Bismillahir Rahmanir Rahiim


KUMB: KKHWT/WMN/1/011
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
S.L.B 2217 Dar es Salaam Tanzania.

YAH: TAHADHARI KWA TANZANIA KUTUMIWA NA MAREKANI DHIDI YA UISLAMU KATIKA SUALA AL-SHABAB

Ndugu Waziri Tarehe 16.11.2011 ulikutana na vyombo vya habari. Lengo ilikuwa ni serikali kutoa tahadhari ya uwezekano wa nchi kushambuliwa na wapiganaji wa Al-Shabab wa Somalia. Wiki tatu kabla, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania naye alitoa tahadhari kama hizo. Katika suala la majeshi ya Kenya kuivamia Somalia Serikali ya Tanzania ilipongeza hatua hiyo.

Sababu zilizo tolewa na serikali katika tahadhari hiyo ni 5:
1. Al-Shabab ni magaidi.
2. Al-Shabab wameshambulia Kenya mara 3.
3. Watanzania wanadhaniwa kujiunga na Al-Shabab
4. Tanzania imekamata ‘wahamiaji haramu’ kutoka Somalia.
5. Al-Shabab wamesababisha ukosefu wa ajira Somalia na hatimaye vijana
wamechagua ugaidi kama ajira

UKWELI KUHUSU AL-SHABAB NA SOMALIA.

Ndugu Waziri, Somalia ni nchi huru katika nchi za bara la Afrika.
Somalia ni nchi ya Waislamu kwa asilimi 99.
Kama zilivyo nchi nyingi duniani, imepita katika kipindi cha amani na vita.
Tafauti zinazoendelea Somalia ni tafauti za ndani na za kiutawala.

Somalia imekuwa na mpishano mkubwa wa utawala kama zilivyo nchi nyingine.Utawala ulio muhimu kwa muktadha wa sasa wa Somalia ni ule wa Rais Mohammed Siad Barre. Yeye aliongoza kwa kufuata siasa za mrengo wa magharibi mpaka alipoangushwa mwaka 1991. Utawala uliofuatia zilikua tawala za Koo. Tawala hizi ziliondolewa na Utawala wa Mahakama za Kiislamu. Utawala huu wa Kiislamu ambao uliripotiwa na mashirika ya kimataifa kurejesha amani kwa kiasi kikubwa katika maeneo kadhaa ya Somalia, ulidhoofishwa na mashambulizi ya majeshi ya uvamizi ya Marekani na Ethiopia. Ni kwa muktadha huo wapiganaji wa Somalia walijipanga upya kwa anuani ya Al-Shabab kulinda nchi yao dhidi ya uvamizi na kuendeleza utawala wa Kiislamu ulio asisiwa na Mahakama za Kiislamu.

UREJESHWAJI WA AMANI SOMALIA

Katika hali inayoendelea Somalia, baadhi ya mataifa ya nje yalijipa jukumu la kuunda serikali mezani kwa kushirikiana na baadhi ya wasomali. Hatimaye serikali hiyo iliyoundwa nchini Kenya imepelekwa Somalia kwa msaada wa majeshi ya nchi hizo na kutangaza kuwa ndio serikali halali kwa wananchi. Matarajio yenye dhamira njema,yalikuwa ni kuona Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na wengineo wakiunga mkono
amani iliyoanza kujitokeza Somalia chini ya Utawala wa Mahakama za Kiislamu.

Vilevile kupinga uvamizi wa Marekani na Ethiopia dhidi ya taifa huru. Matarajio mengine makubwa ilikuwa ni kuona mataifa na makundi yenye sifa ya uadilifu,yakielekea Somalia kutafuta amani kwa njia ya mazungumzo. Kigezo kikubwa kikiwa ni ridhaa ya wananchi walio wengi kwa mfumo wa utawala wanaoutaka wenyewe.

SIO HALALI KUIVAMIA SOMALIA.

Somalia ni nchi huru ni dola ya wasomali wenyewe. Marekani bila ya ushahidi wa kisheria ndio walioanzisha propaganda za kuwahusisha mahasimu wao wakubwa Al-Qaida na Mahakama za Kiislamu na Al-Shabab nchini Somalia. Hatimaye Marekani ikaivamia kijeshi Somalia mpaka leo.

Katika hali ya kushangaza na inayo thibitisha ile dhana ya mataifa makubwa kufikiri kwa niaba ya mataifa ya Afrika, nchi za Burundi, Uganda, Ethiopia na hivi karibuni Kenya, nazo zimepeleka majeshi Somalia kwa tuhuma zile zile za Marekani. Mataifa hayo pia yanalazimisha kukubalika serikali iliyoundwa Kenya. Tanzania kwa upande wake ikijihusisha na mafunzo ya kijeshi kwa serikali iliyoundwa Kenya.

Ndugu Waziri jambo lingine la kuzingatia hapa ni kwamba, takriban nchi zote zilizo peleka majeshi Somalia, hazina amani katika nchi zao kutokana mashambulizi ya vikundi vinavyopinga serikali zao. Ajabu ya Mungu majeshi hayapelekwi katika nchi hizo kupambana na wapinzani wa serikali kama inavyofanywa kwa Somalia.
Ndugu Waziri, hatua hizi za Marekani na wapambe wake sio halali kwa kipimo chochote cha ukweli, utu, sheria, au hatua za kutafuta amani. Kwa muktadha huo utaona wasomali chini ya Al-Shabab wana kila sababu za kupambana na majeshi haya ya kigeni ima iwe ndani au nje ya Somalia na kufanya hivyo sio ugaidi bali ni hatua muhimu katika kulinda sio tu uhuru wa nchi yao bali uhuru wa Afrika nzima.

TANZANIA ISIJIINGIZE KIJESHI SOMALIA

Pia isiwadhuru raia wake kwa propaganda za ugaidi.
Katika magereza yetu Tanzania wafungwa wana ‘vyeo’ visivyokuwa rasmi. Moja ya vyeo hivyo kinaitwa ‘kiherehere”. Huyu ni mfungwa ambaye ana tabia ya jambo lisilo muhusu kabisa lakini atajitahidi mpaka na yeye ahusike. Katika suala la Al-Shabab Tanzania inajitokeza kama ‘Kiherehere’.

