Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen akielekea kucheck in kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jioni ya leo wakati timu hiyo ikiondoka kuelekea  Morocco
Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakichek in jioni ya leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere kuelekea nchini Morocco.





Timu ya taifa 'Taifa Stars', leo imeondoka nchini kuelekea nchini Morocco ,kwa ajili ya mchezo wao utakaofanyika jumapili kukamilisha mchezo wa mwisho wa kundi D kwa kunyukana na timu ya Morocco,katika mji wa Marrakech nchini humo,katika kuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, mwakani (CAN 2012).

Aidha katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa Taifa Stars,Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imetoa sh. milioni 165 kwa ajili ya safari ya timu hiyo,ambapo fedha hizo zimetokana na vifaa, nauli ya kwenda na kurudi na gharama zingine za timu hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Emphraim Mafuru alisema kampuni yake kwa miaka mitano mfululizo imedhamini timu za taifa zikiwemo za vijana na wanawake, hivyo wataendelea kufanya hivyo.Alisema katika kuhakikisha Stars inafanya vizuri wametoa sh. milioni 165 kwa ajili ya vifaa vya mazoezi, zikiwemo jezi na viatu, nauli ya kwenda na kurudi Morocco pamoja na gharama zingine za safari hiyo na kwamba anawaomba Watanzania, waiombee timu hiyo ili itoke na ushindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. WATANZANIA WALISHAKATA TAMAA,WANAONA NI VYEMA WAISHANGILIE TWIGA STARS KWANI INAFANYA VIZURI SANA UKILINGANISHA NA KIKOSI CHA POULSEN. MI NAONA KUNA HAJA WADOU WAKAE WAMTAFUTE MCHAWI.
    HAO WATOTO WA JK WANAHUDUMIWA VIZURI SANA LAKINI WAKIINGIA UWANJANI KAZI YAO NI KUKAMILISHA RATIBA TU. AIBU KWA TAIFA STARS

    ReplyDelete
  2. Minadhani tuanza kuchukua vijana wadogo ambao kuwafundisha sio kazi ngumu maana hatutaendelea hata kidogo kwasababu ya kusajili walewale wazee ambao hawaambili maana tutamlaumu kocha bila sababu na vijana (WATOTO) wapo ambao wanaweza kufundishika na wasomi.navilevile wakulaumiwa ni TFF na siyo mwingingine

    ReplyDelete
  3. Mzee Poulsen kachoka kweli kweli, kama vile anataka kuanguka!!!

    ReplyDelete
  4. MUNGU IBARIKI TAIFA STARS! KWA BARAKA ZAKO ZOTE MOLA WETU
    BY BABU JAY

    ReplyDelete
  5. Du huyu kocha anaomba mkataba wishe maana keshajichokea hebu tz kwanzawasilazimishe mashindano wakae wapange mbinu za muda mrfu kufundisha watoto kuanzia ten na seven kisha tushiriki tena wakishafika angalau 16

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...