JUMUIA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA
TANZ UK
TAWI LA LEICESTER 



Ina furaha kuwaalika Watanzania na wale wote wenye Uhusiano na Mapenzi na Tanzania katika hafla ya “Siku ya mtanzania” Kusherehekea Mwisho wa mwaka pamoja na Uhuru wa Tanganyika Itakuwa ni siku ya Kutathmini mafanikio ya Tawi na Kuhamasisha Wanachama zaidi kujiunga na Jumuia Katiba ya TANZ UK haibagui na inaacha mlango wazi kwa Wote wenye mapenzi na uhusiano na Tanzania kujiunga, japo si Watanzania!

Hafla itafanyika:
Anwani: Taylor Road Primary School. Taylor Road,
Leicester, LE1 2JP
Lini?: Jumamosi 3 Disemba 2011
Wakati: Saa nane Mchana -Kumi na Moja na Nusu Jioni (2.00 pm - 5.30 pm)

Mama Nelly Nsemwa, mtanzania kutoka Sekretarieti ya Jumuia ya Madola (Commonwealth) atawasilisha Mada Maalum:
“Women as Agents of Change” Why women as agents of change. If you can change a woman then you have helped the whole community. How can we move forward?

Pia Mwenyekiti wa TANZ UK Taifa atakuwepo kushirikiana nasi.

Tafadhali, Shime! wakazi wa Leicester na miji ya karibu tujitokeze kwa wingi!
Kutakuwa na Bouncy Castle na michezo kwa watoto, Chakula na Vinywaji
Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi: tanzukleicester@gmail.com
Simu: 07982124581

Ahsante sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hapo umenena kama kutakuwa na maalim biriyan tutakuja bila maalim hatuji?!!!

    ReplyDelete
  2. NYIE JIUNHGENI NA WENZENU WA NORTHAMPTON SIKU HIYO. KUNA VINONO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...