YAH: KAMATI KUU YA CCM KUMWAGIZA RAIS KIKWETE AKUTANE NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

Kurugenzi ya Habari na Uenezi imeshangazwa na tamko lililotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye kuwa “Kamati Kuu ya CCM imemwagiza Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akutane na vyama vyote vya siasa badala ya CHADEMA peke yake” aliendelea Kusema kuwa …… “Pamoja na kukubali akutane na CHADEMA, tumetahadharisha kuwa lazima kushirikisha wajumbe wengine kutoka kwenye vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe CHADEMA pekee”.


Awali ya yote tunapenda kusisitiza kuwa maridhiano ya kitaifa juu ya mchakato wa kuweza kufikia kupata katiba mpya ni suala ambalo ni la muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu na haswa kama muafaka huo utafikiwa kwa nia njema ya kujenga na kuimarisha mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini, rangi, kabila ama itikadi za vyama vyao.



Tamko la Kamati Kuu ya CCM linaonyesha muendelezo wa matamko ambayo wamekuwa wakiyatoa kila mara wanapokutana, mathalani kikao kilichopita kiliiagiza serikali kuwa bei ya mafuta ya taa lazima ishuke, kitu ambacho mpaka leo hakijafanyiwa kazi na hii inaonyesha jinsi ambavyo Kamati kuu hiyo isivyokuwa na msimamo juu ya maamuzi yake na maagizo yake inayotoa kwa viongozi wa kiserikali.



Tamko hili, limetushangaza kwani limeonyesha wazi kuwa kuna hofu miongoni mwa viongozi na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuwa sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa kushirikiana na wale wa CUF haina muafaka wa kitaifa na hivyo wanamwagiza Rais kukutana na makundi mengine ili kupata maoni kabla ya kuisaini sheria hiyo.



CHADEMA tuliandika barua kwa Rais naye alikubali kukutana nasi, kitendo cha Kamati Kuu ya CCM kutoa tamko hili ni dhahiri kuwa kamati kuu ya CCM imejitwalia madaraka ya kuwa wasemaji wa vyama vingine vyenye uwakilishi Bungeni ambao mpaka leo hatujawasikia wakitoa tamko juu ya suala hilo. Tunajiuliza hivi Kamati Kuu ya CCM leo imekuwa ndio wasemaji wa vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA?



Pili, Vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA NA NCCR-Mageuzi waliopinga muswada huu, vyama vingine mathalani CUF, CCM na TLP wao waliunga mkono kupitishwa kwa muswada huu, sasa Kamati Kuu ya CCM inataka wakakutane na Rais ili kujadili kitu gani? Wakati walikuwa ni sehemu ya maamuzi ambayo CHADEMA na wadau mbalimbali wanayalalamikia na ndio maana tukataka kuwasilisha malalamiko yetu kwa Rais.



Tunapenda kuikumbusha Kamati Kuu ya CCM kuwa CHADEMA iliomba kukutana na Rais wa Nchi na sio kama Mwenyekiti wa chama, iwapo Rais atakubaliana na agizo hili la Kamati Kuu ya CCM itakuwa dhahiri kuwa ni muendelezo wa ushahidi kuwa viongozi wa Kiserikali wamekuwa wakitimiza majukumu yao kutokana na shinikizo la Chama hata kwenye masuala ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kama suala hili la Katiba lilivyo.



Mwisho, Tungependa kumshauri Rais kuwa pamoja na kukutana na CHADEMA atenge muda ili aweze kukutana na makundi mengine mbalimbali ya kijamii yenye maoni na malalamiko kabla ya kusaini sheria iliyopitishwa na Bunge kwa maslahi ya taifa letu na ili kuweza kuleta utengamano wa kitaifa .
Imetolewa na:

Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
24 Novemba 2011.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 48 mpaka sasa

  1. Nakubaliana na chadema, na wala sina ushabiki wa chama chochote.

    Tuwe makini na maamuzi yetu ya leo tukijua tunaamua maisha ya vizazi vijavyo pia. Leo hii tunafarakana kuhusu mabadiliko ya katiba kwa sababu waliotutangulia hawakutilia maanani ukweli kwamba katiba hiyo waliyoitengeneza ingetugusa sisi pia, hasa leo hii.

