Meneja wa kanda ya ziwa  wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Ally Maswanya akipokea cheti  maalum kwa airtel ushiriki na shukrani toka kwa kamati na jeshi la usalama barabarani kwa Airtel kuwa mdhamini mkuu wa kampeni ya usalama barabara  kutoka kwa mgeni Rasmi Mh Jaji mkuu Mohamed Chande  Othman katika halfa ya ufunguzi  wa wiki ya usalama barabarani  iliyofanyika  kitafia katika mkoa wa Kagera wiki hii, wakwanza kulia pichani ni Mwenyekiti wa  Baraza la usalama barabarani na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh Hashim Kagesheki
Mwenyekiti wa  Baraza la usalama barabarani na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh Hashim Kagesheki akimshukuru Meneja wa kanda ya ziwa  wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Ally Maswanya kwa  kuwa mdhamini mkuu wa kampeni ya usalama barabara kwa mwaka huu 2011, haya yalifanyika katika halfa ya ufunguzi  wa wiki ya usalama barabarani iliyofanyika katika mkoa wa kagera wiki hii na kuudhuriwa na mgeni Rasmi Mh Jaji mkuu Mohamed Chande (kati) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani masawe (wakwanza kushoto). wadhani wakuu wa mwaka huu ni kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kampuni ya mafuta ENGEN Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...