Na Salama Njani   Habari Maelezo-Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja  Mustafa  Mohammed Ibarahim amewaonya Wanaume wanaopenda kuendeleza vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake kuacha mara moja ili kumaliza kasi ya  vitendo hivyo.

Mustafa ameyasema hayo wakati wa maonyesho ya kazi za vikundi vya mradi wa kuwawezesha  wanawake wa Zanzibar  (WEZA), yaliyofanyika  katika ukumbi wa Salama hoteli ya Bwawani Mjini zanzibar.

Amesema kwa sasa wanawake wengi wamekuwa na uelewa mkubwa wa kujua sheria dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia njia ambayo itawasaidia kuwafichua na  kuwabana wanaume wanaopenda kuendeleza vitendo hivyo.

Amesema kuwa mradi wa WEZA umetoa fursa kubwa kwa wanawake kwa kuwapa elimu ya kiuchumi na kijamii hasa katika masuala ya kujua haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kujua hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa na wanawake mara tu baada ya kupatwa na vitendo vya udhalilishaji.

Mbali ya kupata elimu ya kiuchumi ambayo inawawezesha wanawake kubuni miradi ya kuweka na kukopa lakini pia wamefaidika kwa kupata elimu ya kijamii itayowawezesha kukabiliana na  changamoto za udhalilishaji ambapo kwa sasa wanaume  wataoendeleza vitendo hivyo kukiona cha moto.

Wakisoma risala ya vikundi wanavikundi hao wamesema,kupitia mradi wa WEZA, wameweza kujengeka uwezo kwa wanawake wengi kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi uliopita wa  mwaka 2010 katika vijiji mbali mbali vya Unguja na Pemba .   

Wamesema jumla ya wanawake 27 kutoka vikundi vya WEZA walijitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi ya udiwani ambapo jumla ya wanawake 8 wameshinda nafasi hizo.

Aidha wamesema kupitia mradi huo umewawezesha hata kuweka maelewano mazuri katika familia zao, kwa kuwa na uwezo wa kusaidia  mahitaji ya kifamilia kutokana  na ongezeko la kipato kinachotokana kazi za vikundi vya mradi huo.

Wakielezea changamoto zinazowakabili wanavikundi hao wamesema, pamoja na mafanikio waliyoyapata lakini bado wanakabailiwa na changamoto mbali mbali ikiwemo jamii kuendelea kuficha wahalifu wa ukatili dhidi ya wanawake,ukosefu wa soko wa bidhaa wanazozizalisha na uzorotaji wa kesi za udhalilishaji zilizopo katika mahakama mbali mbali. 

Mradi huo ambao umemaliza muda wake wa miaka minne uliokuwa chini ya Care Tanzania na chama cha wanahabari wanawake Tanzania( TAMWA) ulianza mwaka 2008 ambapo Tamwa ilijikita katika elimu ya jamii na Care ni kwa upande wa kiuchumi, ulilenga kwa  Mikoa miwili ya Zanzibar,ambayo ni  Mkoa wa Kusini Unguja na Mkoa wa Kaskazini Pemba, na  ulidhaminiwa na EU, Serikali ya Australia na Care Australia.

Nae Meneja wa mradi huo  Rose Edwin Matovu  amesema mradi huo ambao umegharimu jumla ya Euro 1500 hadi kumalizika kwake  umefanikiwa  kuwakomboa wanawake wa vijijini kutoka ndani ya mfumo dume na hatimae kuwa mstari wa mbele katika harakati za kujiletea maendeleo.

Amesema kutokana na mafanikio ya mradi huo kwa wanawake umekuwa ni kivutio kwa jamii nzima hata wanaume kwa kuonesha hamasa ya kujiunga na vikundi vya miradi hiyo ambapo kwa sasa wanaume wengi wameungana na wanawake katika kazi za kiuchumi na kijamii.

Vikundi vya mradi wa WEZA vina jumla ya wanachama 7842 kwa Unguja na Pemba wakiwemo 6998 wanawake na 844 wanaume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hata wanawake nao ni wanynyasaji wa wanaume. Waonyeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...