Marehemu JUMA PENZA enzi za uhai wake.

Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana  nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu. 

Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi.  Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road, wauguzi na madaktari  wa Hindu Mandal.

Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru  kila mtu kipee, tunaomba shukrani hizi  mzipokee  wote kwa mikono miwili  kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha  shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.

Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu  nasi  kwa dua  nas msombi wakati wote  hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .

Vilevile  tunapenda  kuwakaribisha  katika  mkesha  wa dua  itakayofanyika  Ijumaa usiku  Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma  itasomwa  nyumbani kwa marehemu  Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .

Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na  Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.
Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...