    ReplyDelete
  2. Nendeni huko...mbona kipindi cha baba wenu wataifa mlikuwa mnafyata kwa kila jambo...mimi nasema wazi bila kusita wala mikwaruzo...CHADEMA ni chama cha udini...KIKRISTO...maslahi ya kanisa kwanza..msituingize ktk mabalaa..wenye akili na kuona mbali tumeshtuka..hukohuko Arusha na mbeya hapa dizim mtachemsha mbaya....chama cha kuandamana na kususasusa....

    ReplyDelete
  3. tena waendezao hasa wanataka suluhu ya nn janja yenu tumeijua raisi atasaini mkitaka kuandama au kufanya fujo fanyeni tu mtahukumiwa kwa yenu na mungu dam za watu hazitaenda bure kwa tamaa yenu ya madaraka wengine mmeisha kuwa wazee mnataka tu uraisi mtatusaidia nn mabadiriko hapo hayatatokea kamwe mnawasakizia watu wanapigwa mkikamatwa nyie mnawekewa zamana mbona walala hoi mnao washawishi waandamane wakikamatwa hamuwatolei dhamana ubinafsi mnauanza hamjaingia madarakani mkipata je

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo kwa kusema "hapa dizim mtachemsha mbaya" unamaanisha DSM ni ya ccm na baadhi...au!?. Tafakari maneno yako kabla hujaandika na kupublish kwa umma!

    ReplyDelete
  5. Kwani kuna ubaya gani akikutana na vyama vingine na kinawauma nini nyinyi Chadema?

    ReplyDelete
  6. Kwanza tumshukuru Rais Kikwete kwa kutoa hii fursa ya katiba.Kwani miaka ya nyuma haijawahi kutokea watu kupewa nafasi ya kuchangia.Hawa CHADEMA wasitake kuitumia hii fursa kwa ajili ya kutaka kujipendekeza kwa watu na kujidai wao ndio wenye kupigania.Kamamkweli wanapigania kwa ajili ya watanzania basi waache tabia za kususa.Kwanza tokea lini ukasikia vyama vya siasa vikakubaliana.Lazima wawe na heshima kwa Raisi itakavokuwa yeye bado ni kiongozi wa nchi.Na sijawahi kuona Raisi ambae amewapa uhuru wananchi wakuongea anagalau watu wanatoa madukudku yao hadarani.

    ReplyDelete
  7. kwa nini mdau unaleta mambo ya udini kwenye mambo ya kimsingi? wao wameomba kuonana na rais na rais kawakubalia. kama kuna hoja rais atasikiliza kama hawana hoja rais atawaambia, ni simple. mambo ya ukristo na uislamu yametoka wapi? wewe unaleta mambo ya simba na yanga na ubishi ubishi tu hadi leo na vibarakashia wanacheza mpira wa maneno maneno wakati mambo yanakwenda kisayansi. rais kikwete anajua na si mdini kama wewe, atasikiliza hoja na kuwajibu, wewe kakae vibarazani na kubishania majungu majungu na kufikiria jina hili la kikristo hili la kiislamu, sura hii ya kikristo, hii ya kislamu - wakati sisi tunataka mambo yaendeshwe kitaalam zaidi. we endelea na dini zako hizo na simba na yanga..

    ReplyDelete
  8. Mtoa maoni wa pili una ufinyu wa mawazo!!!

    ReplyDelete
  9. Hiyo mbona iko wazi kuwa kamati kuu ya CCM imechemka?

    CHADEMA wanamuona Raisi na si kama raisi na si mwenyekiti wa CCM.

    Hapa utaona ni jinsi gani hao jamaa wasivyotumia akili katika kutoa matamko. Na ndio maana nchi mekuwa hapigi hatua kimaendeleo kwa sababu kila anayeibuka na wazo lake hata kama ni la kijinga wengine wanaliunga mkono ili mradi tu ni mwanachama wa CCM

    ReplyDelete
  10. mimi sina msimamo na chama chochote, ila mdau wa pili anaonekana ana tatizo kubwa sana la ufinyu wa fikra na jazba.
    mungu amrehemu na kumuondolea upofu!

