Assalam aleikum Kaka Michuzi,

Naomba unifikishie habari hii inayohitaji mtazamo wa kipekee. Baada ya watanzania na wananchi kutoka mataifa mbalimbali kumaliza shughuli zao za Hija, kuna uzembe mkubwa na unyanyasaji ambao mbali na kuwepo tokea Dar bado umeendelea huko kwenye Hija. 

Kuna watanzania 29 ambao wamekwama baada ya kuachwa na ndege kwa uzembe wa Kiongozi wa msafara wao. Leo hii ninavyoandika habari hii, imekuwa ni siku ya Tatu Watanzania hao hawajui hatima ya msafara wao, Kila wakienda uwanja wa Ndege wanaambiwa bado tunashughulikia.

Imefikia mpaka kiongozi waliokuwa naye, amekata tamaa, hawa watanzania wamenyang'anywa passport zao za kusafiria na wanakaa kama watumwa. Inabidi ieleweke wazi kuwa watoto, familia, ndugu, na jamaa wa hizi familia wana wasiwasi mkubwa, kwani wanaweza kuhisi kuwa ndugu hawa wamekanyagwa na kufa/ama kutokewa na jambo baya.

Ninavyoongea hivi nimeongea na watu wawili walioko Saudia na wametoa habari hizi na baadaye kusema kuwa hawapewi hata nafasi ya kuonana na balozi wa Tanzania Saudia..

Tafadhali fikisha ujumbe huu kama kuna watu wanaweza kusaidia nitashukuru kwa information.

Mdau,
John.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Du what a bad experience for HIJA. Mola awajalie mrudi nyumbani salama.

    ReplyDelete
  2. Assalam Alaykum!

    Sasa hii inakuwa fedheha badala ya Ibada Tukufu ambayo ni nguzo muhimu pia!.

    Hivi inakuwaje Hujjaji anatoa gharama zote kwa Wakala wa Huduma ya Hijja halafu ubora wa huduma unakuwa haulingani na Gharama alizotoa mtu?..hivi kiasi cha angalau US$ 3,000 na ushee ni mchezo?

    Halafu je FAIDA ya huduma ya Uwakala wanazotoa wanapeleka wapi? ,wanatoa mchango wa Kijamii kama Mwenyezi Mungu anavyoagiza?

    Hivi ni mara ya ngapi Waumini wa Tanzania wasio na makosa wananyanyasika na kusumbuliwa na wababaishaji?

    Inakuwa kama Hijja wanaipata kwa msaada!

    Wakati umefika sasa hawa Masheikh Vibandiko na Maustaadh na Masharifu Wabaishaji ,

    Kama ni hivyo ili kukomesha pawekwe msimamo/MKATABA inapotokea usumbufu wowote Mahujaji warudishiwe gharama walizotoa na gharama ya Hijja ilipwe na Wakala.

    Inabidi wasiwe tena chini ya Mamlaka ya BAKWATA bali wawe chini ya Serikali ndio mambo yatakuwa!

    ReplyDelete
  3. ASSALAM ALAYKUM!,

    Jamani usumbufu kwa Mahujaji wa Tanzania sasa basi, mbona nchi zingine hakuna mambo haya?

    Watu walio ktk Hijja wasipewe mzigo wa madhambi wa bure kwa hasira wanazo sababishiwa na Mawakala!.

    Masheikh wa Uwakala wa Hijja mtapata adhabu ya Allah kwa wizi na utapeli,

    mimi,

    Ustadh Mohamed Omar
    Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  4. Assalam Alaykum!,

    Uwakala wa Hijja usichukuliwe ni kama bishara bali ni huduma ambayo ni sawa na Ibadat!

    Tafadhali zingatieni sana hili!

    Inshallah,

    SHEIKH Swalleh Khamis Abdillah
    ILALA-DAR ES SALAAM

    ReplyDelete
  5. Hawa mawakala ni wanafiki sana tena hata taratibu za usafiri wa anga hawafati sio tu kwa kuchelewesha safiri bali hata mizigo ikipoketea hawalipi fidia tena wanamatusi ya nguoni. hujitia kufuga vindevu na kuvaa vikanzu vilivyoparama kumbe wanafiki wakubwa.

    ReplyDelete
  6. wapige simu ubalozi riyadh au jeddah hili suala lazima maofisa wa ubalozi wanaelewa pia hii kero sijui itaisha lini.kuhusu passport zao hakuna hujaji anakaa na passport yake zaidi ya kitambulisho tuu.john mambo mengine kaongeza chumvi kwa jina lake

    ReplyDelete
  7. Tafadhali, tuambie ni wakala gani, maana imekuwa ni tabia sasa. Ndugu zetu hawajarejea, tuna wasiwasi mno. Ni vyema tukafahamu ni wakala gani huyu, maana mwaka jana kuna wakala alifanya majambo hadi mahujaj wakashindwa kuondoka. Ni aibu tosha. Serikali iwafungie hawa wasiotimiza wajibu.

    ReplyDelete
  8. Assalam Alaykum!

    Mawakala wa Hijja chonde chonde msiigeuze Ibada ya Hijja kuwa kama biashara, toeni huduma huku mkijiona kama mnatekeleza Swalat!

    Hii faida ndogo ya ki Duniya mnayo chuma isiwaingize ktk Moto wa Jehhanam!

