaume ndiye mwenye uwezo wa kufanya kila kitu ukilinganisha na mwanamke,hata hivyo ukweli ni kwamba wanawake pia wana uwezo wa kufanya mambo ili mradi wakidhamiria kuliko hata wanaume. Mfano mzuri ni mwanamke huyu mama Mtua mkazi wa kijiji cha Kihagara mwambao wa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Mama Mtua ana kipaji na uwezo wa hali ya juu katika kupiga kasia, pichani mama Mtua akiwa katika mashindano ya mitumbwi akichuana vikali na wanaume katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni. Mashindano hayo yamekuwa na mvuto mkubwa katika utalii mkoani Ruvuma.Historia ya mama Mtua inaonesha kuwa alikuwa anatumia mtumbwi kama usafiri wake wa kwenda shuleni na kurudi katika kijiji jirani cha Tawi kata ya Liwundi umbali wa kilometa nane kutokana na ukosefu wa barabara nchi kavu. Picha na maelezo kutoka maktaba ya injinia Stella Manyanya, uwezeshaji wa wanawake Ruvuma.
Home
Unlabelled
nani kasema kina mama hawawezi kupiga kasia??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...