    ReplyDelete
  11. Mdau wa pili ni mwakilishi kutoka CCM. Hivyo ndivyo wanavyofikiri daima. Wanaogopa mabadiliko, wanaogopa majadiliano, matokeo yake ni matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi, vitisho vya al shsbab, udini usio na msinmgi. Huu ufinyu wa mawazo ndiyo uliotufikisha hapa tulipo.

    ReplyDelete
  12. Rais wa nchi alipoombwa kukutana na CHADEMA hakumumunya maneno, alikubali waziwazi, leo hii kamati kuu ya chama "inamuagiza Rais wa nchi!" huu ni ukosefu wa nidhamu na ni 'isubodination'. Kwa maelezo ya Nape (Gamba) Rais atakutana na CHADEMA kama mwenyekiti wa CCM...wengi tunamjua Nape... ni mfa maji asiye acha kutapatapa.... amani ya nchi itavunjwa na CCM

    ReplyDelete
  13. mdau wa pili,una akili finyu.sidhani kama hata mtihani wa chekechea kama unaweza kufaulu!

    ReplyDelete
  14. Haiingii akilini kwamba aliyesema 'hapa dizim mtachemsha mbaya'... maskini huenda anatoka mbagala kule vikongwe walikokutana na Mwenyekiti wa CCM Taifa juzi (PTA) wakiwa na magwanda ya chama kwa kisingizio cha rais kulihutubia taifa kupitia wazee. ajue tu maeneo nyeti kama kawe, ubungo (ukiacha maeneo yaliyochakachuliwa-Ukonga, Kinyerezi)wananchi wanajua la kufanya.

    ReplyDelete
  15. Pongezi rais wangu Kikwete kwa kukubali kukutana na Viongozi wenzako wa Chadema. Achana na mawazo mgano. Wakikupa ushauri mzuri acha hata kuisaini hiyo sheria ya Katiba Mpya. Usikubali kuwa sababu ya machafuko ya nchi hii. Sikiliza dhamira yako. wanasisiemu wenzako hawakutakii mema. wanapenda muendeleze vikao ili wapate posho. Kama Rais wa nchi toa maamuzi magumu...futilia mbali huo uswada mambo yaanze upya kwa utaratibu mzuri....

    ReplyDelete
  16. yaani kwa maneno mengine kamati kuu inamfundisha rais wa nchi kazi!. chadema wameomba kuonananae kama rais sio kama mwenyekiti. sasa iweje chama "kimuamuru"? hao wengine hawana shida na rais.Watanzania tujifunze kusoma na kuelewa vitu, tuache ushabiki

    ReplyDelete
  17. Kwanza nawapongeza CHADEMA. Vyama vingine kama vinataka kukutana na Rais na wao sio waombe? Jamani CHADEMA pekee yake imeomba kukutana na Rais sasa vyama vingine ambavyo havijaomba au havijaona haja ya kukutana na Rais kwa nini CCM inawesemea eti na wao waende? Kama wangeona umuhimu wa kumuona Rais basi wangeomba, lkn walioomba ni CHADEMA tu. Anayesema CHADEMA ni chama cah udini atafakari sana kauli zake maana nahisi ni wale wale....tujifunze kuchanganua mambo kwa mapana yake jamani. Anayesema Dar CHADEMA haina kitu anasahau kuwa jimbo la Ubungo ni la CHADEMA....tusiandike bila kufikiria jamani.

    Mswada wa awali ulikuwa kwa lugha ya kiingereza. Bunge likashauri ukaandikwe kwa kiswahili ili wananchi waweze walio wengi waweze kuuelewa. Sasa mbona wananchi hawakupelekewa hiyo version ya kiswahili ili waisome waielewe na kuitolea maoni? Imeamndikwa kwa kuswahili na kupitishwa na bunge na ikishakuwa sheria ni basi, sasa kulikuwa na haja gani Bunge kusema mswada ukaandikwe kwa kiswahili? Si wangepitisha tu ule wa kiingerea halafu baadaye watafsiri kwa kiswahili? Hivi mwananchi asiposhirikishwa kikamilifu kwenye hatua za awali, akazielewa, ataweza je kushiriki kwenye hatua za juu zaidi wakati zilizotangulia hazijui kwa sababu hakushirikishwa?

    Mungu Ibariki Tanzania...CCM mnatupeleka wapi jamani? Nguvu ya umma itaamua kipindi cha kuburuzwa kimeshapita.