Viongozi wa serikali ya Tanzania wanawashambulia Al-shabab bila hoja za msingi. Hoja za viongozi ni hizi zifuatazo: Al-Shababu ni magaidi, Al-Shabab wameshambulia Kenya,Watanzania wanadhaniwa kujiunga na Al-Shabab, Tanzania imekamata wahamiaji haramu kutoka Somalia, Al-Shabab wamesababisha ukosefu wa ajira Somalia na hatimae vijana wa wamechagua ugaidi kama ajira. Hoja hizi hazina mashiko.

Kwanini tupewe taarifa za wale tu wanaokwenda Somalia na sio kwengineko?. Na kama mtanzania shida yake imempeleka Somalia kujiunga na Al-Shabab iweje kosa liwe la Al-Shabab?.

Suala la nchi jirani kushambuliwa ni suala la ndani la nchi husika na aghlabu nchi zote tunazo pakana nazo zina matukio kama hayo. Mbona serikali ya Tanzania haijajitokeza kuvalia njuga mashambulizi ya kikundi cha Lord Resistance Arm kinacho uwa maelfu ya raia Uganda?. Mbona hatuja laani harakati za Mungiki wa
Kenya?. Maimai wanapambana na serikali Kongo na huko Burundi na Rwanda nako kuna matukio kama hayo kila siku. Tanzania kama nchi inatakiwa kuimarisha ulinzi wa mipaka yake na matukio katika nchi jirani hayapaswi kubadilisha sera za ndani na nje ya nchi.

Hili la Tanzania kupokea wahamiaji wa kivita ni utaratibu wa kimataifa. Mwaka 2001, serikali ya Tanzania, ilipofanya mauwaji makubwa dhidi ya raia kule Pemba,Somalia kama nchi iliwapokea wakimbizi wa Tanzania. Wakimbizi hao mpaka leo wako Somalia wanatunzwa. Vipi wakimbizi wa Somalia wawe tishio kwa Tanzania
na wakimbizi wa Tanzania wasiwe tishio kwa Somalia?. Katika kuthibitisha kuwa wakimbizi ni utaratibu wa kawaida, mwezi huu, Wakongo wakiwa na silaha za kivita wameingia na kupokelewa nchini mwetu. Ndio maana wananchi hawaja tahadharishwa wasiwasi wa nchi kuvamiwa na magaidi kutoka Kongo.

Ndugu Waziri, historia sahihi ya kuzaliwa Al-Shabab tumegusia huko nyuma. Suala la kukosekana kwa ajira kwa vijana wa Somalia hayo ni mambo ya kawaida kwa nchi maskini. Na kama ni kweli ulichosema, zingatia miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni Tanzania. Je ni sahihi kusema
moja ya viashiria vya kutokea ugaidi Tanzania ni serikali kushindwa kukidhi ajira kwa vijana?.

Hoja nzito mnayoitoa katika kuwashambulia Al-Shabab ni ugaidi. Hivi kweli Tanzania mnao ushahidi wa kisheria unao thibitisha kuwa Al-Shabab ni magaidi?. Au bwana mkubwa Marekani akisema Al-shabab au kikundi fulani ni magaidi basi huo ni ushahidi tosha kwa Tanzania?. Hivi siku moja Marekani akiwageukia
wakatangaza kuwa Chama kinachounda serikali CCM ni magaidi, mtakua na uso gani wa kuwaambia raia kuwa walichosema Marekani ni uongo?.

Ndugu Waziri kwa jinsi mlivyojitokeza katika suala hili wasiwasi wetu mkubw na huenda tayari Tanzania imeburuzwa na Marekani na sasa mnatafuta uhalali wa kupeleka rasmi majeshi Somalia. Tunatumia fursa hii kuwatahadharisha na kuwashauri muachane kabisa na agenda zinazoweza kuitumbukiza nchi katika
madhara makubwa yasiyokuwa ya lazima. Kama mmepeleka majeshi Somalia yarudisheni na kama hamjapeleka msipeleke. Aidha raia wasitiwe misukosuko kwa sababu tu ya kuwaridhisha wakubwa.

MSIMAMO WA WAISLAMU KUHUSU AL-SHABAB

Hawa ni walinzi na wapiganaji wa Kiislamu walio tangaza wazi dhamira yao ya kulinda uhuru wao na kusimamisha mfumo wa utawala wa Kiislamu nchini mwao. Msimamo huu ni agizo la Qur’an Tukufu na historia inathibitisha Mtume wetu Muhammad (SAW) alitekeleza agizo hili kwa ufanisi mkubwa. Hatua yoyote ya kuwashambulia Waislamu wenye msimamo kama huu, hayo ni mashambulizi ya kiitikadi dhidi ya Uislamu na Waislamu wote duniani.

Serikali inapaswa kufahamu kuwa sehemu kubwa ya raia wa Tanzania ni Waislamu,tena wanao fahamu na kufuatilia kwa makini sera na siasa za ndani na nje za Tanzania.

Ndio maana tunawapa nasaha kwamba, kama ambavyo serikali ya Tanzania haikutangaza uadui na Rais Frederick Chiluba alipotangaza Zambia kuwa dola ya kikristo, na kama ambavyo haikutangaza uadui na kikundi cha Lord Resistance Arm kinachodai kutaka kusimamisha utawala wa Kikristo Uganda, na kama ambavyo haikutangaza uadui na Tume ya majeshi ya Kanisa nchini Tanzania, basi vile vile hapashwi kutangaza uadui na Waislamu wanaojitetea na kulinda utawala wa Kiislamu tena nchini Somalia.

SHERIA YA UGAIDI TANZANIA

Ndugu Waziri utakumbuka mwaka 2002 Tanzania ilijadili muswada wa sheria iliyodaiwa ya kupambana na ugaidi. Bila shaka ulishuhudia upinzani mkali kutoka kwa makundi muhimu yakiwemo ya Waislamu, wanasiasa na wanasheria bobezi. Moja ya sababu zilizopelekea kupingwa kwa muswada huo ni kufanana kwa 99% na ule uliounda sheria ya ugaidi ya Marekani. Sheria ya ugaidi ya Marekani haina uhuru kwa watuhumiwa wala ukomo kwa watendaji wanapo shughulikia kinachoitwa ugaidi.

