Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Wanyama wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Shukumu Lemoningata Tuke, wa Jamii ya Wafugaji wa Kimasai ,Wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, akiwa na Mkewe, Helena Laalayok Laizer ,mara baada ya kutunukiwa Shahada yake wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 25, mwaka huu,Mkoani Morogoro.
Mhitimu wa Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Wanyama wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Shukumu Lemoningata Tuke, (katikati ) wa kutoka Jamii ya Wafugaji wa Kimasai , Wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, akiwa kwenye picha ya pamoja na ndugu zake , akiwemo na Mkewe, Helena Laalayok Laizer ( watatu kutoka kulia) baada ya kutunukiwa, Novemba 25,mwaka huu wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo hicho.
Na John Nditi.
WAFUGAJI wa Jamii mbalimbali nchini, wameshauriwa kuanza mpango mkakati wa kupunguza mifugo kwa ajili ya kwenda sambamba na matumizi bora ya ardhi ya malisho kwa lengo la kuleta tija ya mifugo itakayokuza uchumi na maendeleo endelevu katika jamii hizo,imeelezwa.
Ushauri huo umetolewa na Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Wanyama wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA),Shukumu Lemoningata Tuke, wa Jamii ya Wafugaji wa Kimasai kutoka Wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi juzi mjini hapa.
Shukumu alikuwa ni miongioni mwa Wahitimu 53 wa Shahada hiyo na pia alikuwa ni kati ya Wahitimu 1,306 waliotumikiwa Shahada mbalimbali wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo Kikuu hicho ya mwaka 2010/2011.
Hivyo alisema moja ya jukumu kubwa alilonalo akiwa msomi , ni kusaidia jamii ya wafugaji ione kuwa mifugo ni sehemu ya mazao ya biashara kwa kuendesha ufugaji bora wenye kuwaletea tija.
Alisema , kwa sasa idadi ya watu inazidi kuongezeka ,lakini ardhi haiongezeki , hivyo jamii ya wafugaji hususani ya Kimasai ni vyema kuanza kuzingatia ufugaji unaoendena na maeneo ya ardhi , ambapo ili kwenda sambamba na hali hiyo ni upunguzaji idadi ya mifugo.
“ Lazima tubadirike na sisi wasomi wa jamii hii ina tunapasa tuwe chachu ya kuleta mabadiriko haya…tusisitize ufugaji uendane kulingana na maeneo ya ardhi za malisho na hatua hii italeta tija kubwa kwa wafugaji” alisema Msomi huyo.
Alisema, Jamii ya wafugaji siku zote inajifunza baada ya kuona maendeleo ya wenzao na moja ya mfano huo ni wake mwenyewe baada ya wazazi wake kuamaua kupunguza mifugo kwa kuuza na kupata fedha zilizotumia kumsomeshea.
“ Kasi ni ndogo ya kuekelea mabadiriko haya , lakini vitendo vinapoonekana kwa baadhi ya jamii ya wafugaji hasa wa Kimasai , wafikia kupunguza mifugo na kubakiwa na idadi watakayomudu kuihudumia kulingana na ardhi itakayokuwepo kwa kuwa kasi ya ongezeko la watu ni kubwa na ardhi ni ndogo” alisema Shukumu.
Alisema mpango huo wakuifanya mifugo ni sehemu ya mazao yanayoweza kuvunwa na kupoata fedha , itaongeza chachu ya wafugaji kupata tija itakayotumiwa kuwasomeshwa watoto wa jamii hiyo kuanzia shule za awali hadi Vyuo Vikuu.
Katika mahafali hayo , Shukumu, aliambatana na Mama yake Mkubwa, Latick Tuke Lemoringata pamoja na Mkewe Helena Laalayok Laizer, licha ya kumpongeza walisema kwa nyakati tofauti kuwa elimu ni njia pekee itakayoweza kuwa mkombozi kwa jamii hiyo inayotengemea mifugo kuwa sehemu ya njia kuu ya uchumi wao.
“ Tunampongeza ndugu yetu , kwa kuwa huu ni mwanzo wa kuendelea na masomo mengine yatakayomfikisha kupata PHD ili atoe mchango wa elimu kwa jamii yetu ya wafugaji “ alisema Lemoringata.


Sky is the limit but without hypocrisy and conspirancy!!
ReplyDeleteElimu nzuri..sana hiyo Tuke, congratulation.
ReplyDeleteHongera sana kwa kuhitimu. Jambo lililonifurahisha ni kwamba umehitimu fani ambayo ambayo unaipendelea na una uvumilivu nayo. Zaidi ya yote, ajira ya hiyo fani ni kubwa.
ReplyDelete