wadau wa mradi wa kuboresha huduma za mama na mtoto kwa kutumia TEKNOKHAMA . wakijiandaa kuvuka mto kuelekea utete ,Kutoka kushoto Renatus Sona kutoka (CSSC), Twaha Mubarak (Chuo cha Afya Muhimbili),Jacob Mtalitinya(ITIDO),Sunday Morabu (SOFTMED) wa mwisho ni rubani wetu mzee John.
wadau wa mradi wa mama na mtoto wakiwa safarini kuelekea utete wakakutana na mwenye boma lake kaimu mkuu wa wilaya ya rufiji na mkuu wa wilaya ya mkuranga,Mh.Henry Clemens (katikati),kulia ni Jacob na kushoto kwa mkuu wa wilaya ni Twaha .
wadau wa Mradi wakiwa katika kuhamasisha mradi wa kuboresha afya ya mama na mtoto kwa kutumia mtandao ,mradi huu unafadhiliwa na shirika la Spider la Sweden na unalenga kupunguza hatari ya vifo kwa kina mama wajawazito na watoto wadogo chini ya miaka mitano ,simu za mkononi zitatumika katika kutoa taarifa kutoka kwa wahudumu wa afya vijijini kupeleka katika vituo vya afya ili kuwahimiza kina mama na watoto kuhudhuria clinic na kupata tiba .Mradi huu ndio unaaanza na utazinduliwa rasmi hivi karibuni .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...