Muswada huo pia ulikuwa unashughulikia makosa na adhabu ambavyo tayari vina shughulikiwa na sheria zilizopo. Kilicho watisha walio wengi ni kuwagawa watanzania kwani muswada ulikuwa unatazama hisia za Kiislamu kama ushahidi tosha wa makosa ya ugaidi kwa mtu, taasisi au jamii fulani. Na mwisho wa yote ilibainishwa jinsi sheria hiyo itakavyo pingana na Katiba ya nchi na vilevile kujenga fursa kwa mataifa makubwa kuingilia mambo ya ndani na kuvifanya vyombo vya usalama kuwajibika katika kulinda usalama wa mataifa hayo dhidi ya mahasimu wao. Pamoja na yote hayo,hatmae Desemba 14, 2002, Rais aliekuwepo madarakani alisaini muswada huo na kuwa sheria ya nchi. Toka kupitishwa kwa sheria hiyo Waislamu hapa nchini wamekuwa wakihujumiwa na kupata madhara makubwa.

RAIA NA PROPAGANDA ZA AL-SHABAB

Tayari serikali ya Tanzania imeanza kuwakamata Waislamu kwa tuhuma za kujihusisha na Al-Shabab. Kabla ya hapo imekuwa ikizuwia shughuli mbalimbali za Kiislamu kwa tuhuma hizo. Watanzania wenye asili ya kisomali wanapekuli na kudhalilishwa na vyombo vya dola sehemu mbalimbali nchini. Serikali pia imekuwa ikizuia shughuli za vyama vya kijamii kwa madai ya uwezekano wa shughuli hizo kutumiwa na Al-Shabab.

Pamoja na muelekeo tuliouona huko nyuma lakini yaelekea kuna hujuma kubwa iliyoandaliwa nyuma ya pazia hili la ugaidi wa Al-Shabab dhidi ya baadhi ya raia wa Tanzania. Tunatahadharisha serikali isijiingize kabisa katika agenda za kidini za kitaifa au kimataifa. Ichukue tahadhari kubwa kwa mashinikizo na masharti ya mataifa makubwa ikiwemo Marekani.
Imetolewa na:

Sheikh
Ponda Issa Ponda
KATIBU

Nakala:
1. Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisia za Kiislamu (T)
2. Shura ya Maimamu Tanzania
3. Wanazuoni wa Kiislamu (HAY-YATUL-ULAMAA)
4. Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
5. Jumuiya ya Uamsho (JUMIKI) Zanzibar
6. Wanataaluma wa Kiislamu (TAMPRO)
7. Idara ya Usalama wa Taifa
8. Mabalozi
9. Vyombo vya Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 48 mpaka sasa

  1. HIVI HUYU PONDA NI NANI HASA?ANAOGOPWA NINI?Sasa Watanzania tumejua wazi kuwa Ponda ni moja wa makamanda na washauri wa al-shabab.Tujifunze kwa wenzetu Nigeria,makanisa yamechomwa kwa kisingizio hicho hicho cha Dini.Dini inayohubiri kuua kwa sababu za kutetea Mungu,nayo ni ya Kishetani,narudia ni ya Kishetani na ina laana ya Ugaidi.
    Ponda umepotoka na utajuta kama huna washauri basi Hamia somalia huko na wewe ukapiganie mola wako.

    ReplyDelete
  2. sawa kama hao Al Shabab ni watu wema na lengo lao ni kulinda nchi yao mbona wanavamia Kenya na Uganda na kuuwa wasio na hatia? Tujiulize hii dhana ya victimhood isiyo na mwisho itatupeleka wapi wakati wasio na hatia wanaendelea kudhurika

    ReplyDelete
  3. NENDENI MKAITAFUTE ELIMU HATA IKIWA UCHINA.Waislamu tumeusiwa hivyo Elimu ni jambo muhimu sana.Sasa kwakuwa utawala wetu hauna dini(PAGANI)unakuta baadhi ya viongozi wetu hawana elimu ya lugha,hawana umuhimu wa kusoma kiarabu kwakuwa hatoitumia lugha hii sababu Quraan Tukufu siyo muongozo wake.kwa hiyo akiskia Al-shabab akaipa tafsiri ya ugaidi tu kwakuwa ni neno la kiarabu.Jamani Al-shabab ni neno katika lugha ya kiarabu likimaanisha kijana,yaani ni wale vijana balekhe tayari wenye nguvu wanaoweza kujiunga na jeshi ama chombo chochote cha usalama ima kuwe na vita ama katika kulinda amani ya nchi yao.Mashabab wako duniani kote iwe Roma au Dodoma.hata vita ya kagera nyerere alihamasisha mashabab wajiunge jeshi kukomboa nchi.Sasa unakuta hao freemasons huko nyumbani hawana kazi maofisini au wanawashwa na vita wanaona silaha hazitumiki zinawekwa mpaka zinaexpire zinaripukia watu kule gongo la mboto wanaanza kuwachokonoa wasomali waacheni na nchi yao jamani.wale wanapiganaga toka miaka ishirini iliyopita waacheni nyi muwachokoze tu watakuja wasamalue Dar-es-salaam hiyo kwa dakika tano na ndiyo vitega uchumi vyote viko hapo dakika tano nchi hamna.vitega uchumi vyenyewe viwili hivyo toka 61 vikipotea muhesabu miaka 100 kupatikana tena maana siku hizi kila mtu anategeshea nyumbani. kwake

    ReplyDelete
  4. Mbona wanateka meli kama wao ni watu wazuri? Tunaumia bidhaa kupanda bei kwa sababu meli zinatekwa na hivyo ili kufidia inabidi tuumie hata tusiokuwa na hatia. Umesikia Lords Resistance Army wakiteka meli? Umesikia wakilipua mabomu hovyo?

    Kupekuliwa wasomali ni sawa kwa sababu wanakuja na mabomu. Hawaaminiki. Wanalipua hata wasiokuwa na hatia. Mungu gani huyo anayewatuma muuwe watu wasiohusika? Ugaidi ni ugaidi tu hata kama umepitia kwenye ukristo au uislamu.

