Sisi wana Familia ya Marehemu Mzee Wetu DYSON A.BUKUKU,leo November 13/2011.
tunamkumbuka BABA YETU MPENDWA MZEE DYSON A.BUKUKU aliyetwaliwa November 13/2009 na leo hii anatimiza MIAKA miwili kamili.
Anakumbukwa na Mke wake, Caroline Bukuku, watoto zake, Andrew, Pamela, Samuel, Debora, Albert, Herbert. Pia anakumbukwa na wake zake, Dr Albert Ulimali, Mercy Makame, Jackquline Madatta na Wajukuu zake Fiona,Ian na Caroline.
Note: Tunapenda kuwakaribisha ndugu jamaa na marafiki kujumuika nasi katika kumbukumbu ya Mzee wetu,ambapo leo kutakuwa na IBADA na baada ya Ibada tunaelekea nyumbani Mbezi Beach, Mtaa wa kilongawima kwa mawasiliano zaidi wasiliana na ndugu:
Albert Bukuku no: +0713 565 431
pia
Seoul, South Korea kutakuwa na Ibada na baada ya Ibada tutajumuika kwa pamoja mawasiliano:
Andrew Bukuku + 8210 3141 7571
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Asanteni sana
Eh! huyu mzee si mkiristo? alikuwa na wake wengi? au alikuwa muislamu?
ReplyDeletewambea bwana..umeuliza je ni watoto zake,wajukuu au watukuu wake? badala ya kutoa pole ..maana na wewe huko ndiko uendako,unaleta umbea tu hapa. Michuzi vinabo wengine wafungie maana wanachafua hewa.
ReplyDeletetunaomba mwenyezi mungu ampumzishe
marehemu mahali pema peponi.
Bwana alitoa na ametwaa tumshukuru
na kfurahi.
hao ni wakwe
ReplyDeleteKuuliza si ujinga. Nadhani kulikuwa na typo errors. Sasa wewe badala ya kuacha maelezo yatolewe unatoa povu. lol RIP
ReplyDeletewewe uliyeuliza kiumbea hapo juu..ulijibiwa kama ulivyouliza na hiyo R.I.P yako ya kinafiki ungeitoa katika message yako ya mwanzo...wewe ndie mwenye povu naona bado linakutoka...tafuta picha nyingine utolee comment..humu hutakiwi!!!!
ReplyDelete