Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwasha Trekta kama ishara ya uzinduzi wa kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya katika Mkoa wa kusini Unguja.
Baadhi ya matrekta yakianza kuchimbua katika hatua za matayaarisho ya kilimo cha mpunga katika bonde la Cheju, kwa mwaka 2011-2012 kilichozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,leo katika bonde hilo Wilaya ya kati Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na wakulima wa bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kuzindua matayarisho ya kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika Mkoa wa kusini Unguja.
Mwakilishi wa Jumuiya za wakulima katika bonde la cheju Getruda Adolfi Mkude,akisoma risala ya wakulima katika uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu huu wa mwaka 2011-2012,ambapo wastani wa ekari elfu tatu zitalimwa mpunga kwa kutumia mbegu za kisasa
Wakulima waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wakulima hao naa kuwataka kutumia mbegu bora za kisasa ili kukuza pato katika kilimo hicho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiyakagua matrekta ya wizara ya Kilimo na maliasili,wakati wa uzinduzi wa kilimo cha mpunga katika bonde la cheju Wilaya ya Kati Unguja,leo kabla ya kuzindua rasmi kilimo hicho kwa msimu wa mwaka 2011-2012
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwasalimia viongozi wa jumuiya za wakulima katika bonde la cheju alipowasili kuzindua kilimo hicho kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ramadhan Othman IKULU.
hakuna kulala, huku sisi tutaendelea na kampeni zetu za 2015 wenzetu huko Zenj ni kuchapa kazi na kujenga nchi. Mungu awaongezee uwezo, nguvu na hekima katika juhudi zenu za kujiletea maendeleo.
ReplyDeletewakiweza kulima hata nusu ya chakula chao ndipo watapata maendeleo..
ReplyDelete