    ReplyDelete
  5. Kusema Tanzania ina Waislamu wengi ni uongo, angalia hesabu za kawaida mikoa yenye idadi kubwa ya watu ni ya Kikristo mfano

    1. Mwanza about 3.5 mil.
    2. Shinyanga 3 mil
    3. Mbeya 2.2 Mil
    4. Kagera 1.7 mil
    5. Arusha 1.7 mil
    7. Kilimanjaro 1.6 mil
    8. Iringa 1.7 Mil
    9. Rukwa 1.6 Mil
    10. Tabora 1.8 Mil
    11. Mara 1.4 Mil

    Sasa angalia ile yenye wakazi wengi wa kiislamu

    1. Zanzibar yote about 1 Mil
    2. Pwani 1 Mil
    3. Lindi 1 mil
    4. Mtwara 1 Mil
    5. Tanga 1.3 Mil
    6. Kigoma 1.5 Mil

    Utaona mikoa inayobaki ukito Dar amboa waislamu wanaweza kuzidi kidogo mingine yote wakristo wazidi kidogo; mikoa hii ni Ruvuma, Dodoma, Singida.

    Huu ni upotoshaji mkubwa, hata makabila makubwa karibu yote ni Wakristo, mfano

    1. Wasukuma about 8 Mil
    2. Wanyakyusa 1.3 Mil
    3. Wachaga 1.2 Mil
    4. Wanyamwezi 1.4 Mil
    5. Wafipa 1.2 Mil
    6. Wanyalukolo 1.3 Mil

    ReplyDelete
  6. Anoy wa kwanza...
    Maisha tunayoishi leo tunaongozwa na propaganda ambazo zinakubadilisha mawazo na kuwa ktk upande tofauti na ule ulio na usahihi.

    Kwa hakika kuvamiwa kwa Kenya na Uganda hakuna ukweli kama ulivamiwa na Al-Shabab ama ulitumika na serikali wenyewe kwa njia ya kushirikiana na wamarekani ili wapate sababu ya kuipiga Somalia.

    Ukweli ni kwamba Waafrica wengi wanapenda kuburuzwa ama wanatamani ukoloni wa wazungu urudi mbali na mali asilia zinavyochotwa bila raia kufaidika chochote.

    Waafrica wanatakiwa waungane na kulinda mipaka ili kuzuia silaha haramu.Na vilevile Africa ilitakiwa kuwapatanisha wasomali pamoja na nchi nyingine zote zenye vita ili kijenga Africa kwa ujumla.
    Sio leo hii tunapangiwa maisha na nchi nyingine kwa kutumia jeshi letu na kuwaingiza wananchi wetu ktk matatizo.Kuna mifano mingi inayoendelea kutokea hapa duniani na ni vizuri kutafuta ukweli na sio kwasababu pengine huipendi dini ya Kiisilamu ndio watakachosema ni waongo.No waisilamu tunaonewa sana hapa duniani na tunauliwa sana duniani kwasababu tunapinga ushetani.Kwa sababu kuua ni ushetani hata kama ni muisilamu anaua watu bila ya hatia pia na yeye ni kama shetani.

    ReplyDelete
  7. iNAONEKANA WADAU WANA AGENDA ZA SIRI KUWATETEA HAO WAUAJI.
    IKILAZIMIKA TZ ITAVAMIA TU, KWANI TZ HAITISHWI NA MTU YEYOTE AWE KINYAMKELA AU NINI.
    IDI AMINI TULIMUONDOA, MTU YEYOTE ANAYEONEKANA HATARI YA AMANI KARIBU NA MIPAKA YETU LAZIMA TUWAJIBIKE PIA.
    HAO NI MAJAMBAZI TU WALIOKOSA UBINADAMU.

    ReplyDelete
  8. IPO KAZI KWELI,SISI WAISLAMU TUNAHITAJI ELIMU.TUNAHITAJI TUTOFAUTISHE UISLAMU NA VIKUNDI VYA KIGAIDI KAMA AL -SHABAABU CHENYE LENGO LA KUUA RAIA WASIO NA HATIA KAMA WALIVYOFANYA UGANDA,KENYA NA MAENEO MENGINE.KAMA KWELI LENGO LAO NI KUPIGANIA UHURU WANATAKIWA WAPIGANE NA MAJESHI YENYE SILAHA NA AMBAYO YAMEPEWA MAFUNZO YA NAMNA YA KUPIGANA NA SIYO KUUA RAIA WASIOKUWA NA HATIA.HATA KAMA WANGEKUWA NI WAKRISTO WANAUA RAIA WASIOKUWA NA HATIA WATAITWA MAGAIDI TU KAMA KULE IRELAND.IPO HAJA YA SERIKALI KUWAELIMISHA WANANCHI NINI MAANA YA UGAIDI ILI KUONDOA UPOTOSHAJI UNAOLETWA NA VIONGOZI WA KIDINI,KUWA UGAIDI UNALENGA DINI FULANI.NAHITIMISHA KWA KUSEMA ALSHABABU NI KIKUNDI CHA KIGAIDINI SIYO WATETEZI WA DINI FULANI KAMA WANAVYOTAKA KUTUAMINISHA VIGONZI HAO WA KIDINI AMBAO WAMESHINDWA KUTOFAUTISHA DINI NA UGAIDI.VIKUNDI VYA NAMANA HIYO HAKIKA HAVINA NAFASI NA HAVIKUBALIKI KATIKA JAMII YA KITANZANIA NA DUNIA NZIMA.

    ReplyDelete
  9. hiyo al shabib hatuwataki hata kama unasema ni vijana, acha kutetea uhovu, nchi yetu TANZANIA imeenda shule na haifanyi mauaji ya raia wake kama SOMALIA na baadhi ya nchi za AFRIKA. Huo ni ugaidi na TANZANIA tutapambana na wajinga wanaojiunga huko. Lets wait and see.TUPO TAYARI HAPA.

