Taswira za UDOM eneo la Chimwaga mjini Dodoma kutoka angani zikionesha vitivo mbalimbali ambavyo vitapokamilika ujenzi wake vitakuwa na wanafunzi elfu 40 na kukifanya kuwa moja ya vyuo vikubwa barani Afrika, Jumamosi hii UDOM itakuwa na mahafali yake ya pili Ijumaa hii ya Novemba 25, 2011
The University of Dodoma (UDOM) is pleased to announce its second Graduation Ceremony to be held on Friday 25 th (for College of Humanities and Social Sciences (CHSS) and College of Natural and Mathematical Sciences (CNMS)) and on Saturday 26 th November 2011 (for College of Education (COED) and College of Informatics and Virtual Education (CIVE)), at the Chimwaga Building Complex in Dodoma.
On each day, the ceremony will start at 1.30 p.m. and will be for all candidates who successfully completed their studies and qualified for the Certificate, Diploma and Degree Awards of The University of Dodoma for the academic year 2010/2011. The Graduation ceremony will be preceded by the 2nd Convocation and Academic Prizes Awarding Ceremony that will be held on Thursday 24th November 2011 in the Chimwaga Hall.
For that and more visit http://www.udom.ac.tz/
For that and more visit http://www.udom.ac.tz/
wadau mi nadhani lugha yetu inatosha sana hapakuwa na haja ya kuandika "chuo kikuu / university"
ReplyDeletenawasilisha
Hapa ni kuchemka mwanzo-mwisho. Nakuunga mkono mdau wa kwanza. Je, Chuo Kikuu cha University of Dodoma ndiyo nini? Au ukumbi wa Chimwaga Hall ndiyo nini? Kwa kweli naipongeza blog hii kwa kutuletea habari nyingi na nzuri kwa mapema sana. lakini haya makosa yanatuhudhi. Si unajua hata kama kikipikwa chakula kizuri sana, lakini kama kikiwa na mchanga, kitaliwa kwa taabu saana. Mimi nafananisha makosa haya na mchanga. Kwa upande mwingine nafananisha habari nzuri za blog hii na chakula kizuri.
ReplyDeleteWahusika wahamasishe upandaji miti kwa wingi kwa ajila ya kuongeza uzuri wa mandhari ya chuo.
ReplyDeleteni nkweli,hakuna haja ya kuchanganya lugha...na ni bora zaidi ikaandikwa kwa kiswahili tu basi, hata kama kiswahili chenyewe pia kitakosewa kama mdau wa 2 aliposema "yanatuhudhi" badala ya 'yanatuudhi' lakini ni bora kuliko kosa na kutuletea kiswanglish au englhili..
ReplyDeleteTUMEFUNGA AYA YA 1
AYA YA 2
ebwana hiki chuo kumbe ni kikubwa sana eeh, daa. tena ni kizuri mno inavyoonekana. lakini serikali ye2 ijitahidi watu wasome kuwa wataalamu na si kusoma ili kuwa wezi wa fedha za umma, hili linawezekana na kwa kuanzia serikali lazima ifanye juu chini kuhakikisha migomo haipo kabisaa na ikiwepo iwe michache mno na yenye malengo maalumu kama vile ikitokea tusikie kuwa "wasomi wa chuo kikuu fulani wagoma wakishinikiza serikali isikubali nyongeza ya mishahara ya wabunge" au "wasomi wagoma wakiishinikiza serikali ivunje mikataba dhalimu ya uchimbaji wa madini" na vitu vingine kama hivyo. tukifanya hivi nina imani tutafika salama maana lengo litakuwa la kitaifa na si la mtu binafsi
ahsante michuzi
by sm
kazi nzuri ya raisi kikwete
ReplyDeletehata mimi nilitaka kucomment kitu hichohicho but kumbe wadau wenzangu mmeshakisema. tusiharibu lugha kwa kujaribu kuielezea lugha. mfano Uwanja wa ndege wa Tanga airport (kama nilivyoiona kwenye blog yetu hii) this is bad.
ReplyDeleteHii ndio ladha ya blog hii.kumexi lugha na vitu vingine ili kufikisha ujumbe artistically.kama unataka strict hard news na kiingereza au kiwahili cha kimahakama nenda kwenye blog za kiserikali zipo nyingi sitaki kuzitaja hapa. This is news with entertainment. Michuzi anajua kiingereza, kiswahili. Mimi binafsi na wengi tu nipo excellent kiingereza na kiswahili na kisukuma.' Barabara ya Morogoro road' 'chuo kikuu cha university' Kaka 'Nsoji' MICHUZI KANYAGA TWENDE.
ReplyDeleteWate mliochangia hapo juu yaelekea ni wageni katika hii blog. Kuna staili fulani ya lugha ambayo ni kama imekubalika na wapenzi wa hii blog. Maneno kama barabara ya morogoro road, happy birthday ya kuzaliwa na mengine mengi ni maneno ya kawaida hapa.
ReplyDeleteWatoa hoja wa kwanza na wa pili POLENI NA KARIBUNI. Hii ndio 'lugha' RASMI ya Blogu Ya Jamii hata pale kwenye barabara ya Morogoro road ukiwa unapita na mywife wako.....
ReplyDeleteWADAU HAPO JUU WAGENI WA KU COMMENT HII GLOBU. TUACHENIANI WENYEWE TUNAJUANA!!!!
ReplyDeleteSasa Mtoa maono unayelalamikia lugha, mbona wewe unasema "unatuhudhi" badala ya "unatuudhi"?
ReplyDeleteMimi ninafikiri huyo anayeandika university ya chuo kikuu anafahamu kuwa anakosea ila anaamua kufanya utani. Hata hivyo naungana na wewe kwamba lugha haitakiwi kufanyiwa utani kwani inatakiwa itumike kama ilivyo na si vinginevyo.
Jamani punguzeni munkari!! It's just a joke!! Kwani mmeanza kuangalia hii blog lini? Yaani mnaamini kwamba Michuzi haelewi utofauti uliopo?
ReplyDeleteMandhari nzuri sana,ni tofauti sana na ule wakati nilipofika hapo mwaka 1997 kabla ya jengo na eneo hilo kugeuzwa chuo.Ilikuwa jengo nene ndani ya uwanda mnene. Haya ni maendeleo makubwa kwa sector ya elimu.
ReplyDeletehii ndio globu ya jamii ikiongozwa na ankali mjomba michuzi
ReplyDeletekatika kufanikisha shughuli za mywife wako
barabara ya kilwa road chuo cha univesit barthday ya kuzaliwa kwa ankali