Wachezaji wa Yanga wakiomba dua baada ya kumaliza mazoezi yao leo katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kocha wa timu ya Yanga,Kostadin Papic akikata kiu wakati timu yake ikiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Beki wa Yanga Nadir Haroub (kulia) akichuana na mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo jioni.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Dar Young Africans leo wamefanya mazoezi yao chini ya Kocha wao Mserbia Kostadini Papic katika Uwanja wa Chuo Kikuu ikiwa ni maandalizi yao dhidi ya Simba mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi. Wakati Dar Young wakiwa katika ufukwe wa Kigamboni wakiendelea na mazoezi watani wao wa jadi Simba wamepiga kambi katika Hoteli ya Bamba Beach.

Akizungumza na ripota wetu msemaji wa Yanga, Luis Sendeu alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kiko fiti tayari kwa kupambana na Simba na wachezaji wote 28 waliosajiliwa wamehudhuria mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu na hakuna majeruhi.

Naye Kocha wa timu hiyo, Kostadin Papic akizungumza na Blogu ya Jamii mara baada ya mazoezi alisema kuwa kuwa kikosi chake akijiandai kwa ajili ya mchezo wa jumamosi bali iko katika programu ya mazoezi ya kawaida na sasa anawapa wachezaji mazoezi ya stamina ili kukabiliana vilivyo na timu pinzani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...