    Juzi Bunge limebaini madudu Wizara ya Nishati, TANESCO walichangia milioni 40 na sasa ili waweze kufidia fedha hizo, TANESCO wameomba kuongeza bei ya umeme!!!!Watanzania tuamke jamani tunanyonywa na wachache,,,,,

    ReplyDelete
  18. Huyo mtoa maoni wapili masikini tumusamehe bure si kosa lake ni kosa la fikra zake....watu tunatoamaoni ya msingi yeye anakimbilia ukristo. Pole sana una infiriorite compleksi.

    CDMkukutana na rais ni sawa kabisa. Daima mzungumzo hujenga. Tukae tusikilize wataamua nini ktk mazungumzo yao...Wote wale nawaaminia. Kutoka rais mpaka wenyeji wake wa vyama.

    ReplyDelete
  19. CHADEMA wako sahihi,kwa sababu waliomba kuonana na RAIS na si Mwenyekiti wa CCM,pia ni kwa nini RAIS akutane na vyama vingine wakati viliunga mkono muswada wa katiba,mwisho mchangiaji wa pili ana matatizo saaaana na haitakii nchi hii mema nashindwa kuelewa swala la udini ameliletaje humu,inawezekana anawakilisha kundi la Al-Shabaab na makundi mengine yenye mlengo kama huo

    ReplyDelete
  20. kama Rais yuko makini, kama vyombo vya usalama viko makini, mjadala wa katiba Bungeni juzi ilikuwa ni aibu ya miongo mitano ya uhuru. Asilimia 87% ya wabunge (CCM na CUF) waliijadili CHADEMA na siyo muswada wa KAtiba. Kama kawaida hawakuusoma muswada wenyewe, sasa ili kumwonesha boss wao kwamba wapo wakaishia kuishambulia Chadema wakiwemo wanasheria maarufu kama Mzee wa Vijisenti!

    ReplyDelete
  21. Ushauri kwa mdau wapili. Usiangalie chama wala sura, wala dini ya mtu. Angalia lililo baya, uliache na lilo jema ulifuate. penye ukweli simamia ukweli. acha ushabiki wa kisiasa na kidini. TAIFA LIPO KWENYE KIPINDI MUHIMU, Tusilete mzaha.

    ReplyDelete
  22. CHADEMA wanaposema wanakwenda kuonana na Raisi na sio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,sasa wao wanakwenda kama nani? wabunge au chadema? kama wanakwenda kama chadema kwanini hawamtambui kua raisi kama mwenyekiti wa chama tawala? ama kweli nimeamini hawa watu ni zero...hawa ndio mnasema wakabidhiwe nchi?

    ReplyDelete
  23. msimseme sana mdau wa 2 kwani amesema kwa mtazamo wake..ni uhuru vilevile, maana na yeye ataona wewe umekosea kwa mtazamo wake...lakn wengi wape na wachache waheshimu...si mbaya wachache wape pia inapobidi na inapowezekana pia.

    waha chadema ni freemasons hawa kiukweli na lengo lao la kulazimisha madaraka...tumeshajua kuwa wanatumiwa tu na mataifa makubwa kwa lengo lile lile la freemasons kuitawala dunia. alama yao ni ileile mbili...angalia alama ya freemasons, alama ya chadema, alama ya waasi wa libya na alama ya watu wate wanaopingana na utawala uliopo utapata jibu...
    sina ushabiki wa chama mimi mpaka sasa na niliwapenda chadema mwanzo sana, lakini nimeshashtuka kuwa tunaweza kujichimbia kaburi letu wenyewe kwa hawa chadema kuwapa madaraka...hawana wanalotaka zaidi ya madaraka...mbona posho wameendelea kuzimega isipokuwa zitto tu?...MWANAHARAKATI HAPO NI ZITO TU HAKUNA MWINGINE...MNYIKA NAE ANAWEZA KUWA LAKINI AWE MAKINI ASIJE AKAJIHARIBIA MAANA HADI SASA AMEONYESHA MWANZO MZURI WA KUWA NA UPEO...kafulila wa NCCR nilimsifu sana wakati wa kampeni yake lakini kumbe alikuwa anahitaji kula tu yule, saiv kimyaaa kama kafa vile..kazi tunayo wa TZ maana bado hatujapata mkombozi.

    ahsante

    sm

    ReplyDelete
  24. MDAU WA PILI KAMA ULIENDA SHULE BASI HAIJAKUSAIDIA BIRA URUDI TENA!NA UTAKUWA HUJUI ULISEMALO MASKINI WEE NA KINACHONIUMA SANA TANZANIA WATU KAMA WEWE NI WENGI SANA HAWATAKI MAENDELEO KITAALUMA WAMEZOEA BABAISHABABAISHA TU.POLE SANA.