    ReplyDelete
  10. Nanukuu, "Kwa muktadha huo utaona wasomali chini ya Al-Shabab wana kila sababu za kupambana na majeshi haya ya kigeni ima iwe ndani au nje ya Somalia na kufanya hivyo sio ugaidi bali ni hatua muhimu katika kulinda sio tu uhuru wa nchi yao bali uhuru wa Afrika nzima". Kwenye hiyo nukuu ninayo ya ghafla naomba nisaidieni kuelewa:- Moja,nashawishika kuamini kuwa mauaji yanayofanywa na Al-Shabab ni halali na kama ni hivyo, ina maana ni sawa/ ruksa hata kuwaua raia kama wale waliokuwa wakitazama mpira kule Kampala ambao naamini hawakushiriki katika maamuzi ya kupeleka majeshi Somalia achilia mbali kujua kuwa majeshi ya Uganda yako Somalia. Anayejua anijuze uhalali wa kufa kwao. Mbili, je njia hii ya ulindaji uhuru ( inayotumiwa na Al-Shabab) kama ilivyoelezwa hapo juu inakubalika na nchi zote za Kiafrika hata zisizoongozwa na mtazamo huu ambao naomba niutenganishe na imani?.Tatu, mtoto aliyeachwa yatima, mjane, n.k baada ya Al-Shabab kumuua babaye, mumewe, n.k pale Kampala akiiteje hicho kikundi kama si cha kigaidi. Mwisho, siungi mkono Tanzania kupeleka majeshi Somalia (kama mpango huo upo) iwapo maslahi yetu kama Taifa hayako hatarini kwa vitendo vya Al-Shabab. Nadhani sikuchafua hali ya hewa, naomba tu kuelimishwa manake haya mambo ni magumu na yananichanganya.

    ReplyDelete
  11. We Ponda acha ujinga wako. Mimi ni Mwislamu 100%. Nasema kuwa al-shabab ni magaidi na wauaji na si Waislamu. Quran Takatifu imeeleza wazi kuwa Kumuua mtu mmoja asiyekuwa na hatia ni sawa na kuwaua binadamu wote. Pili, sheria na kanuni za jihadi ziko bayana : jihadi inaruhusiwa katika kujitetea tu, si ruhusa kuwaua watio wasio wapiganaji na si ruhusa kuwaua maadui walitupa silaha zao. Sasa wewe Ponda unataka kutufundisha Uislamu gani. Tamko lako ni porojo la kisiasa tu. Wewe ndio unayetumiwa na magaidi.

    ReplyDelete
  12. wote wajinga tu cha msingi, tambueni Tanzania ni nchi pagani,hatuna haja ya kulumbana,kinachotakiwa ni kulinda na kuijenga nchi yetu kiuchumi.hakuna haja ya kuanza kuelezea mambo ya nchi nyingine wakati ndani ya nchi yako uchumi unaporomoka

    ReplyDelete
  13. kama vipi tuingie nasisi maana freemasons ndo wanataka kuitawala dunia na baadhi yetu hatuko tayari kwa hilo. kama noma wacha iwe noma hasa katika kuitetea haki yetu hususan waislam maana kila kona uislam ndio kizuizi. hamuuwezi uislam jamani maana Allah kaahidi kuulinda hadi dakika ya mwisho. mnajisumbua tu. mtapunguza wengi lakini hauishi abadan...TAKBIRIIIII....na waislam tuhimizane kusoma na hasa kuwasomesha watoto wetu waijue vizuri dini yao tupambane nao hao kielimu ya dini na kisilaha..,TUMECHOKA NA NADHANI DUNIA IMEFIKA MAHALI PA NYAKATI ZA MWISHO>>>

    ReplyDelete
  14. There is something wrong with you.

    ReplyDelete
  15. Wadau nawashauri muache ushabiki bali angalieni zaidi uchambuzi wa mambo na hoja zilivyosimama kwa maislahi yako binfsi na nchi kwa ujumla vinginevyo Tz tutatafuta pakuweka ubavu tusipapate.

    ReplyDelete
  16. WeANNON WA KWANZA FUNGA DOMO LAKO...KAMA USOMI KILICHOANDIKWA TAFUTA KOPO UENDE MSALANI...ACHENI CHUKI WAKRISTO..

    ReplyDelete
  17. Please the author of this letter/article that is your own view and does not represent all Muslim, for me Al-Shabab is a terrorist group and all their activities are illegal and we should fight to get rid of them, nothing can justify their motives

    ReplyDelete
  18. Waislamu lazima muelewe kuwa hii Somalia isipofanyiwa kazi ita destabilize ukanda huu wa Afrika. Serikali za Kiafrika lazima zichukue hatua kuhakikisha Somalia inadhibitiwa kikamilifu. Hapa hakuna cha ukristu au uislamu. Suala la uharamia halina mwislamu wala mkristu. Ni suala ambalo tunatakiwa kupigana nalo kama waafrika. Waafrika tusipofanya kazi hii, wazungu wataifanya, tena kwa ufasaha na ufanisi wa hali ya juu? Sasa mnasubiri wazungu wafanye kazi hii? Nadhani kupambana na hawa wasomali wanaoua wananchi wa nchi nyingine ni wajibu na si suala la uislamu au ukristu.

    ReplyDelete
  19. Hivi kuteka meli na kutaka walipwe pesa nyingi ili waziachie nako ni kulinda nchi yao. Wengine walitaka kuteka meli pwani ya mafia je nako ni kwao?.
    Tuongee ukweli tusifiche mambo. Weka wazi mambo yote.

    ReplyDelete
  20. Kweli kuna mtu na akili zake anasema Al Shabab inasaidia wasomali? Hapo kuna kupotoka sana, mimi kama msomali aliyekaa TZ kabla ya kuja huku USA nashangazwa sana na mutu aliyesema kuwa Al Shabab anasaidia wasomalia. Je anaua watoto, wabibi na wengine ambao hawana makosa. Suala la Somalia haliko kwenye dini ni lipo kwenye kutosikilizana na kugombea madaraka ya president, kwani hao ambayo wanauawa ni waislamu kama sisi na wala hawapigani kwenye mosque ni huko kwa street. Naomba sans hao wanaosema al shabab wanasaidia watu waende Somalia especially Mogdishio waone kama kweli ni watu wazuri. Otherwise munapaswa kukaa kimiya.

