Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Shirika la Makapuchini nchini Tanzania, Padre Wolfgan Peter, kuomboleza vifo vya mapadre wanne wa shirika hilo waliopoteza maisha yao katika ajali ya gari jana, Jumanne, Novemba 22, 2011 eneo la Ruvu kwa Zoka, Bagamoyo, mkoa wa Pwani. 

 Katika salamu hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa na vifo vya mapadre hao. “Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi habari za vifo vya mapadre wa Shirika lako la Makapuchini katika ajali ya gari. Napenda kukutumia wewe binafsi salamu za rambirambi na kupitia kwako kwa waumini wote wa shirika lako.” 

 Ameongeza Rais Kikwete katika salamu zake: “Napenda kukuhakishia kuwa Serikali yangu na mimi binafsi tuko nanyi katika wakati huu wa huzuni. Msiba wenu ni msimba wetu. Namwomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu.

 Amen.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...