    ReplyDelete
  25. kuna mpumbavu analeta mambo ya dini kwenye siasa naona anataka kukanyaga moto usione watu wa ko kimya ukawadharahu dini ya Kikristo imekufanya nini kama sio unataka maneno. chama ni chama na dini ni dini.mi naona huna akili ni wale wale mnaopewa kanga na kofia na pilau mnaridhika mjinga wewe mtoa maoni wa pili fikiri kabla ya kusema sheitwani wewe, mwanaidhaya we. CDM NAKUBALIANA SANA NA NYIE 100% ACHANENI NA HAWA WATUMWA NA VIBARAKA WENYE WAUME ZAO KAMA DAVID CAMEROON

    ReplyDelete
  26. ufinyu wa mawazo mnao nyie kwa kukumbatia chama kisichokuwa na uwiano...wala kujuwa sheria..fujo tupu..mnatuwakilisha bungeni then mnasusa..sasa mnawakilisha nini kama c ujinga mtupu...kwa hiyo mawazo finyu unayowewe usiyejuwa lolote ila ushabiki na chuki uliyokuwa nayo...narudia tena...chama cha CHADEMA NI CHA KIKRISTO...utaki ndiyo hivyo usitake ni hivyo...! ushahidi tunao..mnakipigia debe makanisani na mapadri na maaskofu ndio vinara...we sema udini...na wewe c mdini?

    ReplyDelete
  27. Mdau wa pili watatu na tano tafakarini kabla ya kuandika tumia akili, halafu mjue ni kwa maslahi yenu pia esp mdau wa pili wewe kama una udini kapande mlimani upayuke maaana naona huna busara

    ReplyDelete
  28. Wooote mnaojidai hakuna udini waongoo! Na Chadema watake kumuona rais wao pekee yao wao kama nani? Wao sio serekali, na kama wanataka kumuona rais kama rais basi fursa hiyo wapewe pia vyama vingine, wamevimba kichwa kama kitu gani wajue ikitapasuka. Wao wamejaza wahuni kina Lema......mtu wa kijiweni hana busara majungu tu, huyo Sugu ndio Sugu anajisifia eti kitabu chake kinaelezea jinsi gani mtu unaweza kutoka from no where to bungeni.......yaani baada ya kuwa encourage vijana kusoma, kujiendeleza anawaambia inawezekana kutoka kijiweni hivi tu ukawa mbunge kama ilivyokuwa kwake........ndio maana chama chao kitaendelea kuwa chama cha fujo maana hawakusoma hawawezi kujadili kwa hoja.

    ReplyDelete
  29. Amrehemu kafawaombee nduguzo walifarikiiiiiiiii mda mwingi.Kwa nini wakatae vyama vingine? Kweli chedema Hakifa katika nchi Hii yaani hawa wanatakiwa wangekuwa kuleeeee kuzimuuuuuuuu dini dini dini dini imewatawala nyamafuuuuuuuuuuuuuuu na mtashindwa daima. Mlitoka bungeni mlitegemea nini?????? tumeawachagua mkatuzarau ningejua mie hata kura yangu ninge itupa hata mtoni ikachukuliwa na maji kule, mnakera sana mnatoka baadala ya kutetea yaliyokuwa ya muhimu na kupinga ambayo hamyakublia eti mnatoka nje yaani ningekuwa na uwezo mie basi tu chadema mnauudhi sana hata udini unatawala chama chenu hicho CCM, CUF, TLP, NA vyamna vingine tuteteteeeeni haya yaondoke zao kule wameniuzi kama nini. Niliacha kazi zangu nachagua chadema kwanini??????? yanapenda VUFUGU KA NINI WATU AU MIZIMU HAWA JAMANI MUNGU TUNUSURU NA CHADEMA maana na wengine wanakojotwaaaaaa tu

    ReplyDelete
  30. Mdau wa pili umechemsha asee, fikiri kwanza kabla ya kuandika. Jamani tujifunze kujadili "POINT ZA MSINGI"B katika hili kinachoongelewa ni "KUKUTANA CHADEMA NA RAISI" basi tujadili hilo na kuachana na mambo ya Udini, Rangi na Ukabira. Hakika hatutafika popote kama hatuzingatii haya, badala yake tutakua tunapotosha watu na kutoka ktk mada ya msingi. Tuelimike jamani loh!.

