Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam Inaeleza kuwa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro (pichani) pamoja na washtakiwa wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratias Mgasa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh10 milioni,leo wamefutiwa mashtaka hayo yaliyokuwa yakiwakabili na kuachiwa huru kabisa.

Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 57 mpaka sasa

  1. mungu mkubwa
    tumeon haki ikitendeka
    thank you jesus

    ReplyDelete
  2. Hongera Jerry na pole sana.

    ReplyDelete
  3. mungu ashukuriwe mungu ashukuriwe

    ReplyDelete
  4. Kwa mara ya kwanza naona haki na demokrasia yaanza kukubalika bongo, halafu siamini eti Kikwete kakabali maombi ya chadema, kweli mungu ibariki Afrika

    ReplyDelete
  5. Nimefurahi sana, Jerry am happy for you as if wewe ni kaka yangu wa kuzaliwa, mwenyezi mungu akujaalie maisha yenye amani na furaha

    ReplyDelete
  6. Truth will always prevail. hongera jerry. aluta continua

    ReplyDelete
  7. amen
    Jerry, rudi kwenye habari na report maalum ukatupe macho tuone yanayoendelea nchi hii. Hongera kwa ushindi huu mkubwa na jina linazidi kupaa

    ReplyDelete
  8. yaani duh nimefurahi sana utafikiri ki2 gani, mungu hamtupi mja wake na nashukuru haki imetendeka ila nilitegemea ingekuwa hivi, pole sana kaka ndo mitihani ya maisha hyo jipange upya.

    ReplyDelete
  9. Hongera Jerry Muro kwenye ukweli uongo hujitenga

    ReplyDelete
  10. Hongera sana jerry, its true that truth will always prevail. am happy for you brother. Endeleza libeneke kaka songa mbele.

    ReplyDelete
  11. Sidhani kama aluta continua; nadhani atakuwa makini sana kwenye reporting. Maana kimenuka walomwajiri wamemwacha acheze rumba peke yake wakati alikuwa anafanya kazi kwa ajiri ya shirika lake.

    ReplyDelete
  12. Pole sana Jerry. Walikubambika kesi ili usione walichokuwa wanafanya. Sasa hivi wameshamaliza kula wameamua wakuachie. Hata hivyo Mungu ni wa kushurkuriwa kwa kukupa uhuru. Na Mungu huyohuyo awalaani wale wote waliokubambika kesi (kama kweli ulibambikiwa).

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli Mungu mkubwa kwake yote yanawezekana. Jerry pole sana watanzania wenzako tulikuwa tukikuombea na kweli umeshinda. Ukimkabidhi Mungu njia zako zote yeye huwa ni mwaminifu na hukumu yake huwa ni ya haki. Jerry mdogowangu utapata kazi nzuri as long as unaelimu yako ya kutosha na usiache kupambana hao mafisadi, wala rushwa usiache kuwafichua njama zao zote. Huta kufa bali utaishi na utayasimulia matendo ya Mungu Zaburi 118:17.
    God bless you

    ReplyDelete
  14. Siku zote UONGO NA UKWELI vitajitenga na ukweli daima utashinda. Ndio kazi za mafisadi hizo lakini Mungu yuko upande wako

    ReplyDelete
  15. Mie ushauri wangu kaka muro kamahi unachengine cha kufanya shika kaka maana ukitaka urejee tena saivi naota kama watakupoteza kabisa hio ndo bahati kaka . ila mwisho shika lile unaloliona lina maslahi na wewe . maoni yangu tu ni hayo.

    ReplyDelete
  16. Aibu yao kova na polisi wake!!!! ningeshangaa sana,kwani sijawahi kuona wala kusikia sehemu nyingine kuwa rushwa inaombwa kwa mtutu wa bunduki,dpp gani anaweza kupeleka kesi ya hovyo hivi mahakamani?
    hongera sana jerry,najua ulijua hakukuwa na kesi ndio maana uliendelea na mipango yako ya kimaisha,wakurudishie pingu zako,kama wanazitaka wakupe elfu ishirini na tano zako.

    ReplyDelete
  17. God Is Great Always! Tunamshukuru mungu kwa Ushindi huu Mkubwa. Hongera sana Kaka kwa Ushindi endeleza libeneke, bongo pakikuzingua nenda zako Aljazeera au BBC huko.

