Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji "MO" akisalimiana na waumini wa kanisa la FPCT wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha vijana wa Kanisa hilo.
Askofu mkuu wa kanisa la FPCT Paul Samwel akimkabidhi zawadi ya Mbuzi Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji kama shukrani ya kutembelea kanisa hilo.
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akizindua kituo cha vijana cha kanisa la FPCT eneo la Mwenge mjini Singida, anayeshuhudia na Askofu Mkuu wa kanisa hilo Paul Samwel .
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji Akihutubia waumini wa Msikiti wa Rahman Kindai, katika halfa hiyo MO alichangia mifuko 500 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Msikiti huo.
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akiambatana na vionozi wa kanisa la FPCT kuelekea kwenye uzinduzi wa kituo cha vijana wa kanisa hilo.
Mh. Mohammed Dewji akijumuika na Vijana wa kanisa la FPCT kucheza kwaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. this guy has a cook body for a tanzanian MP!

    ReplyDelete
  2. Katika wanasiasa wote bongo huyu ndo nazani anafanya kazi ya maendeleo na kujenga taifa wengine wote ni vilaza tuu kunywa tuu moja baridi moja moto kodi zetu. Nawengingine wanataka tuandamaneee tuu kila kukicha

    ReplyDelete
  3. sorry wanted to say he's got a cool body - not cook. he looks good!

    ReplyDelete
  4. Anajitahidi sana.

    ReplyDelete
  5. Duuh rozari shingoni!!

    ReplyDelete
  6. wao waandamane huku watu wakusanya voti. Sasa wewe Rais mwenye sifa ya kuandamana akakae Ikulu. Wamasai wamjengee boma huko huko hapa Dar es Salaam hatawali mchaga na Ikulu haingii.

    ReplyDelete
  7. jamani mbuzi mpaka ndani ya kanisa!!?

    kweli pesa inaweza kutia watu ukichaa!!

    ReplyDelete
  8. Namuunga mkono sana sana lakini kwa upande mwingine wananchi wanakuwa dependent na pesa binafsi za mbunge. Je, mbunge masikini afanyeje kusaidia maendeleo? Au ni bora kuchagua wabunge matajiri? Hili ni jambo ambalo vyamna vyote vwa siasa inabidi kuangalia kwa makini sababu mwisho wa siku it boils down to "money rules"

    ReplyDelete
  9. Anajitahidi angalau kutumia nafasi ya utajiri wake kuwasaidia wananchi pale panapowezekana. Si sawa na wale wenye mavijisenti vya dollar zinazoza ughaibuni. Ila mbona kwenye blog yake http://dewjiblog.com/ hivi vitu haweki kuna nini anachoficha?

    ReplyDelete
  10. simuungi mkono kabisa

    ReplyDelete
  11. Achaneni na mambo ya ukabila je wachaga wakisema hawawataki wazaramo? Tanzania hatutaongozwa na makabila tutaongozwa na mtu mwenye akili timamu na mcha Mungu.
    Tusiweke makabila katika hilo please

    ReplyDelete
  12. Seriously? Kwanza kabisa mbunge kutembelea jimbo lake ni responsibility yake kwahiyo this shouldn't be front and center as breaking news. Pili, kama alivyoesema mdau hapo juu, pesa binafsi isiwe ndio namna pekee kwa mbunge kuendeleza jimbo lake. I would be more impressed ningeona anatumia channels nyingine pia otherwise inaonekana kama ni hongo tu kwa wananchi ili waendelee kumpa kura. Mo, please prove me wrong bro.

    ReplyDelete
  13. sasa mbunge maskini wa nini??? mimi maskini halafu tena nichague maskini??? big No for me, yaani nimpe nafasi ya kula mpaka atajirike yeye mimi si nimeshakufa. ni wakati sasa tuwe kama marekani mwenye pesa ndio achaguliwe maskini atakuwa na tamaa ya kuiba kwanza maendeleo baadae.

    ReplyDelete
  14. Anon wa Nov 12 11:18:00PM kutoa ni moyo na sio utajiri!Je matajiri wangapi wanamali lakini ni wachoyo kusaidia hata ndugu yake acha mtu baki. Kama MO angekuwa na roho ya kutu hata hivyo mnavyosema vyake asingetoa.
    Anon wa Nov 14 12:42;00AM Mbunge kutembelea jimbo lake ni wajibu je ni wangapi wanatembelea majimbo yao??!

    Anon wa Sun Nov 13, 07;35:PM - BIG UP Kwa mchango wako wenye hekima !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...