    Mdau.

    ReplyDelete
  31. Acheni woga, ukiritimba na kujitafutia sifa za bei poa, kuna tatizo gani kwa vyama vingine navyo kukutana na Raisi na kutoa maoni yao juu ya hiyo katiba? Katiba ni uchochoro ambao mmeupata kuendelea kuvuruga, na hapo hamna suluhu mpaka mpewe hiyo katiba ili muitunge wenyewe!

    ReplyDelete
  32. Mimi kama nilimuekewa Rais vizuri katika hotuba yake basi naona hakuna haja ya CHADEMA kuhofia chochote maana alisema yeye atapokea mawazo ya vyama vyote na kuyawasilisha katika tume ya katiba atakayoiunda.Pia akawaomba CHADEMA wawasilishe maoni yao kama walivyofanya CUF so naona CDM wamekubali kuwasilisha mawazo yao kwa kukutana naye,hivyo na wawe CDM peke yao,hivyo vyama vingine viombe kwa muda wao pia.Hii ndiyo demokrasia ambayo inatakiwa tuifwate mara zote,kuandamana kwa kivuli cha nguvu ya umma huku watu wanauawa sidhani kama ni mbadala ktk kila jambo.Kinachoniudhi huwezi sikia hata mwenyekiti wa tawi wa chama kaumia katika hizo vurugu but always poor civilian.Let's change,this is the perfect way of solving problems!!

    ReplyDelete
  33. Afu mnauliza kwa nini Tz masikini. Tutabaki hivi hivi. Wenzetu Ghana wanaotegemea mali asili kama sisi tayari ni middle income country,. Sisi tuendeleze maslahi binafsi mbele tuendelee kuwa wa kwanza kwenye umatonya.Hii Katiba si ya CCM wala CHADEMA wala Rais ni kwa manufaa ya wananchi na nchi. Kwa nini watu mnakuwa SELFISH???? I hate some of Tanzanians. Mnanifanya nijutie Utanzania wangu.

    ReplyDelete
  34. MTOA MAONI WA PILI NI MGONJWA WA AKILI NAMJUA MIMI HUYO ALITOROKA MILEMBE ANATAFUTWA MUONEENI HURUMA SANA.

    ReplyDelete
  35. Mchangiaji wa pili nafikiri una ufinyu wa mawazo na unaleta mambo ya udini katika jambo kama hili la katiba, Nakupa pole sana.

    ReplyDelete
  36. Kwa kweli mdau umeongea jambo zuri. Ubinafsi unatusumbua sana. Ila kwa hoja ya CHADEMA kutakiwa wamuone raisi wakiwa na vyama vingine haina mantiki yoyote. Kwa sababu vyama vingine havijaona tatizo kwenye hicho kilichopitishwa bungeni. Sasa kwanini watakiwe kumuona raisi eti kwa vile tu chadema wametaka kumuona raisi? Hapo CC imechemka kubalini tu. Halafu wanamuagiza raisi akutane na vyama vyote. Wao ni kama nani kwa raisi. Hilo sio suala la chama ni suala la kitaifa. kwa hiyo chadema hawaendi kumuona yeye kama mwenyekiti wa ccm bali raisi wa jamhuri. Ubinafsi hapo ni wa ccm peke yake na wala sio chadema. Labda NCCR nao waombe kuungana na chadema kwani walishaonesha tangu mwanzo kuwa hawaungi mkono hiyo rasimu ya kutengeneza katiba.

    ReplyDelete
  37. Mdau wa pili ameniudhi kupita maelezo anafanya dini yetu ya kiislam inaonekana kuwa na wajinga wengi kumbe ni wachache tu wenye mawazo finyu,na hii imesababishwa na kwenda vyuo vya kusoma kuanzia kushoto kwenda kulia badala ya kwenda vyuo vya taaluma.

