AJALI YA LORI LA MCHANGA IMETOKEA JION YA LEO AMBAPO UTINGO WA GARI HILO AINA YA FUSO ALINASA NA KUPOTEZA MGUU WA KUSHOTO,SHUHUDA WAMESEMA NI UZEMBE WA DEREVA WA FUSO ALITEREMKA KWENYE KILIMA AKIWA KWENYE MWENDO KASI ASIJUE KAMA KUNA TUTA KABLA YA DARAJA. PICHA NA MDAU PAUL MARENGA
 WASAMARIA WEMA WAKIJITAHIDI KUMUOPOA UTINGO WA LORI HILO
UTINGO WA LORI HILO AKIWA AMENASA BAADA YA AJALI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi waandishi wa habari huwa wana akili kweli? Baadala ya kuokoa majeruhi, wenyewe wana kazana kupiga picha tu. Nyambafu!

    ReplyDelete
  2. Michuzi, kwa hii picha ungewapa watu option ya kuitazama au la ingekuwa vema sana. Namna hii sio vizuri kabisa, hasa kama baadae tutapata habari mbaya kuhusu huyu utingo (hatuombei iwe hivyo kabisa, ila ya Mungu tumuachie Mungu). Naye ni bianadamu tu kama wewe na mimi. Angekuwa ni mtu unayemfahamu (rafiki yako) ungemuweka hapa namna hii?

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe mchangiaji wa kwanza hivi huoni hapo kuwa bodi inatakiwa kukatwa na msumeno wa chuma ili jamaa atoke. Au ulitaka waandishi wararue hayo mavyuma kwa meno?

    ReplyDelete
  4. kila mtu anatakiwa afanye kazi yake, na ikiwa hivyo hayo malalamiko yako hayatokuwepo, asingepiga picha, ajali hii usingeiona, na watu wakumuokoa majeruhi walikuwapo kama unavyoona kwenye picha. si kweli kwamba daima waokoaji wakiwa wengi sana ndio uokoaji utafanyika vizuri na haraka, bali idadi ya waokoaji inayohitajika ni ile inayohitajika kwa ajili ya uokoaji mzuri na wa haraka.

    ReplyDelete
  5. Picha muhimu.

    David V

    ReplyDelete
  6. Sasa wewe ungepataje taarifa. Kazi yao si kuokoa bali kuhabarisha

    ReplyDelete
  7. Kama Kuna Daraja na Tuta!! Halafu Tuta Hakuna Kibao Cha Kuelekeza Kuna Tuta!! Huu UUtakuwa na Uzembe Mkubwa wa TANROADS NA SIO DEREVA!! TANGU LINA CHINI YA MLIMU KUKAWEKWA TUTA? AMA KWELI HII NCHI WATUMIA MASABURI NI WENGI!! MAGUFULI UMEKWENDA WAPI? WENGI WA WATANZANIA HAWAJUI VIASHIRIA NA VISABABISHI VYA AJALI!!

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza kazi ya mwandishi wa habari ni kutoa taarifa kwa umma na kama asingepiga hizo picha maana yake wewe ungekosa cha ku-comment, wote wakiwa na mawazo kama yako itakuwa ni balaa. Hapo mwandishi ametupa hali halisi ya ajali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...