Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ludewa,Mh. Filikunjombe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa.Rais Kikwete alizindua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utoonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya Maua kutoka kwa mtoto Chipukizi wakati walipowasili mkoani Iringa.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiwa na Mbunge wa Ludewa Mh Filikunjombe na Mwenyekiti wa CCM Iringa muda mfupi kabla ya kuzindua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Katibu Mkuu Kiongozi,Mh Philemon Luhanjo akisalimia wananchi wa Mawengi wakati wa mkutano wa hadhara kufuatia uzinduzi wa mradi wa umeme wa Luwawa
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Mawengi wakati wa mkutano wa hadhara kufuatia uzinduzi wa mradi wa umeme wa Luwawa.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimia wananchi wakati akiwa njiani kuelekea Mawengi, Ludewa Kuzindua mradi wa umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utaonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Wanafuzi wa shule za msingi katika wilaya ya Ludewa,Mkoani Iringa ambako yupo kwa ziara ya kikazi na kuzindua wa mradi wa umeme wa Luwawa.
Wananchi wa Ludewa wakimshangilia Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia.
Rais Kikwete akioneshwa sehemu ya maporomoko ya mradi wa umeme wa Lumama
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya Mradi huo wa Umeme kutoka kwa Mtaalam wa Mradi huo.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akizindua na kukagua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utaonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishukuru kwa zawadi ya kuku aliyopowa kijijini Mawengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa umeme.
Rais Kikwete akimshukuru Meneja wa Mradi wa Umeme wa Lumama Bi Alice Michelezi wa taasisi ya Acra baada ya kupokea risala yake aliyoitoa kwa Kiswahili fasaha na kumfurahisha kila mtu.
Rais Kikwete akipata mapokezi makubwa kijijini Mawengi.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisalimiana na kupiga picha ya pamoja na watawa wa Kanisa Katoliki la Mawengi mara baada ya kuwasili hapo.Picha Zote na Ikulu.
Nimefurahi kwa kanisa kujenga mradi huo wa umeme.Ila nasikitika kuona mtoto mdogo anayemkabidhi maua Salma Kikwete kavalishwa nguo ya kijani huo ni uhaini-huyo hajawa na uamuzi na hajafika 18.Pia Raisi kaenda si kama kiongozi wa chama bali serikali,na anawekewa Jukwaa la kijani na spika njano na kijani pia huo ni uchokozi tena wa kijinga.
ReplyDeleteHongera kwa mradi.Kwenye hizi picha kuna kitu nimekumbuka,miaka ya 1980 hivi wakati niko shule ya msingi tulikuwa 'tunacheza'gwaride inaitwa CHIPUKIZI.Ilikuwa nzuri sana hadi tulikuwa tunagombania kushiriki.Suruali nyeusi,shati za kijani na skafu shingoni..bado ipo hii kitu??Uzalendo ulikuwa unaanzia hapa.
ReplyDeleteDavid V
Kiongozi asante kwa kutuleteamatukio muhimu kama haya. Ila nadhani jina la Mbunge anayesalimiana na Mhe.Rais siyo Filikunjombe wa Ludewa huyo ni Deo Sanga/ Jah people wa Njombe
ReplyDeleteMdau kutoka Tokyo
ccm oye
ReplyDeleteYa hiyo nzuri nimefurahi pia kumwona Askofu wa Jimbo kat.Njombe.Maluma Haya ndo maendeleo watu hawa watafaidika vizuri tu na maendeleo yao yatakimbia vema.Sehemu kama Lugarawa na Kungineko Njombe hawajui maana ya Tanesco wana Umeme wao safi na wa uhakika.Changamoto mikoa mingine, shime tuamke.
ReplyDeleteNadhani kabla ya CCM oye, mimi kwa uzalendo ningeanza kwa kupeleka oye kwa wajenzi/wafadhili wa mradi. Tuwape moyo ili na wengine wapate chachu.
ReplyDeleteAnkel, kinachonishangaza, hawajatajwa wahusika/wafadhili waliojenga au kuwezesha mradi huu wa umeme. Yafaa kuwajua ili nasi tuwaombe waje kutusaidia ujenzi katika maeneo yetu, maana maporomoko kama haya yapo kwetu pia.
Mdau, Makete.
Chadema bado hamjafanya kazi. Nyie endeleeni na maandamano tu mpaka 2015. Mnakwenda nje hamjaleta chochote cha maendeleo hata katika majimbo mnayoongoza, ila vurugu. Mnabisha. Arusha na sasa Mbeya, kwenye vurugu maendeleo yatokee wapi. Jiulizeni masuali wenyewe, kusema kweli. Kuuza bidhaa barabara ndio mnaona maendeleo nyie.
ReplyDelete