    ReplyDelete
  21. Napenda kumuelekeza mchangiaji wa kwanza kwamba sababu za Kenya na Uganda kushambuliwa zimeelezewa katika hiyo barua na ni kutokana na wao kujiingiza katika mambo ya ndani ya Somalia.
    Kwa kuvamiwa kwenye nchi yao kuna watu ambao wanakata tamaa. Mtu aliyekata tamaa huchukua maamuzi yoyote ikiwa ni pamoja na kujiua na kuua watu wengine. Sasa kama tukiwaingilia tutawanyima chaguo lingine zaidi ya kukata tamaa na wao kuja kumalizia hasira zao kwetu. Imagine mtoto/baba/mama/ndgu yako akumbwe na mashambulizi ya hivyo kwa sababu tu ya kiherehere cha kujipendekeza kwa wamarekani, utaisamehe serikali? Mbona Cameroon mmempinga? Ila hili la Waislam kushambuliwa mnashabikia?
    Sasa nawashauri watanzania tutumie akili zetu kuweza kupambanua na tusichukuliwe wazima wazima na propaganda za vyombo vya magharibi. Wao wana maslahi yao ambayo yanatokana na sisi kuingia kwenye machafuko. Ndo sababu kuna sera za "Ugaidi" na "Udikteta". Mwenye uzalendo na nchi yake ambaye haruhusu wamagharibi kuvuna rasilimali zake basi ataitwa gaidi au dikteta na baada ya hapo wanamuangusha kwa mbinu ambazo tumeona Kongo, Iraq, Misri, Libya na hata Somali halafu ndiyo wanaanza kuzivuna zile rasilimali kirahisi kwa sababu wanaua system ya utawala na usimamizi bora wa rasilimali na kuweka vibaraka wao wenye njaa. Sisi Tanzania ambao tunawapa madini yetu bure ndio tunasifiwa tuna demokrasia.waaaaaapi hamna lolote!

    ReplyDelete
  22. Insha'Allah atakae anzisha vita Mungu ajalie wamlipue yeye kwanza sisi tuwe salama!Kwani vita haina macho sisi hatutaki makasheshe,,,,anaetaka kupigana aondoke maeneo ya watu,,akapigane huko polini na Al-Sha'ababu!
    Kweli nyie watu mnacheza mnakuwa kama hamna macho na masikio,,hamuoni huko Libya Bahrain,Yemen Egypt na huko kote!jamani watu damu zinamwagika kama maji,watoto wanawake wanakufa miguu inakatika mikono,,Hamuoni nyie!!!Anaetaka hayo wala asimshawishi sha'abab yeyote mtanzania kwenda kupigana,,aende mwenyewe,,,Tuachie kanchi ketu ka Amani!Acheni ukiritimba wa ubaguzi wa Dini!!Kila mtu ana Imani yake na aabudu atakavyo,katiba yetu inaruhusu,,,Ahlam UK

    ReplyDelete
  23. Kama hao Al-shabaab ni vijana tu mbona serikali ya somalia ime wa declare kama ma terrorist. uki google unaona habari serikali ya somalia inajiunga na kenya na uganda kupambana na Al-shabaab. Sasa kama hata serikali yao wenyewe haiwataki sisi unataka tuwapende sababu ya jina lao?

    ReplyDelete
  24. Ivi jaws wazungu wanataka nn hasa waingereza wanataka tuwe mashoga wamarekani vita

    ReplyDelete
  25. Pola Bwana Ponda. Hivyo ndivyo ilivyo.Kwa sasa hivi dunia nzima inamtumikia Mmarekani, hata blog uliyotumia kutoa maoni yako.

    ReplyDelete
  26. Tanzania ni secular state na idadi ya raia wa dini moja haiwezi kuifanya serikali kufuata siasa za kidini.

    Idadi wanayoisema inatokana na kuzaa bila mpango ndio maana nchi maskini zina ongezeko la watu kuliko nchi maskini.Hiyo sio sifa kwani inasababisha nchi kuwa tegemezi kwa resources ndogo kuliko population.

    Al-Shabab wenyewe wanasema wana uhusiano na Osama. Kikundi chochote kinachoua raia wake kwa kisingizio cha dini ni cha kigaidi kiwe cha kikristu au kislamu.

    Kikundi hiki kinapinga kucheza mpira,kusikiliza muziki kwenye radio n.k Je waislamu watanzania wanakubaliana na mtazamo kama hiyo? Nchi nyingi za kikristu na kislamu zimeona upungufu kwenye vitabu vya dini na ndio maana hazifuati kila kitu kilichoandikwa.Kwa mfano nchi ya Tunisia inakataza polygamy kwa kujua ni sheria zilizoandikwa kupendelea wanaume.Je unataka Tanzania iruhusu ndoa ya mtoto wa miaka 9? Je unataka wanawake wasiruhusiwe kuendesha gari?

    Dini ni ihari ya mtu na hakuna sababu ya kikundi cha dini kujifanya kinatetea kikundi cha kigaidi kwa sababu ya kidini.

    ReplyDelete
  27. HIVI NYIE WAISLAMU WASOMI WATANZANIA KWANINI MNAWACHAGUA VIONGOZI WENU WA DINI AMBAO HAWANA UELEWA WOWOTE? NINGEKUWA MUISLAMU NINGEANZISHA HOJA YA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA.
    KUSEMA UKWELI WANAWAAIBISHA MNO!
    WAPELEKENI SOMALIA WAJIONEE UKATILI UNAOFANYWA NA AL-SHABAAB TENA KWA WAISLAMU WENZAO.AU TUONE KAMA WATARUDI WAKIWA HAI.

    ReplyDelete
  28. Ninaishi ughaibuni na Wasomali. Nimewahadithia jinsi Tanzania tunavyowakirimu ndugu zake kwa kuwapa hifadhi (kwa mfano wakimbizi waliopewa uraia kule Tanga). Hawajamaa kila mmoja alionekana kutoa tahadhari. Namnukuu wa kwanza; "Angalieni sana mnapowapa hifadhi wasomali wana hila ni watu wabaya sana watawaharibia nchi msipoangalia".

    Wa pili akasema; "angalieni wengine ni Al-Shabab, mtakuja kujutia".

    Wa tatu akasema "Wasomali ni wakorofi, wako corrupt na wanatumia pesa kupindisha sheria".

    Leo hii Ponda unawatetea wakati ndugu zao wenyewe wanawapinga?