    ReplyDelete
  38. Anonymous wa saa 03:21:00, 12:56:00 na 12:06:00 hamna fikra, mnaandika tu kwa vile mna access ya internet, lakini hamna upeo.

    Msitangulize ushabiki bila kuelewa walichoandika CHADEMA. Wanaukweli. Kama vyama vingine walikubali CCM wanawashurutisha kwenda kuonana na Rais kwa nini? CHADEMA wamemwomba Rais kama mkuu wa nchi siyo kama mwenyekiti wa Chama, CCM wanasema wanamruhusu na eti na vyama vingine waende!!! Kuna maantiki gani??

    Mwacheni Rais afanye mambo ya Serikali kwa kofia ya Serikali, na siyo kila kitu kuingiza chama.

    Mamobo ya Serikali yawe ya Serikali na ya Chama chake yawe ya Chama chake.

    ReplyDelete
  39. Hata mimi najutia Utanzania kwa fikra finyu za baadhi ya WaTZ. Yaani watu wanakurupuka tu kupinga na kushabikia bila kufikiri kwanza. Hivi wewe mwandishi wa pili umelogwa nini!!! Nakushangaa sana. Halafu haya mambo ya udini udini yatawafikisha wapi??

    Hutapata madaraka kwa kuvaa barakashia au kujigamba juu ya udini wako bali kwa kutimiza vigezo. Unakaa kufikiria huyu mkristo, huyu muislamu mpaka lini?

    Tujenge nchi yetu kwa umoja wa Utanzania wetu, siyo kwa fikra za kidini au kiitikadi.

    ReplyDelete
  40. Wala sishangai kwanin Tanzania ipo hapa tulipo maana hapa tatizo liko wapi,ni sawa na kumwambia mtu nenda kanywe maji wakati hana kiu, kama vyama vingine havikuliona hilo iweje NEC ndo wajifanye wameliona na hao wataenda ongea nin kama hawana cha kuongea!na katiba si ya chadema na mawazo yao kimsingi si mabaya inakuwaje kuna baadhi ya watu wanaufinyu wa mawazo wanathubutu kusema ukristo au uislam yametoka wapi bila aibu anasema janja yenu tumeijua looh huu u ccm na uchadema utatupeleka pabaya kama ccm wana wazo zuri wapongezwe na chadema vivyo hivyo wote ni watanzania

    ReplyDelete
  41. CHADEME NDIO WALIOMBA KUONANA NA RAIS VYAMA VINGINE HATUKUWASIKIA JAMANI IWEJE LEO KAMATI KUU YA CCM IWASEMEE?JAMANI TUFIKIRINI TENA MDAU WA PILI KAA CHINI NA UFIKIRI TENA NDUGU JAZBA NA HASIRA HAZITATUFIKISHA POPOTE

    ReplyDelete
  42. nilidhani ni chama cha maendeleo nikahamaiska, ila nimekuja kuona hakuna lolote. Kususia sehemu amabayo wangeongea wasikike ina maanisha nini, kuhamasisha maandamano ni kurudishana umasikini, niache kazi zangu nikaandamane kwa sababu ya kijinga tu hatuwezi kufika popote. wananchi tupime, wao wanalipwa kwa kazi ya siasa, kuandamana na kuhutubia wanakuwa kazini, wewe unaacha duka lako, kazi ofisini, kulima ukaandamane, au unafunga ofisi, duka, shamba ili wahuni kwenye maandamano wasipore. kuandamana kwa misingi sahihi inaruhusiwa, sasa kuandamana kwa sababu ya katiba amabayo hata wananchi hawajaanzxa kujadili ndio nini sasa, eti mswada usomwe mara ya 1 na sio mara ya pili, to me its nonsense!

    ReplyDelete
  43. Mimi naona chadema wanatupotosha na kutuvurugia amani tuliyonayo. baadhi ya wabunge na viongozi wao walichaguliwa vile wana uwezo wa kuongea, kutukana viongozi walioko madarakani! sasa kama Lema ana point gani ya kuleta maendeleo? kama sio kuchafua waarusha na kuendeleza kote nchini. nawafagilia wabunge wa chadema wanaokuwa wapinzani ila wakitoa point za kitaifa wakiwemo Zitto, Halima mdee, Mbowe, kamnyika nako sometimes yes ila sometimes kanakomaa na upinzani usio na tija ya kitaifa!! pia wa NCCR wako sawa japo walipotoka kususia mjadala wa katiba. akarudi mmoja akasema akasikika, na hio ndio demokrasio sio wasusiaji!