    ReplyDelete
  18. wale waliojiuliza kwanini ameoa wakati ana kesi mmeona Mungu anavyojua kutenda...Jerry Pole na Hongera...Mungu akupe moyo wa kusamehe, ndio mitihani ya dunia

    ReplyDelete
  19. Hauchi hauchi kumekucha. Haki hucheleweshwa tu, lakini haipotei.

    Jery, rudi kacheze kwenye namba yako, sasa hivi kuwa makini sana wakati wa kufunga magoli, kwani mabeki wanajua sana jinsi ya kumkaba straika au mfungaji bora.

    Mungu akuzidishie umakini katika kazi yako. Amen.

    ReplyDelete
  20. Hongera sana Bro.Tunasubiri vitu vya ukweli ktk kipindi chako chenye utalaam wa hali ya juu.Mungu mkubwa.

    ReplyDelete
  21. pole ila bora ufuate maisha yako wa2 wabaya kaka

    ReplyDelete
  22. pole sana kaka ni mitihan tu ya dunia, wamekukuza kitaaluma kwan bila changamoto hakuna mafunzo. Endelea kumuomba mungu kwani ni mwema wakati wote.

    ReplyDelete
  23. ALLAH ndio wa kushukuriwa, jema linatoka kwake na shari pia inatoka kwake na hii yote ni mitihani ya maisha. Waja tunachotakiwa ni kuvuka salama kwenye mmoja kati ya mtihani atakaokujaalia. Anachotupima jee tutamshukuru au tutamkufur pale tunapopata mitihani toka kwake? Naamini kijana wetu umemshukuru yeye ALLAH wakati wote na ndio maana amekuvusha kwa mtihani huu. Ombi langu usivunjike moyo na tunataka tuone au tusikie kutoka mdomoni kwako ripoti hii maalum. Wala usikubali kuwa wamekuachia kwa sharti la kukufunga mdomo usitoe ripoti maalum, wao hawana uwezo wa kukuachia huru ni ALLAH tu peke yake ndio mwenye uwezo huo amesema kwenye Qur an takatifu kuwa ni yeye peke yake mwenye uwezo wa kusema "kuwa na jambo likawa" TUNASUBIRI RIPOTI HII MAAALUM

    ReplyDelete
  24. mbona mnasena mungu, mungu....? haya ni mambo ya kisheria si kiimani

    ReplyDelete
  25. wooow! at looong last you are free my brother! ALLAH is great,im real happy for you,may ALLAH guide in the right path,i would like to congratulate you for marrying that woman who believes in you!

    ReplyDelete
  26. Sasa je nini hatma ja ajira yake?...atapata mafao ya namga gani?...mtamlipa fidia au kiinua mgongo?..au mtamrudisha kazini TBC?...kwa kuwa inaonyesha kesi yenyewe ni ya yeye kukomolewa tu kwa vile aliwaumbua wakubwa!

    ReplyDelete
  27. Mwenyezimungu ni mkubwa, hatimaye haki imetendeka na hila za wachache wanaofikiri wao ni Watanzania zaidi kuliko wenzao zimeumbuliwa.
    Mwanagu Jerry tunakusubiri kwa hamu na utakuwa na nguvu zaidi kipindi hiki. Mtegemee tu Mwenyezimungu na ufanye maombi sana kwani japo shetani ana nguvu lakini hawezi kumzidi muumba wake. Tuko pamoja japo kutokana na tulipofikishwa na hii system na mafisadi wao hatuwezi kukupa support sana zaidi ya kuwa wapenzi wa makala zako na kazi zako.

    ReplyDelete
  28. wow!hongere sana jerry Muro kwa ushindi wa kesi>angalia sana wasije kukutega sana maana tanzania sasa ni wasanii sana.Jipange sawasawa kaka!kuhani wa kweli ni Mungu na ndie atahukumu sasasawa siku ile ya mwisho.

    ReplyDelete
  29. TO GOD BE THE GLORY..

    ReplyDelete
  30. HONGERA SANA JERRY, MUNGU NI MKUBWA SANA. AIBU IMEKUWA KWAO.

