Heshima yako kaka mkubwa.
Kwanza napenda kukupa hongera kwa kazi nzuri unayoifanya, kiukweli umekuwa mfano mzuri kwa wanablog wote hapa nchini na mimi nikiwa mmoja wapo.

Naomba kuchukua nafasi hii kuweza kutambulisha na kuiombea nafasi ya kuitangaza Blog Mpya kabisa inayojihusiha na utafutaji na ukusanyaji wa habari zinazouhusu wanafunzi waliopo katika elimu ya juu hapa nchini.

Blog hiyo inajulikana kama 

 www.tzcampusvibe.wordpress.com
Blog hii ni maalum kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuweza kuhabarisha jamii kupitia shughuli mbalimbali zinazoendelea vyuoni ili jamii iweze
kuelemika, kuburudika na kuhabarika kuuhusu matukio hayo.

MADHUMUNI YA BLOG.
Kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wanafuniz pamoja na jamii kiujumla juu ya maswala mbalimbali yanayohusu wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania ambapo watapata fursa yakuelezea mambo yatakayosaidia
kuendeleza jamii. Wanafunzi na jamii kiujumla inakaribishwa katika kutoa habari, maoni ushauri pamoja na kutangaza sherehe na matukio anayotokea au yanayotarajia kutokea vyuoni au hata nje ya vyuo lakini yakiwahusu wanafunzi.

Natambua changamoto ya nafasi katika libeneke lako Ankali, lakini natumaini uwezekano wa kupata nafasi hiyo adimu.

Asante sana.

Naomba kuwasilisha.

Contacts
Tanzania Campus Vibe
P. o. Box 45722
Dar es Salaam
Tanzania.
Calls:             +255 713 441 892                  +255 715 540 052                  +255 714 126 088      .
Email:  tzcampusvibe@gmail.com , Website: www.tzcampusvibe.wordpress.com




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Daaaah watanzania hatutafika kamwe tumekaa kuiga iga tuuu kila kitu sasa hawa nao wameona wenzao wa www.tzwanavyuo.blogspot.com wanafanikiwa nao wameamua kuiga kila kitu na kufungua libeneke hili.. mimi kama mdau mkubwa wa Matukio na wanavyuo hawa jamaa wamekosea sana kwa nini wasiplan kitu kingine kulipo kuiga kila kitu inasikitisha na inaonesha jinsi ambavyo watu elimu haijatukomboa kabisa this is a Shame.... and shame on them na pia nawatumia the same email kwa email yao si muda wamekera sana sana sana..... daah kweli Tanzania balaaa. wetazama wameiga mpaka mwanzo wa jina tz..... kila kitu angalia malengo yao na ya matukio na wanavyuo angalia tuu utaona wamekera na kuboa bwana

    ReplyDelete
  2. Mi nadhani huo ndio ushindani wa soko huria kwamba kwa wanaoamini katiki soko la ushindani hujivunia pale wanapoona wameona mtu anawaiga katika kitu ambacho wanakifanya so mi naona hakuna kosa lolote lilifanyika na hata kama ukisoma maudhui yao vizuri katika Blog zao wote ndio wanakusanya taarifa za wanafunzi vyuoni lakini wakatofautiana angle ya kuandika taarifa izo ivyo kuleta uwelewa mzuri sana.
    Inamaana leo Tanzania magazeti yote yafutwe libakie moja tu, au Radio zote zifutwe na ibakie radio RTD peke yake so sidhani kama kuna kitu kibaya kimefanyika.
    Ankali leo wangapi wamejifunza kutoka kwake na wanafnya maswala ya blog, makampuni ya simu yote yanafanya kazi moja lakini kila mtu anacustomers wake, kwenye vinywaji kuna makampuni tofauti yanauza same vinywaji lakini vina ladha tofauti.

    Tuamini katika soko la ushindani na hata kama Idea zinafanana kwa wanaotengeneza bidhaa au service basi faida huwa ni kwa mteja kwani anakuwa na uwanja mpana zaidi wa kuchagua bidhaa gani atumie.

    KWA FAIDA YAKO NA WENGINE Katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wetu, vyombo vya habari vimeongezeka na kuimarika sana nchini. Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na kituo kimoja tu cha redio, leo nchi yetu inavyo vituo vya redio 73, vituo vya televisheni 26 na magazeti yaliyopata usajili 71. Kwa upande wa Vyuo vya Habari leo hii kuna vyuo 12 vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya habari, ambapo kati ya Vyuo hivyo, vyuo vikuu vipo vinne.

    Pengine hawa jamaa wa TzCampusVibe walikuwa na hilo wazo toka muda mrefu kabla hata hawa Tzwanavyuo lakini walikuwa hawajapata nafasi nya kufanya ivyo.

    Na ndo maana hata hapa Dar kuna events kibao za wanafunzi zinakuja lakini zinatofautiana kwenye maudhui, angalia tukio la mbalamwezi la kesho kutwa na la mwezi ujao tarehe 4 yote ni iidea sawa sema wanatofautiana ladha.

    Changamoto ni muhimu katika maendeleo.

    HONGERENI WANA TZCAMPUSVIBE MMEONYESHA JINSI GANI MNAWEZA KUSHINDANA KATIKA SOKO LA USHINDANI. KAZI YENU NZURI MIMI NIMEIPENDA.ENDELEENI KUTULETEA MALIBENEKE TOKA MAVYUONI WADAU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...