TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIKA baadhi ya vyombo vya habari jana na leo, kumeripotiwa taarifa za kuwapo kwa ugomvi baina ya wachezaji wawili wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi na Haruna Moshi Shaaban (Boban). Ugomvi huo umeripotiwa kutokea mara baada ya pambano la watani wa jadi lililofanyika jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vyombo hivyo viliripoti kuwa chanzo cha ugomvi huo ni madai ya hujuma na kutoaminiana ndani ya timu. Kwa masikitiko makubwa, Simba Sports Club (SSC) inapenda kukanusha kwa nguvu zote kuwapo kwa ugomvi wa aina yoyote baina ya wachezaji au viongozi wa klabu mara baada ya pambano la Jumamosi.

Mara baada ya mechi, hali iliyotamalaki ilikuwa ni ya fadhaa na huzuni kwa wote wanaohusika na Simba, wakiwamo wachezaji na washabiki. Habari hizo za ugomvi wa wachezaji ni uzushi unaoenezwa na watu wasioitakia mema SSC.

Kuna mambo mawili yanayoweza kubainisha kuwa habari hizo hazikuwa za ukweli. Kwanza, kwamba vipo vyombo vilivyodai kuwa Okwi alipigwa hadi kuvimba uso. Ukweli ni kuwa Okwi yuko salama, buheri wa afya na hajavimba popote mwilini mwake, achilia mbali usoni.

Pili, kuna magazeti yaliyoandika kuwa Okwi alipigwa vichwa vinne na Boban kabla hawajaamuliwa. Mengine yakaripoti kichwa kimoja. Kuna redio imeripoti kuwa vilikuwa vichwa vitatu. Tukio moja, taarifa tofauti lukuki. Kikubwa ni kuwa, hakuna mwandishi wa habari hata mmoja aliyeshuhudia tukio hilo na kulithibitisha pasi na shaka zaidi ya kusimuliwa na wale waeneza uongo.

SSC inashukuru kwa ushirikiano mzuri inaopata kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje. Tunawaomba wana Simba wawe watulivu katika kipindi hiki na tujipange kwa ajili ya mechi yetu ijayo ya VPL dhidi ya Moro United. Kama tutashinda, tutaongoza ligi hadi mwakani.

Timu inarejea kambini leo tayari kujiandaa na pambano hilo la mwisho la raundi ya kwanza ya VPL.

Ezekiel Kamwaga
Msemaji
SSC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 01, 2011

    "ETI KAMA TUTASHINDA TUTAONGOZA LIGI HADI MWAKANI" HAWA JAMAA NAONA BADO WANA HANGOVER YA KIPIGO!

    ReplyDelete
  2. WASWAHILI WANASEMA LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO BASI LIKO NJIANI LAJA. BWANA KIMWAGA SIKU MOJA UTAWAJUA TU SIMBA MUULIZE NDIMBO.

    ReplyDelete
  3. Hata Simba wakifungwa mechi ya mwisho mzunguko wa kwanza, bado wataendelea kuongoza ligi labda kama Yanga watashinda kwa mabao kuanzia 5 bila.

    ReplyDelete
  4. wewe YANGA BOMBA HAKUNA HANGOVER YA KIPIGO WALA NINI SIMBA BADO NI TIMU BORA KULIKO YANGA, WALIOKUWEPO MPIRANI WAMEONA!!!! TEHE TEHE,, NDIO MAANA YANGA WAMEANZA UZUSHI AT OKWI NA BOBAN WAMEPIGANA.. HAITOTOKEA KWA SIMBA BANA LABDA YANGA TEH, WAMETIMUA TIMBE NA KURUDIA MATAPI TEHE,TEH, KANDAMBILI BANA KANDAMBILI TU TEH,,,.

    ReplyDelete
  5. ACHANI UBWEGE MIMI NI MWANACHAMA NUMBER 23657 NIKWELI BOBAN ALIMPIGA OKWI KWANINI MFICHE HABARI HIZI? ACHENI UTOTO BWANA EBO!

    ReplyDelete
  6. SIMBA MOJA KANGA MOKO NDEMBENDEMBE LAKI SII PESA

    CHELSEA FIVE STAR MODERN TAARABU FOOTBAL CLUB

    ReplyDelete
  7. HAJAKOSOA BRO ANA MAANA KAMA WATASHINDA. NA KAMA ITAKUWA HIVYO, KWA KUWA HIYO ITAKUWA MECHI YA MWISHO YA MZUNGUKO WA KWANZA, NA KWA KUWA MZUNGUKO WA PILI UTAANZA MWAKANI BASI LIGI ITAKUWA IMESIMAMA NA HAO JAMAA WATAKUWA WANAONGOZA KWA MUDA HADI MZUNGUKO WA PILIN UTAKAPOANZA MWAKANI

    hao jamaa wa kwa jonathan na mwenzie ni kweli walikuwa na bifu na wamekaripiwa wasiseme lolote kwenye vyombo vya habari ndio maana jamaa anawahi hapa kukanusha. ila huo ndio ukweli mimi nilikuwa shuhuda ila sikuwa na camera

    ReplyDelete
  8. tehe tehe ama kweli ukigongwa na nyoka hata kamba inakutia adabu.kwa taarifa yenu msipojipanga mnatwangwa na moro.

    ReplyDelete
  9. sasa mbona mimi simuelewi? mimi ni simba lakini taarifa kama hii ingepitia kwangu nisingeiruhusu iende on air, waeleze watu kilichotokea halisi ni NINI? sio kujikanyaga na kukanusha ujinga, ukieleza ukweli unawafunga midomo, ukieleza pumba unawapa nafasi ya kuongea zaidi!!! UMETUANGUSHA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...