    ReplyDelete
  31. mungu mkubwa walijua watakumaliza kwa mbinu za aina yoyote ile lakini haluna km mungu aliopewa kapewa na aliopangiwa kapangiwa tu kaza buti usirudi nyuma mwendo ni ule ule tu nimefurahi sana sijui nielezee nini furaha ynagu

    ReplyDelete
  32. Jerry anastahili fidia kwa kupotezewa muda wake,kazi yake na gharama alizotumia

    ReplyDelete
  33. yote ni mema asante Mungu

    ReplyDelete
  34. TBC SASA WAMEUMBUKA MANAKE WALIKUFUKUZA KAZI BILA HATA YA KURUDI NYUMA KUANGALIA WAPI MMETOKEA NA NINI UMEWAFANYIA WALITAKA WAZIDI KUKUCHANGANYA LAKINI MUNGU NDIYE MUAMUZI SASA UKO HURU KAZI KWAO NA WENGINE KM HAO HONGERA SANA

    ReplyDelete
  35. Mungu ni mwema. binafsi roho ilikkuwa inauma sana, kila nikisikia Jerry yuko kizimbani.kweli kama mdogo wangu. Nilihuzunishwa sanaa. Mungu akupe moyo wa kusamehe

    ReplyDelete
  36. nahisi ni furaha ilioje leo yaani mungu mkubwa sasa ndio wakati wa kufanya kweli manake walitaka kukuzika wakati uko hai hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ni kazi tuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  37. I Think he deserve that.
    Good up bro broo n make sure u make da follow up of dis issue until u get back ur respect to the society.
    benson

    ReplyDelete
  38. hao wengine wawili alioshtakiwa nao ni wazee wa mjini sijui walikuwa wasindikizaji tu.

    ReplyDelete
  39. kaka hongera sana na pole. kuwa makini wasije kupa kikombe cha babu yao ukasinyaa ka mahindi ya kiangazi kaka.

    ReplyDelete
  40. Mbele kwa mbele sasa angalia sana usije mwagiwa tindikali ya macho. Hongera mwanangu

    ReplyDelete
  41. UNABAHATI WEE MCHAGA ACHA TAMAA DOGO!!

    ReplyDelete
  42. Kova ona aibu, wakubwa walikutumia sasa umechuja na watu hawana imani na wewe tena.

    Ulianza kwa kasi nzuri ulipotokea Mbeya na mabo ya polis jamii, hili la Muro lilikuchafulia sana na kushsha hadhi yako.

    Siku hizi nikiona unaongea kwenye TV naizima kabisa. Ulivalia njuga kitu wananchi wasichokipenda.

    ReplyDelete
  43. we anony unaesema ana bahati...unasema kama nani na unauhakika na kauli yako? au ndio nyie nyie haters....haooo mmeumbuka sasa...mtu akifanya kazi yake kiukweli mnamzushia majungu.....wachache wasikatishe tamaa wengine...tutafika tuuuuu

    ReplyDelete
  44. Muro inabidi ujifunze jinsi ya kuchukua Rushwa.... sio unaomba omba kila mtu! Next tym kuwa makini manake najua huwezi kuacha... Hii umeponea ponea ungeungana na akina Babu Sea.

    ReplyDelete
  45. Hongera sana kaka angu!pole pia kwa kupotezewa muda na kuharibiwa kazi ila usijal watanzania wenzako tulikuwa pamoja nawe kwa sala atimaye ukweli umefichuka na aibu wamepata, hongera kaka Mungu ni mwema atakupa kazi nyingine usijal, tuko pamoja.

    ReplyDelete
  46. Angalia sasa wasije wakakuua kwani una malalamiko mengi na COMPASATION hio sio ya mchezo yaani anza kudai kuanzia Tanzania shs 10 billion, za usumbufu na kukuharibu kisaikologia, wakati wewe ulikuwa mchapa kazi wa hoja na chukua ukimbizi popote ulaya au marekani utapata kwa siku mbili kwani kesi yako inajulikana na nchi nzima .

    DUNIA NZIMA IT WILL SUPPORT YOU

    ReplyDelete
  47. Massawe.. najua watu wanakuita Jerry, but sisi ndugu wako wa damu tunakuita Massawe....
    Umeshinda kesi good for us and family , pole sana Mama mdogo.
    Ila you need to send message kuwa hujashinda kwa bahati you were innocent.i dont know sheria za Tanzania zikoje ila angalia kama kuna uwezekano wa kuwashitaki pia kwa kuharibia your reputation.
    Na moto mbele usisite to do what you do best report hao mamluki na walarushwa...
    Big up ...
    Your bro from Mbezi

    ReplyDelete
  48. Pesa ya walipa kodi imepotea hapo! Kesi ilikuwa baseless na ilionekana kabisa kwamba ilikuwa kumkomoa na kumzima katika kupambana na rushwa. Now they need to claim restitutation. Lazima serikali iwalipe gharama zao zote za kuendesha kesi pamoja na usumbufu, wanatakiwa kulipwa bilioni kadhaa hapo. Jerry fungua kesi dhidi ya jeshi la polisi. Huu ni mchezo mchafu kwani walijua kabisa wamebambikiza hii kesi na lazima wawalipe na pesa hii ni itatoka kwa walipa kodi au mnasemaje wanasheria hapo?

