Na mwandishi wetu
Wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Abbas Hamis Kinzasa ‘20%’, Kundi la Waimbaji la Glorious Singer, Dot Com Generation na wengine wengi wanatarajiwa kuwasha moto wa burudani kwenye Tamasha la Street University litakalofanyika Novemba 27, mwaka huu jijini Arusha.

Tamasha hilo kubwa la ujasiriamali lenye kaulimbiu ya Kujikomboa na Kuondoa Umaskini kupitia Ujasiriamali litafanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo na kuwakutanisha wajasiriamali, wafanyabiashara na vijana watakaofundishwa mbinu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini kupitia ujasiriamali.

“Ukiachilia mbali burudani, tutatoa mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo namna ya kupata wazo la kibiashara, kupata mbinu za kujitajirisha, kujifunza kuwa mwajiri badala ya mwajiriwa, jinsi ya kuomba mikopo mikubwa benki, kupanua mitaji na mada nyingine kemkem. Nawasihi watu wajitokeze kwa wingi kwani ni tamasha la kipekee kwa kiingilio cha Sh. 5000 tu,” alisema mratibu wa tamasha hilo, James Mwang’amba.

Watoa mada katika tamasha hilo ni wajasiriamali wa kimataifa na wazungumzaji wa kutia hamasa (motivational speakers) Eric Shigongo na Mwang’amba. Wadhamini wa tamasha hilo la kihistoria ni Kampuni ya Global Publishers Ltd, Malta Guiness, Airtel, Azania Bank na Mfuko wa Penseni ya Watumishi wa Umma (PSPF).


Wengine ni wauzaji na wasambazaji wa vipodozi asili wa Oriflame, Hoteli ya Corridor Springs ya Arusha, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 20% imefaa sana kurudi ktk upande wa kiimani, hii itasaidia sana kuujenga mwenendo wako!

    Big up 20%!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...