Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),Dioniz Malinzi akimkabidhi bendera ya Taifa,Kapteni wa timu ya Taifa Stars,Henry Joseph pamoja na kocha wa timu hiyo,Jan Paulsen leo jioni kwenye hafla fupi ya kuagwa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Chad.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),Dioniz Malinzi akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa,Taifa Stars kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila  kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi  dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo kampuni ya SBL walizindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao ishinde,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.

Rais wa TFF,Leodga Tenga akizungumza machache jioni ya leo kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila  kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi  dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo kampuni ya SBL wamezindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao ishinde,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.



Bendi ya Muziki wa dansi, Kalunde band ikiongozwa na Deo Mwanambilimbi a.k.a Mzee Goba (pichani nyekundu) wakitumbuiza jioni ya leo kwenye hafla hiyo.








Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jioni ya leo kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila lakheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,ambapo pamoja na hilo SBL wamezindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA,kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao iibuke na ushindi.Aidha Teddy amewashukuru Watanzania wapenda michezo kwa mshikamano walionao kwa timu yao ya taifa,kama vile haitoshi Teddy pia ameipongeza Serikali kwa mchango wake thabiti kwa timu ya Taifa  na shauku ya kuona timu hiyo  inafika mbali katika kampeni yake ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la Dunia huko Brazil ifikapo mwaka 2014,hivyo kuondokana na kasumba ya kuonekana kichwa cha mwendawazimu.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT),Dioniz Malinzi  akisalimiana na katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki,Nicholas Musonye kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya New Africa,jijini dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Endapo mnaenda kupigana kama mzazi anayemuokoa mwanae kutoka katika nyumba inayowaka moto, basi kwa herini na kila la heri.

    Lakini kama ni yale yale tu mliyotuzoesha, nyie nedeni tu mtengeneze kipato chenu. Mimi hayanihusu.

    ReplyDelete
  2. Hao wanaume wanatunzwa kama mboni ya jicho lakini juhudi zao wakiwa uwanjani hazilingani na huduma wanazozipata. Hivi tatizo ni mwl au/ wachezaji au watz hatujui mpira? Wadau mmedundua tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  3. Tuna tatizo kubwa sana kwenye benchi la ufundi. Shida ni kuwa waandishi wa habari walifanya kazi kubwa sana kumng'oa Maximo kiasi kwamba wanaogopa kusema ukweli juu ya Mdenimaka.
    Angalia hata wachezaji kwenye picha hiyo wanaonesha kutojiamini tofauti kabisa na walipokuwa wanafunzwa na Mbrazili.
    Tusubirie kudra tu lakini kwa mbinu Babu hawasaidii kabisa vijana.

    ReplyDelete
  4. Soka la Tz ni la majuju tu na sio la kiufundi na matayarisho ya zima moto, ndio maana Taifa haifiki kamwe. Ngoja tuone kama kawaida tu.

    ReplyDelete
  5. Siku hizi timu haichezi 'friendlies'nyingi kama wakati wa Maximo.Offcourse Chad tutawang'oa lakini..

    David V

    ReplyDelete
  6. Masikini maximo walimsakama buuuure, mimi sioni kigeni heri ya maximo tutamkumbuka. Huyu hasemwi kwakuwa mdhungu. Ni kutilia mkazo ktk mafunzo (mazoezi) na uhamasishaji,iko siku tutatoka tusikate tamaa. Kila la heri vijana wetu mwende mkatuletee ushindi, tuitangaze Tanzania ulimwenguni kote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...