Na Mwandishi Wetu
CHAMA
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) leo kimewakutanisha
wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kujadili ukatili wa
kijinsia kwa jamii.
Hatua
hii ni moja ya programu ya Kihistoria ya Siku 16 za wanaharakati
kupinga ukatili wa kijinsia kwa jamii ambayo ilianzishwa tangu mwaka
1991 na Kituo cha Kimataifa cha Wanawake katika Uongozi (Centre for
Women’s Global Leadership).
Akizungumza
katika semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya (pichani) amesema
lengo la semina kwa wahariri hao ni kuhakikisha wanafahamu mchango wa
wanaume katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Tanzania.
Akifafanua
zaidi Mkurugenzi huyo alisema lengo lingine ni kuhakikisha wahariri
wanakuwa mstari wa mbele kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 10 kuwaamsha
kiutendaji pande husika kuchukua hatua juu ya vitendo hivyo vya
kikatili.
Aidha
mada anuai zimetolewa kwa washiriki ili kujenga uelewa juu ya namna ya
kutumia nafasi zao kwa vyombo vya habari na kuleta mabadiliko katika
suala zima la ukatili wa kijinsia ambalo limekuwa likiwaathiri zaidi
wanawake na wanafunzi hasa wa kike.
Kauli
mbiu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni “Miaka
50 ya Uhuru: Pinga Ukatili Kuimarisha Tanzania Huru”.
huyu mwanamke kihere here sana i hate her.
ReplyDeleteHata mie simpendi kweli, anauma na kupuliza hana jipya zaidi ya jazba tu na chuki za kijinga.
ReplyDeleteUkweli unauma!
ReplyDeleteTena Madam endelea na Mapambano.
Wa mama wengi wanakufa kwa kufanyiwa ukatili Mkubwa vijana kwa wazee wanaambukizwa ukimwi, hawana pa kujitetea na hawajui wafanye nini,wanachanganywa na Mabinti zao,watoto,H'made na wadogo zao. Jamii imechafuka!!!
Endeleza Mapambano.
Huyu ni chadema damu hivi kweli ana tetea au unafiki? mbona swala la mkuu wa wilaya alivyodhalilishwa hakusema kitu?
ReplyDeletenyie wote mnaomchukia huyu mama mtakuwa mafisadi pia hamna jipya. Maana hampendi Ukweli
ReplyDeleteyeye wenyewe ni dictator wenzake hawapendi kakatilia kwenye cheo huku anajifanya ni champion wa democracy
ReplyDeleteHuyu ni kibaraka wa chadema, hamjui hilo, Mbona ya kule Tabora hakusema? Yule alinyanyaswa sio mwanamke? Mzandiki mkubwa!
ReplyDeleteMimi ni mwana chama wa TAWA na weza kusema kuwa huyu mama ni mnafiki, mdini, na chadema, hana kutetea haki wala nini, sisi wenyewe kwa huyo mama tunaipata laivu, ni mroho wa madaraka hivyo hapo alipo anategemea labda chadema ishinde achukue nafisi ya Mh Sofia Simba hili tunamuombea kila siku lisiwe na inshallah Mwenye enz Mungu atalisikia.
ReplyDelete