Kundi la wanariadha wanaoshiriki katika Mbio za Bendera ya Taifa za Kili  likiwasili katika Mji wa Korogwe Mkoani Tanga juzi. Jumla ya Wanariadha 30 wanaikimbiza bendera hiyo wakitokea Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kupitia kampeni ya "Jivunie Utanzania" inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambapo wataungano na wenzao kutoka mikoa mingine ili kuipandisha katika Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru.
Wanariadha wa timu ya Mwanza (njano) na Timu ya Dodoma (nyeusi)wanaoshiriki katika mbio za Bendera ya Taifa za Kili kutoka Mjini Mwanza na Dodoma walipokutana katika Mji wa Karatu mkoani Manyara wakielekea mjini Moshi ambapo jumla ya wanariadha 60 walikimbiza bendera za rangi ya njano na Nyeusi kupitia Kampeni ya Jivunie utanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya KIlimanjaro Premium Lager.
Wanariadha wa timu ya Mwanza (kulia) na Timu ya Dodoma wanaoshiriki katika mbio za Bendera ya Taifa za Kili kutoka Mjini Mwanza na Dodoma walipokutana katika Mji wa Karatu mkoani Manyara wakielekea mjini Moshi ambapo jumla ya wanariadha 60 walikimbiza bendera za rangi ya njano na Nyeusi kupitia Kampeni ya Jivunie utanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya KIlimanjaro Premium Lager.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...