TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari
ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge
kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge.
Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu
katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na
Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi
Desemba 31, mwaka jana, 2010.
Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria
hiyo.
Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Novemba, 2011


Tuwekee hapa hiyo sheria
ReplyDeleteHivi ni nani anawajibika kutoa na kusimamia elimu kwa umma kuhusu katiba? Tafadhalini wananchi tunahitaji kuelimishwa kabla ya kuchangia au kutoa maoni.
ReplyDeleteSasa Ankal sisi wananchi wa kawaida tutawezaje kupata hiyo nakala ya muswada je itawekwa online kwa waliombali tuweze ku-download ili tuweze kuupita na kuchangia mawazo yetu? Tunaomba utupatie majibu kabla haujaondoka ikulu tafadhali au kesho ukienda ikulu tunaomba umuulize mheshimiwa JK ni jinsi gani tutaupata huo muswada aliotia sahihi yake. Asante
ReplyDeletemgomo kesho jmatano nchi nzima Uingereza kupinga mabadiliko ya pension serikali inasema haitambui mgomo huo,sasa nani sahihi wananchi au serikali,na hiyo katiba ni kwa ajili ya nani?raisi au wabunge au wananchi majibu yanahitajika haraka.Napinga bunge la tanzania kwa nguu zote kwani ni sawa na ushabiki wa Simba na Yanga.Katiba mbovu ni chazo cha migogoro Afrika,Tanzania si kisiwa cha Amani ni sawa na Volkano inayosubiri kulipuka.Raisi kwa kusaini hayo mapendekezo ni kutojali pingamizi la wananchi na taasisi zake.
ReplyDeletehaya ndugu zangu watanzania tujiandae kwa mchakato mzima wa katiba mpya hiyo ni maliyetu sote watanzania si ya ccm wala chadema ni kwetu wananchi tujitokeze kwa wingi busara itumike sio kuzomeana hatuna utamaduni huo watanzania ubishi na majigambo sio wakati wake na kwa nn tuwasikilize wanasiasa kwa kitu chetu wenyewe?tusikubali kuyumbishwa
ReplyDeleteJUZI NILISEMA HIVI: Kikwete amekubali kuonana nao kwasababu anajua amekosea. Anajua CHADEMA wana point na wananchi walio wengi wanajua hilo. Ila amekubali kupunguza tension na ku-buy time. Ni mchezo wa kisiasa tu.
ReplyDeleteNi kama CUF kule ZNZ: sio kwamba CCM walitaka kuwa nao, ni kwamba walifika mahali wakaona CUF wanaweza wakashinda siku moja, itakuwaje?. Wakaona bora nusu shari kuliko shari kamili. Baada ya mapambano ya miaka mingi, wakasema tuunde SERIKALI YA PAMOJA. Ina maana hata CUF siku wakishinda, bado CCM watakuwa kwenye serikali. Hawatoki. Hata huku bara, siku ukiona CHADEMA wanaelekea kushinda, tegemea wazo la SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA kutoka CCM.
LEO NASEMA: Mmeelewa vizuri sasa?
Katika katiba mpya kusije kukawa na makosa ya kuongeza mda wa Rais kuwa madarakani,sheria itakayo mfanya JK arudi tena madarakani. Jamani nchi yetu inapolomoka tujihadhali!! Mabadiliko yanahitajika na waliojivua magamba hawatakiwi kurudi na wale wenye magamba hawatakiwi.
ReplyDeleteMunyonge Tanzania anaendelea kuteseka kitu ambacho hakitakiwi.
Ushikaji umezidi ktk kuiongoza nchi.
Please post the bill on this blog for us to review and provide feedback. Asante.
ReplyDeleteHivi ni kwanini cdm pekee ndio wanajifanya Watanzania halisi? wakati sisi pia ni Watanzania na sio membars wa cdm wala hatuungi mkono mawazo yao! sidhani kama hawa jamaa wana nia njema na umoja wa nchi hii, Huwezi kutawala nchi hii huku ukidharau na kuitenga jamii fulani ya Tza..Kama ukiangalia mtandao wao wa 'Jamii Forum' Watu wa maeneo na imani fulani sio watu'..jee wao sio Watz?
ReplyDeleteHiyo kitu mchakato wa Katiba ni vizuri iwekwe hapa ktk blogu ya jamii angalau kwa ucheche!
ReplyDeleteTafadhali Mdau yeyote mwenye kuweza hilo atuwezeshe na sisi!
Hivi, wanaoomba hii sheria iwekwe hapa waione, kumbe walikua wanadai marekebisho ya kitu wasichokijua?.. kwa vile tuu cdm wamesma!..acheni 'ukasuku'
ReplyDeletewadanganyika bana wanatia huruma sana elimu ndogo.....kila wanachokianzisha watu fulani ndio hicho wanachokitolea macho
ReplyDeleteswali hivi jamani wananchi ni wale viongozi pekeyao?
ikiwa kuna suala la mabadiliko inakuaje kusubiria mpaka kikundi fulani kuanzisha ndio kila mtu anatolea macho?
wakati wote mlikuwa wapi kwanini wadanganyika wa nchi nzima msiamue kuomba hayo mabadiliko wakati huo wote?
hivi wadanganyika hawawezi kujisimamia wenyewe katika kudai haki fulani au maombi fulani kwa pamoja mpaka wasikie fulani kaanza?
hivi wadanganyika wataendelea kudanganyika na kuwa nyuma mpaka lini?
hivi wadanganyika kwanini wasiwe na umoja maana wao ndio wenye danganyika yao ndio wahusika wakuu ukiachilia mbali wale viongozi wanaojishibia wenyewe?
hivi hiyo nchi ni ya viongozi pekeyao au ni nchi ya wadanganyika wote kwa ujumla?
ankali haki ya nani tena waachie wadanganyika wasome huu ujumbe unawahusu sana ni kama muswada wa katiba.