    ReplyDelete
  49. sheria ni mchezo mchafu tu ukikosea kidogo tu imekula kwako .nani aliamini Zombe angetoka salama kwenye kesi ya mauaji lakini sababu sheria ni mitego akatoka bila watu kutegemea ,Jerry rushwa aliomba hilo halina shaka kabisa amshukuru mungu wake kuwa jamaa walikosa ushahidi wa kumtia kwenye kumi na nane zao maana kule hotelini alipofanya kikao gari yake iliandikishwa namba na kwenye cctv camera alionekana akifanya kikao na bwana wage japo alimkana kuwa hamjui kabisa lakini sababu ya ugeni wa technologia yetu hakimu akagoma kwa sababu picha inaonesha ni kivuli tu na si picha halisi.ukifuatilia mahojiano ya jerry kweny globalpublisher siku alipotoka central alijikanyaga sana na kukata tamaa maana alijua wazi segerea imeshakaribia ..ushauri wangu kwako bwana mdogo jerry ulichokifanya unakijua na umeshajifunza acha tamaaa maana tamaa mbaya

    ReplyDelete
  50. sijui ukweli uko vipi lakin maana sikufuatilia kesi yenyewe ilikuwaje na kwa nini..ni kwa vile niko bali kidogo na mji ndo maana pengine nijipe moyo tu.lakin kutokana na maoni yalivyo hapa, nashawishika kusema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja...yawezekana kwa asilimia kubwa hukuwa na hatia...wabaya wako ni wale ambao walitoa maoni ulipooa wakisema utakwenda jela na wao watamtunza jennifer lakini hawajaonekana kutoa maoni hapa kwa vile ni aibu kwao, wmeonekana wawili tu hapa..imekula kwa upande wao.hongera kama ulisingiziwa na kama hukusingiziwa na umeshinda Allah ni mjuzi kwa yote..kama ulisingiziwa tunategemea utaendeleza kazi kama kawaida na tunategemea neno toka kwako kuhusu hii kesi.

    ahsante

    sm

    ReplyDelete
  51. hongera sana jerry hakuna linalomshinda mungu...usiache kusali

    ReplyDelete
  52. suala la kuomba rushwa lipo kw watangazaji wot bongo, sioni la ajabu hapa. Wasanii wa fleva kibao uonga nyimbo zao zipigwe redioni kila kukicha na ndiyo maana unaona hatuna nyimbo za maana redioni TZ kwa ajili ya kazi hii.

    ReplyDelete
  53. jamani kama ni kesi tayar imekwisha yanini majungu tena?sasa kama alionekana kwenye cctv kwanini huo ushahidi usikubalike?hata ungekuwa wewe ukipata mwanya wa kula lazma ule!kwani wangapi wanakula live na hamuwagusi?BIG UP KAKA!!IKUBALIKE tu kuwa ni aibu tena kubwa kwa mkubwa kutangaza ishu hiyo kwa mbwembweeee na mwisho kuumbuka!

    ReplyDelete
  54. WOTE WAONGO TU, MBONA MLIKUWA MNASEMA ALIKUWA NA KIHELEHELE, SASA HIVI KATOKA HONGERA, WABONGO BWANA, WANAFIKI KWELI, HONGERA MURRO

    ReplyDelete
  55. wewe anon wa wed nov 30,02:00:pm 2011 mwogope Mungu usitake upewe mtihani wa maisha ndio uamini kuwa kuna Mungu - na ndicho kitakachokupata.

    Afande Kova ushauri wangu wa bure kwako ni kwamba unapopata jambo lifanyie uchunguzi kabla ya kukurupuka, maana una udhaifu mkubwa wa kukurupuka na mwishowe unaishia kwenye aibu; kusema kweli mie nikikuona unaongea jambo kwenye TV lazma nilifikirie mara kumi kumi kabla sijalipokea - badilika kaka urudishe heshima yako katika jamii.

    ReplyDelete
  56. Kikubwa UDHALIMU sio njia sahihi...tuache utamaduni wa kutengeneza mambo kama kesi ya huyu bwana mdogo ilivyo tengenezwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...