    ReplyDelete
  44. Dah!! Natamani kumsikia Nape baada ya Lowassa kumwaga sumu Dodoma. Sisiemu hoyeee!!!

    ReplyDelete
  45. ktk mfumo wa siasa dunian kiongoz wa nchi lzm atokane na chama cha siasa ilo halina ubishi na halipingiki.kwa iyo chama kwanzandio maana wananch wa arusha walichagua madiwani wao lknkwa utashi wa chama cha chadema kiliamua kuwanyima haki ya wananch wa arusha kwenye uwakilishi ktk mabaraza ya ya madiwani kwa kile kinachosemwa masalahi ya chama kwanza mtu baadae.kwa iyo cc ya ccm ina haki ya kutoa maagizo kwa mwanachama wake kwa maslahi ya chama ukizingatia hao waliotoa ombi ilo walisusia kikao halali cha bunge.na cha ajabu na cha ajabu hata iyo kamat iliyoteuliwa imeshindwa kuona umuhim wa wanawake ndani ya chama.kwa kuendeleza mfumo dumu mana hakuna hata mwanamke mmoja ktk iyo kamat ya kumuona rais kwa iyo lzm mlijue rais hawekwi na familia yke anawekwa na chama

    ReplyDelete
  46. Cha kuchekesha kuna siku walisusa kumsikiliza alipokuwa anazindua Bunge....hahahaha leo hii mnamuomba kumuona, muongee nae, si hamkumtambua siku ya kwanza iweje leo? najua hii ni political game na JK ameshashtukia mnataka kujustfy maandamano yenu...eti tulienda kuongea nae tunamuambia hakutusikiliza ...sasa tunaenda kumshtaki kwa wananchi...nalitabiri hilo kutokea

    ReplyDelete
  47. JAMANI WATZ WENZANGU. NINAWAOMBA SAANA. MUDA HUU TUUTUMIE KWA KUJADILI MAMBO MUHIMU. TUUONE KAMA MUDA MFUPI NA NYETI. KWELI KITAKUJA KIPINDI AMBACHO TUTAJUTA, MAANA MULANGO WA KUJADILI HAYA YOTE UTAKUWA IMEFUNGWA!UMEFUNGWA SIYO NA MTU, BALI NA HALI YENYEWE.
    SISI WOTE NI WATOTO WA MWALIMU. ALITUACHIA MWONGOZO. NI KWELI KUWA DUNIA INABADILIKA, NA MAADUI TOKA NJE WANATUNYEMALEA KILA KUKICHA LAKINI KWA BUSARA ALIZOTUACHIA MWALIMU TUNAWEZA KUSIMAMA IMARA. TUNAWEZA BADILISHA KUTA NA PAA YA NYUMBA YETU, LAKINI MSINGI UKABAKIA PALE PALE. TUNAWEZA KUKUMBATIA MAADILI HAYA? KWA MFANO:

    1. TAIFA LETU HALINA DINI
    2. SISI SOTE NDUGU
    3 HAKI ITAWALE
    4. RUSHWA MWIKO
    5. IKULU PATAKATIFU
    6. PASIWE NA UNYANYASAJI WA AINA
    YOYOTE
    7. PESA SIYO MSINGI WA MAENDELEO
    8. MOYO WA KUJITOLEA
    9. NK.

    MDAU.

    ReplyDelete
  48. Huyo mtoa maoni wa pili asituchukulie muda sana. Nadhani amesikia, na amejifunza maana nae ni mwanadanu.Makosa ni sehemu ya ubinadamu. Mimi ni mkristo lakini ninaamini kuwa dini kuu tatu hapa duniani zimeleta majanga na machungu mengi kuliko neema. Ninaomba nieleweke kuwa ninaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, ila waliotuletea dini hizi pamoja na wapambe wao wanatuvuruga sana na kutugawa. Na kwa uhakika kesho kiama ndiyo yatakuwa maskani yao ya milele.
    Tuendelee na katiba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...