    Wa Billah Tawfiq

    Sheikh Othman Ali Said
    MASJIQ ANSWAAR MUSWAAB
    MBAGALA-KICHEM CHEM
    DAR ES SALAAM

    ReplyDelete
  9. Sidhani kama kuna mtu wa kulaumiwa hapa.
    Ishaelewezwa kuwa ni UZEMBE, walichelewa ndege, kama kawaida wabongo hatu-keep time.

    ReplyDelete
  10. balozi zetu zilizo huko zisaidie,kisha wazishitaki kampuni zilizowapeleka huko,kuliko kuwaacha raia wake wakitaabika


    Sheikh

    Joseph Johnson

    Malindi Zanzibar

    ReplyDelete
  11. ASSALAMU AALAYYKUM!

    Tamaa ya Dunia inawapeleka wapi Mawakala wa Hijjat?

    Acheni ubaya Hijja ni Ibaada na sio biashara!

    Kwa vile mmeifanya kuwa biashara ndio maana pana ubabaishaji na mipango mibovu ili kupata faida zaidi!

    Wabbillah Tawfiqq

    Ust. Suleiman Khalid Uzayru
    AL MADRASSAT ANSWAAR ISTIQAAMA
    MBAGALA-KIBONDE MAJI
    DAR ES SALAAM.

    ReplyDelete
  12. Hapana usimlaumu John kwa maelezo bali tumshukuru kwa kutujuulisha ndugu zetu waliokwama.Kwa mimi nahisi wasipewe jukumu BAKWATA tena la kupeleka mahujaji ila ziwepo kampuni binafsi ambazo zisimamie shughuli nzima mpaka wanarudi salama.

    ReplyDelete
  13. Hiyo john kafanya vizuri kuifikisha hii habari katika blog hii,kwani bila yeye tungejuwaje,,wewe mdau hapo juu acha kumlaumu kwani john anafidia kuleta hii habari japo awape pia na hicho kimtwango maana dini sio ya kwake.Ni kweli sometime waarabu huwa wanamanyanyaso kwani kuishi Makkah sio ucha Mungu,watu wengi wanalalamika wakienda Hijja manyanyaso ya baadhi ya waarabu,,,Siku zote watu wengi wanaofanya biashara ya Hijja yaani mawakala au kitu kingine wanajali sana pesa kuliko utu wa mtu na Dini wanaiweka pembeni,unaweza kukuta mtu mwigine ni mfanya biashara ya kawaida na nimcha Mungu kweli kweli,na business anaiendesha kidini,,lakini hawa wanaojidai eti sijui wanasimamia mambo ya Dini wengi wao ni WAAANNNAAAFIIIIKIIIII!,,,Ahlam UK

    ReplyDelete
  14. Hivyo si tunaweka Balozi kwa kuangalia maslaha ya Watanzania huko nje? Basi na tuwaulize wawakilishi wetu watwambie nini kimetokea na kwa kutambua hivyo nimeuliza na kuelezwa kuwa habari hii imetiwa chumvi.
    Ni kweli mahujaji 29 walichelewa ndege
    sababu za kuchelewa ni uzembe wa wenyeji kwani usafiri wa ndani ni jukumu lao
    Kwa kutambuwa makosa yao waliwapeleka hotelini mahujaji hao.
    Huduma muhimu wanapatiwa ikiwa ni malazi chakula na matibabu
    Ubalozi unafahamu na umekuwa ukufuatilia kila hatuwa ikiwa pamoja na kuwatembelea na kutowa misaada midogo midogo
    Wenyeji kwa kutambuwa jukumu lao unatayarisha safari lakini hilo linachukuwa muda kwa vile ndege zote zinakuwa zimejaa wakati kama huu
    Mahujaji waliokwama wako huru na wako karibu na kati ya mji na walio na uwezo wanatembea watakavyo. Kinachoshindikana ni Fedha za matumizi kwa vile kila mtu alishamaliza fedaha yake kwa kuhisi kuwa tayari wanaondoka.
    Ni kweli kuwa kuna baadhi ya mawakala wanaowatesa Mahujaji lakini mawakala hao ni hao watu binafsi ambao hapo juu waliombwa wafanye kazi hiyo.
    Mwisho ni kuwa ni bora tufanye utafiti wa mambo kabla ya kuyaandika kwa njia ya lawama.

    ReplyDelete
  15. JAMANI BABU YANGU SIJUI YUKOJE HUKO. MWENYEZI MUNGU ATAWAFANYIA WEPESI INSHAALAAH. ASANTE JOHN MUNGU AKUBARIKI KWA KUPOTEZA MUDA WAKO KUTUJUZA

    ReplyDelete
  16. Napenda maoni ya Blog hii maana kwangu huwa ni burudani tuuu...!

    ReplyDelete
  17. Assalam Alaykum,

    Mawakala wa Hijja tusiiangalie Hijja kwa mtazamo wa ''tijara'' yaani maslahi ya kiduniya tu.

    Tushiriki kwa kuwawezesha Mahujjaji kufikia lengo kwa ufanisi ni vile Thawwabu zinafikwa kwa wote Mawakala na Mahujjaji.

    Wa Lillahi Lihamdu,

    Shk.Yassin Hussein Mustafa
    MNENIA-KONDOA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...