Afisa tarafa Bw. Peter Masidi akifungua rasmi vyumba viwili vya madarasa ya shule ya Sekondari Lusaka yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation yenye thamani ya shilingi milioni 37 (kulia) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule akimshukuru afisa ElimuYaSekondari Wilayaya Sumbawanga Bi. Emilia Fungo mara baada ya hafla fupi ya kukabidhi vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya sekondari Lusaka wilayani humo vyenye thamani ya sh. Milioni 37 vilivyo jengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation.
Kikundi cha wanawake kikitoa burudani katika hafla fupi ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyo jengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation kwa Shule ya Sekondari Lusaka Wilaya ya Sumbawanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kazi nzuri Vodacom. Sasa naamini kuwa mnasaidia hata ambako mapaparazi hawapo. Kudos!

    Mdau wa Lyazumbi (RUKWA)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...