MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu kushoto,akizindua kitabu chenye taarifa mbalimbali za maendeleo za mkoa huo tangu mwaka 1961 hadi 2011 katika sherehe za kutimiza miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania ambazo kimkoa zilifanyika katika viwanja vya nane nane manispaa ya songea juzi,kulia mfanyakazi kutoka sekretariet ya mkoa huo Jackline Tarimo,
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwahutubia wakazi wa wilaya ya mbinga jana katika sherehe za miaka hamsini ya uhuru ambayo kimkoa lifanyika wilayani humo. 
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu akijaribu kuendesha gari lililotengenezwa na fundi mdogo wa mitaan jana  wilayani mbinga wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya kazi za wajasiriamali wadogo na shughuli mbalimbali za taasisi za serikali na mashirika kwenye sherehe za kutimiza miaka hamsini ya uhuru ambayo kimkoa ilifanyika wilayani mbinga juzi,
Bw Thadei Ndimbo kulia mwenye kepu akimuonesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu jinsi mashine  ya kukoboa karanga iliyiotengenezwa na mafundi wa chuo cha veta songea inavyofanya kazi,
Mkuu wa kituo kikuu cha polisi wilaya ya mbinga mkaguzi wa polisi   G I Ng'uhumbi,kushoto akitoa taarifa ya matukio  mbalimbali ya uharifu kwa mkuu wa mkoa wa ruvuma Said Mwambungu jana mjini humo kwenye sherhe za miaka hamsini ya uhuru ambayo kimkoa lifanyika wilayani mbinga,
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu,kulia akiangalia makopo ya kahawa inayozalishwa na kiwanda cha kukoboa kahawa cha Mbinga mkoani Ruvuma,kabla ya kufunga shereha za miaka hamsini ya uhuru  wa Tanzania ambayo kimkoa lifanyika wilayani humo juzi,
Baadhi ya wanafunzi waliofika katika sherehe za maadhimisho ya miaka hamsini ya huru wa Tanzania wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma wakiangalia vipeperushi mbalimbali katika banda la mamlaka ya mapato tanzania kwenye viwanja vya michezo wilayani humo juzi, PICHA NA MUHIDIN AMRI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyo kamanda kwa kweli anastahili hongera. BMI yake ni sawa kabisa kwa askari si kama wengine ambao wako wanavitambi ikitokea kurupushani bila shaka hushindwa kumudu. Makamanda na wananchi wote tuige mfano wa huyu bwana.

    ReplyDelete
  2. Serikali uinatakiwa kutoa pesa kwa hawa watengenezaji wa magari na mashine ili waendeleze nchi badala ya kununua nje na kupoteza fedha za watanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...