Na Francis Dande
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda jioni hii amefika katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kumjulia hali Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amelazwa katika chumba cha Min ICU.


Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Spika Makinda alisema kuwa ofisi yake inaandaa utaratibu wa kumpeleka Mh. Zitto nchini India ili akapa matibabu zaidi.


‘Hali ya mgonjwa sio mbaya lakini tutaandaa utaratibu wa kumsafirisha kwenda India pindi madaktari watakapomuaandaa mgonjwa tayari wa safari hiyo na taarifa tutazitoa ni lini hasa hatasafirishwa alisema Mh. Spika’.


Naye Professa Victor Mwafongo amabaye ni Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Magonjwa ya dharura pamoja na Dk. Juma Mfinanga ambao ndio wanaomshughulikia mgonjwa huyo walisema kuwa ya mgonjwa huyo hali yake siyo mbaya sana ila anahitaji muda mwingi wa kupumzika kitu ambacho kwa sasa kinakosekana kutokana na idadi kubwa ya ndugu jamaa na marafiki kufika hospitali hapo kutaka kumjulia hali.


Aidha Dk. Juma Mfinanga aliongeza kuwa taarifa zaidi kuhusu hali ya Mh. Zitto ikiwemo safari ya kupelekwa India itatolewa pindi itakapokuwa tayari.

 Spika wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe juu ya hatua ya ofisi ya bunge kumsafirisha nchini India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
 Spika wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akimjulia hali mbunge wa viti maalumu Masasi, Crala Mwituka wa CUF ambaye amelazwa jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na Vidonda vya tumbo pamoja na Presha. Kulia ni  Daktari wa magonjwa ya dharura, Dk. Juma Mfinanga na Professa Victor Mwafongo ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya dharura.
 Spika wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akisalimiana na madaktari na wauguzi alipowasili katika hospitali ya Taifa ya muhimbili jioni hii kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.
 Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila akibadilishana mawazo na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kati) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (shoto) wakati walipofika kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jioni hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Badhi ya watu waliofika kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wakiwa nje ya chumba cha Mini ICU alikolazwa mbunge huyo wakati walipofika kumjulia hali.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akiongonzwa na daktari wa magonjwa dharura Dk. Juma Mfinaga (kulia) wakati alipofika katika hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. POLENI SANA WAGONJWA.
    INAMAANA WABUNGE HAWANA KAZI WOOTE WANATIRILIKA HOSPTALI. JAMANI AMKENI HII NI KARNE YA 21.

    WATANZANIA LINI TUTAJITIBU WENYEWE KWANINI TUKATIBIWE INDIA INAMAANA SISI NI MIZUMBUKUKU HATUWEZI JITIBU?

    AIBU AIBU AIBU AIBU.

    ReplyDelete
  2. ha ha ha ha hiwezekani mdau hao wataalamu tutatoa wapi na matumbo yetu je????

    ReplyDelete
  3. Jamani ni kweli Zitto amefariki dunia!!!

    ReplyDelete
  4. Shut ur mouth wee hapo juu...nyamafu..Zitto get well soon. Mungu akusaidiekwa kweli

    ReplyDelete
  5. kwani zito anpatwa n nini??

    ReplyDelete
  6. michuzi na wewe hutoi ufasaha, kwani zitto anaumwa na nini?

    ReplyDelete
  7. Jamani malaria tu jamanaa anandaliwa safari ya India au la kuna la zaidi ya hapo? Kuweni wa wazi.

    ReplyDelete
  8. muwe na tabia ya kusikiliza tv na redio jana wametangaza hivi, anasumbuliwa na maleria kali homa haishuki. hata msgs tigo wametuma, sasa mnataka kuchimbua ugonjwa gani tena zaidi ya maleria?

    ReplyDelete
  9. kwa mujibu wa chombo kimoja cha habari jana jioni kilisema Zitto anaendelea vizuri na amekutwa na maralia 1.5 na vipimo vingine vinaonesha yupo pouwa hana tatizo lolote ila kaka yake alisema Zitto huwa anasumbuliwa na tatizo la kichwa....LAKINI ANAENDELEA VIZURIIIII..tuzidi kumuombea Kamanda wetu.

    ReplyDelete
  10. MUNGU AKUJAALIE AFYA ZITTO,TUNAKUOMBEA NA WASHINDWE WANAOPIGANA NA WEWE

    ReplyDelete
  11. Nashauri Zitto apelekwe kwenye maombi, atapona kwa JINA LA YESU.

    ReplyDelete
  12. Jamani hospitali zetu zinaposhidwa kutibu hata malaria, sisi watanzania tujiulize hawa wataalamu wetu wanafanya nini? na pesa zetu za kodi zinatumikaje? Tumekosa kuwaza na kujithamini utu wetu kiasi hiki!! Hivi haya maendeleo tunayosubiria kwa kila mwananchi si ni ndoto tu za Alinacha!! Au ndio vile hatujui hata maendeleo yenyewe ni yapi?? Inaniuma sana tunaishi na kufa hakuna kinachobadilika. No safe running water, no sanitation and sewage system zinazoeleweka, hii misingi imetushinda, umeme, elimu, usalama barabarani na mengineyo.... TUTAFIKA KWELI?

    ReplyDelete
  13. Kun radhi!!!!!!!!!
    mi ni anonymous namba tatu kwenye comment!! mara ya kwanza nilipost comment nikiuliza nimepigiwa simu kuwa amefariki!! michuzi akaiweka kapuni!!! nikauliza tena chanzo changu kikaendelea na msimamo huo huo, nilichokosea ni alama za mwisho ie (!!!!) lakini nilikuwa na maana ya swli(????). Samahani sana!!!! ZITTO na wapiganaji wengine . TUKO PAMOJA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...