    ReplyDelete
  29. Ukiwa na tatizo ufumbuzi wa awali lazima utoke ndani kwako. Tatizo kubwa letu waislamu (wa jana na leo - na nahofia pengine na wa kesho) ni kutoukabili ukweli na kutafuta vyanzo vya matatizo yetu nje ya mazingira yetu. Al Sahbab ni tatizo n aibu kwa wasomali. Nasema kwa wasomali kwa sababu naona haya kuwahusisha na uislamu ambayo mafundisho yake yote yanapingana na falsafa ya Al shbab. Kama kuna mtu atasimama na kutetea Al Shabab - ama mwenyewe ni tatizo au hajui kinachotendeka duniani au vyote...

    ReplyDelete
  30. Nashukuru Mungu kama Mwislamu kuona baadhi ya Waislamu washamshtukia Ponda kuwa hana dili. Kwanza nani aliyempa yeye mamlaka ya kutusemea kwa niaba yetu? Hawa wapuuzi ndio wanaotupeleka pabaya bahati nzuri naona kuna Waislamu wenzangu wengi waliokuwa na upeo wa kuona huyu Ponda na wenzie ni wapuuzi ambao wanawatumikia mabwana zao wa huko Uarabuni badala ya kujali maslahi ya Watanzania. Shule zetu za kiislamu nyingi zinatia aibu we Ponda umekaa unawatetea shababu!!?? kichwa maji kweli kweli!! Kuanzia sasa hakuna kumualika huyu sheikh Ubwabwa kuja kula wali!! Pambaaf!!
    Mdau mwenye mapenzi ya kweli na dini na nchi yangu nikiwa Ughaibuni.

    ReplyDelete
  31. Niliwahi kutoa tahadhari kuwa kuna mambo matatu ambayo yanaweza kutumiwa na mataifa mengine kupenyeza maslahi yao na kutuvuruga.

    mambo hayo ni:
    1. Dini
    2. Umaskini wetu
    3. Utandawazi

    Mwenye kuitakia mema Tanzania atazame mambo haya kwa upana wake kabla hajapokea ushauri, msaada au mafundisho ya dini kutoka kwa watu wa nje.

    ReplyDelete
  32. Inaniuma sana nikifikiria huaga ninalia.
    Watanzania tumezidi, huyu nae sijui katoka wapi. Mbona hajawahi kutoa tamko juu ya Maalbino wanaouwawa tanzania? Hii inaonyesha ni chuki binafsi na marekani na upeo mdogo wa mambo. Msilete conspiracy theory za vijiweni, fanyeni kazi na utafiti wa kutosha kabla ya kuanza kuropoka.

    ReplyDelete
  33. we Annon unayepanga wingi wa wakristo kufuatana na mikoa acha uzushi..nyinyi mko wengi kwa hesabu gani...angalia takwimu hizi...1.. nyinyi mnaowana mke mmoja na mnajifanya wazungu kwa kupanga uzazi wa mpango...na mapadri hawaoi..huku masister sijui watawa hawaoelewi..sisi dini yetu wake mpaka wanne...watoto hakuna kugeza wazungu..hapo tuu kama una akili utajuwa nani wengi ktk nchi hii...mjinga we usiye na akili wala kufikiri...

    ReplyDelete
  34. ETI JITU LINAJINADI MIMI MUISLAM...UMEULIZWA? WEWE WAKUMBATIE HAO WAZUBGU NA WAMAREKANI...KARIBUNI UTAKUWA SHOGA..WAISLAM WA KWELI TUNAPINGA KUZUSHIWA KILA JAMBO BAYA,, KWA GIA ZA UGAIDI..NA TUPO PAMOJA TUNAOMBA ALLAH ATUPE UJASIRI KILA KUKICHA..HII DUNIA TUNAPITA..SISI TUNATAKA PEPO..WE WAKUMBATIE WAZUNGU NA WAKRISTO WANAOPENDA DUNIA..KILA KUKICHA WANAWZA UTAJIRI NA MAISHA MAZURI HAPA DUNIANI..WACHUNGAJI KUENDESHA MAGARI YA KIFAHARI KUVAA DHAHABU MAJUMBA MAZURI WAO KWAO HAYO NDIYO MAISHA..UONGOO MWINGI MADHEBAHUNI..MARA KAOTESHWA NA YESU MARA KAMUONA YESU...FIKSI TUPU..NAWEWE ANNON MNAOJIFANYA WAKRISTO MKO WENGI..PUNGUWANI KWELI WEWE...

    ReplyDelete
  35. Jambo la ajabu mnawachukia wazungu halafu mkiziwa na maisha magumu mnagombania kwenda kwao.

    ReplyDelete
  36. Haribuni nchi yenu kwa kuwakumbatia al-Shabab mkawe wakimbizi kwa watu wengine. Halafu majuto atakuwa mjukuu. Wakati huo Ponda anaponda raha huko uarabuni.

    ReplyDelete
  37. mtalumbana bure bila sababu. Ukweli utabaki palepale,,,,,, Matamshi ya mtu hutafsiri uono wake. Zinduka chukua hatua.

