UJUMBE WA ZANZIBAR UNAOONGOZWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI ULIPOKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA BIASHARA LA MAREKANI LINALOSHUGHULIKIA KANDA YA AFRIKA (USTR).
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI (KULIA) AKIKABIDHIWA HATI MAALUM YA HESHIMA YA UKAAZI WA JIMBO LA HOUSTON,TEXAS NA SENETA WA JIMBO HILO BWANA RODNEY ELLIS.
NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR DR. SIRA UBWA MAMBOYA (KULIA) AKIMKABIDHI ZAWADI ZA MAVAZI MAALUM YA ZANZIBAR SENETA WA JIMBO LA HOUSTON, TEXAS BWANA RODNEY ELLIS (KUSHOTO).KATIKATI NI MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI (KULIA) AKIZUNGUMZA NA SENETA WA JIMBO LA HOUSTAN,TEXAS NCHINI MAREKANI BWANA RODNEY ELLIS WAKATI ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE HOUSTON , TEXAS.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA RAIS WA SOKO LA KIMATAIFA LA TAASISI INAYOSIMAMIA MIRADI YA SAMAKI YA (GRI) BWANA TOMAS NEWLAND ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE ILIYOPO KWENYE MJI WA TEXAS NCHINI MAREKANI.

Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Taasisi ya Ushirikano ya Jimbo la Houston,Texas Nchini Marekani zimefikia hatua ya kukubaliana kufanya utafiti wa pamoja utakaopelekea kuanzishwa kwa Mradi mkubwa wa Samaki Zanzibar.

Hatua hiyo ya makubaliano imekuja kufuatia Kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Zanzibar ulioko Nchini Marekani Kujitanga kwa wawekezaji wa Nchi hiyo ukiongoza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Taasisi inayoratibu Miradi mikubwa ya Samaki Nchini Marekani ya { GRI } ikiongozwa na Rais wa soko la Kimataifa la Taasisi hiyo Bwana Tomas Newland.

Mazungumzo hayo yamefanyika hapo katika Afisi za Taasisi hiyo kwenye Jimbo la Houston, Texas Nchini Marekani.

Bwana Tomas Newland aliueleza ujumbe huo wa Zanzibar kwamba mradi huo mkubwa una uwezo wa kutoa ajira kwa Wananchi zaidi ya thalathini elfu.

Alisema miradi kama hiyo ambayo tayari imeshaanzishwa katika baadhi ya Mtaifa ya Afrika,Asia, Marekani na Ulaya inazingatia zaidi uhifadhi wa Mazingira pamoja na utoaji wa mafunzo kwa Wavuvi na Wakulima wa maeneo ya Vijijini.

“ Miradi kama hii ambayo hufadhiliwa na Taasisi za Uwekezaji Vitega Uchumi za OPIC na IFC hugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 20,000,000.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri kuharakishwa kwa mawasiliano ya pamoja kati ya wataalamu wa pande hizo mbili ili kuona wazo hilo la muelekeo wa kuanzishwa kwa mradi mkubwa wa Samaki linafanikiwa.

Balozi Seif alisema kuanzishwa kwa mradi huo mbali ya kuleta uhusiano wa karibu kati ya Zanzibar na Marekani lakini pia utaleta faraja kwa Wananchi walio wengi kujipatia ajira ya uhakika.

Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikuwa na mazungumzo na Seneta wa Jimbo la Houston,Texas Bwana Rodey Ellis.

Katika mazungumzo yao Senata Rodney aliiponhgeza Zanzibar kwa juhudi zake za kharaisha Maendeleo ya Kiuchumi.

Seneta Rodney Ellis amemkabidhi Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake hati Maalum inayompa heshima ya kuwa mkaazi wa Jimbo la Houston, Texas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. This is a disgrace! Formal meeting kama hii lakini kuna vigilasi vya chee vya plastiki mezani?
    Hivi hawakuweza ku-afford proper glasses? kuna watu wataanza kutetea mambo ya recycling.

    ReplyDelete
  2. Last time I checked Texas was a state not a city. You might want to change the caption on that picture

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...