Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam ( DUCE) wakati walipokusanyika leo katika ofisi za benki hiyo tawi la NMB House jijini Dar es Salaam kufuatilia malipo yao baada ya benki hiyo kuchelewesha fedha za mikopo kupitia akaunti zao.
Akiongeza na Globu ya Jamii Bw Kajula amefafanua kwamba mhasibu wa DUCE alipeleka hapo NMB orodha ya wanaostahili kulipwa siku ya Alhamisi iliyopita, lakini haikuwa na majina. Alipoambiwa kurekebisha muda wa kazi ulikuwa umepita na hakuweza kupeleka majina siku iliyofuata ya Ijumaa kwani ilikuwa ni sikukuu (Nyerere Day). Akaongeza kwamba mhasibu huyo alileta majina hayo leo asubuhi na baada ya taratibu za kibenki kukamilika malipo yalianza kutolewa saa sita kasoro dakika kumi leo, hivyo wanafunzi hao wakachukua chao na kuondoka bila mgogoro.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam ( DUCE) wakiwa wamembeba Rais wa wanafunzi, Msafiri Kidunye wakati walipokusanyika leo katika tawi la NMB House jijini Dar es Salaam jana kujua hatima ya malipo yao baada ya benki hiyo kuchelewesha fedha za mikopo kupitia akaunti zao. Hata hivyo walianza kulipwa leo na mambo yote yakaenda sawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...