Mkazi wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoani Tanga ambaye jina lake halikuweza kupatikana,akichafua mazingira kwa kutupa takataka katika mto uliopo katika eneo hilo kama alivyokuta na kamera man wa Globu ya Jamii ambapo alipobaini kuwa anapigwa picha alianza kuficha sura yake huku akiendelea na shughuli yake ya kutupa taka hizo bila uoga wowote.
 Hapa ndio hakutaka kabisa kuonekana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. sababu ya elimu duni

    ReplyDelete
  2. inafahamika kabisa ni kosa kutupa taka ovyo!...? Je huyo cameraman alichukua uamuzi gan zaidi dhidi ya mtu huyo??? Au ndo aliishia kupiga picha tu???...

    ReplyDelete
  3. Wewe Cameraman ulimchukulia hatua gani huyo mpuuzii

    ReplyDelete
  4. Tanzania chafu inawezekana

    ReplyDelete
  5. Kithibiti kipo hicho, na nyie watu wa Tanga mwamjua huyo; mwataka mpiga picha akamkamate avunjiwe kamera yake?!!?

    Kamwulizeni Jery Muro!!

    Usiwaone hivyo hao, kwanza hali yake tu inafanana na shari. Ona, anajua kabisa anapigwa picha lakini hatishiki bali aficha uso tu, nyie mwadhani mtu mwema huyo. Mchunguzeni upamba aliouficha kiunoni kwanza, mwataka mpiga picha apoteze damu yake?

    ReplyDelete
  6. Watu wengine bwana, ungekuwa wewe ungemsogelea? Mnajua kulaumu tu na kusuta watu. Mnapiga kelele ndani ya chumba, mbona hujaandika jina lako hapo kama kweli ungefanya lolote?

    Tanga kulee, kunani kulee?

    ReplyDelete
  7. Moneni yule anayemwangalia toka kwenye nyumba ile, yule ndiye anafaa kuchukuwa hatua mara moja kwenda kumkamata. Mpiga picha anathabarisha tu, kwa wasiotambua utunzaji wa mazingira.

    Huyu ni bingwa wa wachafuzi wa mazingira kule kwao.

    ReplyDelete
  8. picha hii imenikumbusha mpiga picha aliyeenda sudan kuandika madhara ya njaa na kumkuta mtoto aliyelemewa na njaa huku pembeni kuna tai(ndege) akimsubiri afe ili amle,yule mpiga picha alichofanya alichukua picha nzuri ya kuuonyesha ulimwengu hali ya njaa ilivyokuwa.Mwanzoni alisifiwa sana kwa kufikisha ujumbe mzuri kwa watu,lakini baadaye wachambuzi wa mambo walipoanza kuhoji kwanini hakumwokoa yule mtoto asiliwe na tai badala ya kukazania kuchukua picha tu,alikosa jibu,akasononeka ,mwishowe nilisikia aliamua kujiua kwa kugundua kosa alilolifanya.Sasa swali mpiga picha ulichukua hatua gani dhidi ya mtu huyu adui wa mazingira na maisha ya watu ?au ulifurahia kumpiga picha tu!!!!!

    ReplyDelete
  9. wee mpiga picha kama hukumchukulia hatua yoyote tafadhali nyofoa lipicha lako mara moko!

    ReplyDelete
  10. Mpiga picha kafanya kazi yake mengine sio ya kwake na hana nyenzo za kufanya zaidi ya hapo. Wahusika waanzie hapo!!!

    ReplyDelete
  11. Nyie vipi kazi ya kamera man si kufikisha ujumbe? sa mnataka afanye nini zaidi?

    ReplyDelete
  12. Wafuasi wa CHADEMA hao na ukimwambia lolote kama una gari litavunjwa na camera yako halafu siku ya pili maandamano kuvunjia watu maduka yao.Upsss nimesahau kama wamekuwa mke wa pili na maandamano yamekwisha.

    ReplyDelete
  13. mpiga picha kafanyakazi kubwa na ya muhimu. Next ni dola.Tuko pale pale nchii hii sheria hazisimamiwi. Ela imechukua nafasi ya sheria

    ReplyDelete
  14. PAMBAFU KABISA!!!SIJUI NISEME HUYU KAKA AKAMATWE NA KUPIGWA MIJELEDI KADHAA AU NISEME ATIWE DARASANI NA KUFUNDISHWA SOMO LA MAZINGIRA NA HIFADHI ZAKE?
    NAONA BORA YOTE MAWILI YANAMHUSU HUYU KAKA

    ReplyDelete
  15. sasa mnataka atupe wapi nawakati system mbofu, na hisitoshe hizo takataka si mmempawenyewe, mlijua anaenda kuzitupa wapi?huyo jamaa anafanya kazi naye ,kwani taka taka si nikazi ya jiji au kila mtu anatakiwa kuipeleka taka taka dampo mwenyewe?

    ReplyDelete
  16. Jamani msameheni huyu jamaa, Kwa jinsi alivyo na mavazi yake sidhani kama ana akili timamu.

    ReplyDelete
  17. hapa ni daraja la pale Hale, jirani na kituo cha uzalishaji umeme cha pangani falls

    ReplyDelete
  18. Ni keli ni uchafuzi wa mazingira na inafaa kuchukuliwa hatua. Na hata kama si mtoni uchafu ni uchafu tu! Ila,nimezaliwa Mkanyageni, nimekulia Mkanyageni lakini ninawasiwasi na huo mto unaopita katikati ya nyumba au kijiji sijapata kuuona. Naomba mpiga picha ataje jina la huo mto. Naujua mto kivumiro na sijapita siku nyingi sina ila sidhani kama kumeshajengwa kwa kiasi hiki. Au siyo Mkanyageni ya Wilaya ya Muheza kata ya Ngomeni tarafa ya Ngomeni?

    ReplyDelete
  19. ASANTE SANA MPIGA PICHA KWA KAZI NZURI SANA. UMEMALIZA JUKUMU LAKO. MGAWANYO WA MAJUKUMU (DIVISION OF LABOUR"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...