Kaka Michuzi, 

Napenda kutoa shukrani zangu za pekee pamoja na watanzania 29 waliokuwa wamekwama Saudi Arabia, kuwa watanzania hao, sasa hivi wako njiani kurudi makwao baada ya kilio chao kusikika. 

Blog yako imekuwa mchango mkubwa sana katika kufanikisha matendo ya wahusika, na kusababisha balozi wa Tanzania Saudi Arabia kwenda kuwaona kwa haraka na kuwashughulikia. 

Balozi huyo, alieleza wazi jinsi habari zao zilivyoenea katika mitandao, haswa katika Blog yako, na jinsi watu walivyochangia katika kutoa maoni yao. 

Napenda pia kuwashukuru watu wote waliotoa michango yao ya kimawazo inayojenga zaidi  katika kufanikisha jambo hili. 

Ni matumaini yangu kuwa uzembe huu hautatokea tena, na mawakala waliohusika watachukuliwa hatua zinazoeleweka ili  iwe mfano kwa watu wengine. 

Na kwa wenzetu walio na mtazamo wa kwenda hija, hii iwe onyo kuwa mambo kama haya yanatokea na yanaudhi. 

Mdau 
John

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. bro michuzi hapo umepiga bao, uongo mbaya

    ReplyDelete
  2. Assalam Alayikum Bwana Issa Michuzi.
    kweliBlog yako ni chachu ya mafaanikio ya sehehmu nyingi na sekta mbalimbali za kijamii.
    kukwama kwa Mahujaji Jeddah ni tatizo ambalo linaweza kumtokea yoyote kwa wale wanaosafiri toka sehemu kwenda sehemu nyingine.
    Mahujaji walichelewa kufika kiwanjani na hivyo kuachwa na ndege yao waliokuwa wasafirie kutoka Jeddah kurejea nyumbani, kutokana wingi wa Mahujaji wanaorudi kutoka Jeddah na Madina inakuwa vigumu sana kupata nafasi za watu 29 kwa wakati mmoja kuwasafirisha, Wizara ya Hija Saudi Arabia ilichukuwa jukumu la kuwapeleka Hoteli Mahujaji wote na kuwalipia kila kitu . Maafisa wa Wizara wamejitahidi sana kutoa mchango kuwasaidia Watanzania hawa waliokwama Jeddah King Abdul Aziz International Airport na kisha kupelekwa Azhar Hotel Jeddah.
    kwa ushirikiano wa karibu toka siku ya awali kati ya uongozi wa Al-Madina (Wakala wa Mahujajihao) na Maafisa wa Ubalozi imesaidia sana kutatuka kwa tatizo la booking yao ya kurudi nyumbani, maafisa hao wa Ubalozi wa Jeddah na Riyadh ambayo ni kilo 1300 kutoka Jeddah walikuwa wakiwafariji mara kwa mara Mahujaji hao na hadi kufikia hatma ya safari yao ya leo ambayo wametumia South China Airlines kupitia Dubai/Muscat/Dar na wanatarajiwa kuingia Dar saa za jioni kesho kwa shirika la ndege la Oman.
    Mwenyezi Mungu awe pamoja nao, nawasifu kwa uvumilivu wao.
    Ahsante.
    Sabrina Ali

    ReplyDelete
  3. Mdau John kwanza nakushukuru kwa mchango wako mkubwa ulio utoa kwa kutuhabarisha na mwenyezi mungu atakupe fungu lako na akujaalie imani zaidi.Mwenyezi mungu awajaalie mahujaji wafike salama na dua zao kukubalika kwa ibada walizofanikisha.Amin.

    ReplyDelete
  4. Mdau John na hijja ni wapi kwa wapi? Au ulikwenda kuchukua video ya ibada hiyo?

    Halafu hebu tutajie jina la hao wakala ili tuweze kuepukana nao, haitoshi tu kutoa onyo

    ReplyDelete
  5. ... moja ya sifa za m'Tanzinia ni ujamaa, amani, uhuru na umoja bila ya kujali dini wala kabila, hapo ndipo mchango wa mdau John unapoleta thamani ya u'Tanzania, zaidi ya hapo hakuna zaidi. bwana mkubwa hapo juu ulitakiwa ulitambue hilo

    ReplyDelete
  6. hii ndy moja ya sifa ya kuwa mtzania, tunapendana hasa kwenye dhiki na dharura, Bw John, mungu akujaalie kila lenye kheri katika maisha, huwezi amini jana wtz, tulishtuka na taarifa yako, leo tumefarijika sana sana, miongoni mwao ni wazee wangu, mie mwenyewe sikujuwa maskini, kwa niaba ya watanzania wenzangu tulio ughaibuni, nasema asante pamoja na global ya jamii kwa kutusitiri!

    ReplyDelete
  7. Assalam Alaykum,

    Sawa tunakubali udhuru uliotolewa, isipokuwa sio mara ya kwanza Mawakala wa Hijja kwa Tanzania pekee wamekuwa wakilalamikiwa zaidi kuliko sehemu zingine za dunia kwa nini?

    Mbona nchi kama Nigeria ndio ktk Afrika inatuma Mahujjaji wengi hatujapata kusikia wakikwama hata mara moja?

    Tanzania pekee imekuwa ndio msitu au kisiwa cha madhila haya?

    Inshallah tujirekebishe!


    Salaams,

    Ust.Jabbir Hassan
    TABORA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...