Kila Jumapili ya mwisho wa mwezi ni Visiting day katika shule ya wasichana ya Barbra Johanson Model Girls High School jijini Dar ambapo wazazi, ndugu, jamaa na marafiki hufika kuwatembelea wanafunzi wakiwa shuleni. Ni siku njema na inapendeza sana kwani kunakuwa na kila aina ya shamrashamra na picnic chini ya vivuli vya miti  mingi iliyopandwa katika bustani nzuri za shule hiyo.
 wanafunzi na ndugu zao na jamaa wakiwa katika picnic shuleni jana
 pametulia
 Ni furaha kukutana na wazazi baada ya masomo magumu ya kila siku
Ankal alikuwepo kumtembelea binti yake mpendwa Mamou  ambaye alimkuta akiwa na marafiki na wadogo  zake. Ankal anamtakia masomo mema Mamou na wenzie. BOFYA HAPA kupata post zake za awali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ankal next time make sure unanipitia tuende tukamtembelee Mamou! Mimi ni kijana mzuri mwenye heshima na nipo very focus katika maisha. Nimevutiwa sana na picknick! Usinisahau next time Ankal! Asante

    ReplyDelete
  2. Lo ,Ankal hapa niandae ng'ombe wangapi bana mi nshafika bei hahahaha

    ReplyDelete
  3. ankal lini anamaliza shule? itabidi tuwasiliane nifanye booking kabisa!

    ReplyDelete
  4. Ankal haya umeshaanza kuombwa invitation za kumtembelea Mamou sema sasa- -- -

    ReplyDelete
  5. Tokea nimeanza kusoma sijawahi kutembelewa na mzazi lakini cha ajabu nilifaulu vizuri na nawashukuru sana wazazi wangu kwa malezi waliyonipa. Ama kweli zama hubadilika.....enzi hizo nikiwa mazengo(1999-2001), tosamaganga(1995-1998)

    ReplyDelete
  6. Tokea nimeanza kusoma sijawahi kutembelewa na mzazi lakini cha ajabu nilifaulu vizuri na nawashukuru sana wazazi wangu kwa malezi waliyonipa. Ama kweli zama hubadilika.....enzi hizo nikiwa mazengo(1999-2001), tosamaganga(1995-1998)

    ReplyDelete
  7. Hehe mdau hapo juu kavutiwa sana na picknick au anataka kumuumizia ankali si bora useme tu kijana unataka kuanza vita na mjomba

    mjomba ankali inaonyesha mambo yako sio mchezo umeingia na shangingi la nguvu kama la waheshimiwa wabunge.

    ReplyDelete
  8. mdau hapo juu unasema hukuwahi kutembelewa, umesahau nilipokuwa msalato nilikutembelea sana mazengo na sometimes tulikuwa tunakutana guest kule mtaa wa airport, hali kadhalika baada ya wewe kwenda Tosamaganga (kwi-tosa) mie nikawa pale iringa girls (zoo) tukaendeleza libeneke - ndo maana ulifaulu vizuri

    ReplyDelete
  9. huyo dada picha ya kwanza aliyeshika mkono mtoto inaonekana dona na mandondo vimempenda....maana shavu shavu, au sijui ndo dada mkuu anapata "top layer" daily...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...