    ReplyDelete
  38. Nlichokiona hapa kny maoni ya watu ni kwamba watu wengi hamna data wala hamfatilii mambo kwa kina bali mnapoteza muda wenu mwingi kny facebook,mpira na blog km hii michuzi.Kwa mwenye kufatilia hawezi kusema kwanini Al-shabab walishambulia Uganda au Kenya bcoz ni Uganda ndo walianza kuenda Somalia na ndiopo kwao kukalipuliwa na kwa kenya n hivyo hivyo.
    Pia mwenye kufatilia mambo hawezi kusema Al-shabab wanateka nyara meli,hii inaonesha ujinga mlonao wadau wengi.Somalia kwa miaka mingi imekua haina serikali na kulikua na wababe wakivita wakikabila km akina Mohamed Fara Aydid,Almahd Mohamed,Jama Ali Jama nk.hawa wambabe wakivita wanamitia wao na baada yakushindwa ktk vita yakuiongoza Somalia baadhi yao ndo wamekua pirates na pia ifahamke kwamba Somalia sio kwamba wenye silaha ni Shabab tu bali kuna vikundi vingine vingi tu vyebye silaha.
    Vile vile kusema Al-shabab wnauhusiano na Osama nikweli lkn uhusiano wao ni simple tu kwamba wote ni waislam km mm ninavyohusiana na waau wote hapa kwa utanzania au uafrika wetu.
    Khs swala la idadi ya wislam na wakristo sijaona hata mmoja alotoa rejea za takwimu zake isipokua hypothesis tu,ulimwengu wa sasa hauendi kwa matakwa yako bali unaenda kwa facts ukiweka mbele matakwa yako utakua unajifool mwenyewe tu.
    Swala la huyu anaesema yeye ni muislam na anawaona Al-shabab ni magaidi kwanza namuuuliza nini maana ya Ugaidi?then namwambia aangalie sana asikurupuke tu nakujiita muislam 100% coz usilam sio jina wala sio kuswali nakufunga tu.Pia namtahadharisha huenda tayari akawa yuko corrupted na hizi main stream media.
    Mwisho ukweli utabaki kua ukweli hata km watu wadunia nzima watasema ni uongo.Nampongeza sna Sheikh Ponda kwa ujasiri alouonesha na nyie mnaehoji uhalili wa uongozi wake nawauliza je huyo mufti Simba nyie mumemchagua kwa kura zenu?mbona huhoji uhalali wake?Acheni ujinga amkeni..

    ReplyDelete
  39. Tunaomba serikali ya TANZANIA impatie tiketi huyu SHEIKH PONDA aende SOMALIA akaongee na AL-SHABIB maana anaonekana kuwa na ukaribu wa kuwafahamu sana kikundi hiki cha KIISLAM. Then akirudi HAI tutapata ukweli. Huyo PONDA hana deal , anatia aibu sana, watoto na wanawake wa SOMALIA wanauwwawa kinyama kabisa kwenye street. Theres no hope in SOMALI.

    ReplyDelete
  40. Ushauri wangu ni kuangalia habari tofauti na sio kuangalia habari ktk chanel moja tu.Kila stesheni ya TV hutoa habari kutokana na kusapotiwa na watu gani.Na vilevile tujaribu kujisomea historia za zamani nadhani tutajifunza mengi na kujua ukweli ulipoanzia au uongo ulipoanzia.Kwani historia hujirudia kila mara na nimesoma maoni yote na nimehisi kwamba bado tunahitaji kuangalia kwa makini sana.Haya masuala ya vita yanahitaji kutumia akili zetu sana.Kwasababu tunaweza tukajikuta tunagombana wenyewe kwa wenyewe kumbe tunawapa nafasi adui wa kweli kuchukua nchi kirahisi.Na kuipata itakuwa ni ngumu sana.Kwa mtazamo wangu hapa ni kwamba ukoloni wa mzungu unarudi Africa tena kwa kasi kubwa kutokana na uchumi wao kufa.Na njia rahisi ni kutupiganisha na majirani na wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi.Naheshimu maoni ya watu wote lakini hili ni muhimu kuliangalia kwa faida ya wote.

    Mwenyezi mungu inusuru nchi yetu na watu wake.Amin

    ReplyDelete
  41. Wewe ponda una NJAA TU. Unaishi kwa hizi harakari za chuki chuki bila kujali nani atadhurika. Shida yako kubwa ni NJAA.

    ReplyDelete
  42. inalillah waina ilaih rajiun

    ReplyDelete
  43. Anonymous wa sita kutoka juu ,uliyetoa TAKWIMU ZA IDADI YA WATU ktk mikoa : Wakristo na Waislamu:

    TAKWIMU ZAKO NI ZA UWONGO: NA KAMA UNAUSHAHIDI KAMILI TUPATIE TAKWIMU ZILIZOKUWA DOCUMENTED FROM ''TANZANIA BUREAU OF STASTICS'' OR ANY RELIABLE SOURCE LIKE UNDP, WORLD BANK OR SO ON..SCAN POST NA UTUPE DETAILS ZA KIANZO ''SOURCE'' ULIKOZIPATA ILI WATU WAFUATILIE USIJE UKA CHAKACHUA KAMA ULIVYO CHAKACHUA TAKWIMU ZAKO HAPO JUU,!!!

    ReplyDelete
  44. hii naona sasa kashshe, nyie mnaokataa kutoshabikia wazungu ni waongo na wanafiki wakubwa, automatically hata wewe unawashabikia, kama hutaki, usitumia internet, simu, usipande gari, usiwatch tv, usiende shule, hapo nitatambua yes hautumikii kafir, kuwa wide, hapa tumeshashashikwa pabaya tanua tu kitu kipennye babake!dunia hii utakata wamangaribi utaishije? inauma but ndo hali halisi hiyo sasa!ALSHABAAB ni maghaidi fulstop, even serekali yao haiwataki wewe ponda (aliepondwa) unatak kutuambia nini? nenda ukajiunge uongelee ukiwa huko, usituchafulie usilsam, kwani nyie ndo mnaosababsha uislam uonkane kussuoport utmbo wa terorists!na ndio tunawapa wamarekani nafasina sababu zaidi ya kuja africa kwani wanayo sababu!

    ReplyDelete
  45. Anymous wa sita kutoka juu, uliyetoa TAKWIMU ZA IDADI YA WATU ktk mikoa:Wakristo na Waislamu:

    KUDHIHIRISHA YA KUWA TAARIFA YAKO NI UWONGO MKUBWA,YA UPOTOSHAJI, YA KURATIBU, YA KUCHAKACHUA NA YA KU CHAPA KWA KEY BOARD YA COMPUTER YAKO TU,,,hizo ni personal opinion zako na sio rasmi::::ZINGATIA HAPA CHINI:

    1.Mashirikisho ya kimataifa kama UNDP, UNESCO, WORLD BANK ,IMF na mengineo yanazo taarifa ''documented report'' ya kuwa Tanzania Waislamu ni zaidi ya 63%

    2.Ktk mikoa kwa nini Dar Es Salaam na Morogoro hujatoa takwimu zako?

    3.Toa mwelekeo umepata hizo takwimu zako kutoka (source) kianzo kipi?

    4.Hii blogu inasomwa na watu wengi sana na walio makini kiakili...!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...