Mheshimiwa Hamad Rashid,
Hivi karibuni vyombo vya habari kama vile Gazeti la Mwananchi na mengineyo vimeripoti ya kwamba kuna mgogoro mkubwa ndani ya chama cha CUF unaosababishwa na dhamira yako ya kuutaka ukatibu mkuu wa chama hicho.
Halkadharika imeripotiwa ya kwamba vurugu zilizotokea hivi karibuni zinahusiana na mkutano wako katika kata ya Manzese.
Kwa mujibu wa Bwana Julius Mtatiro mkutano wako ulikuwa hauna uhalali ndani ya chama kwa kuwa ulikuika taratibu za chama.
Mheshimiwa Hamad Rashid, kwa kuwa wewe ni mwanasiasa mkongwe, mashuhuri na mzoefu, tukio hili mimi pamoja na wadau wengi tunaofuatilia matukio mbalimbali nchini, kwa heshima na taadhima tunaomba ulitolee tamko lako rasmi pamoja na tathmini juu ya athari kwa chama cha CUF kutokana na malumbano yenu kupitia vyombo vya habari.
Shukran
US Blogger
Usblogger11@gmail.com
Pointi ya Hamadi Rashid ni wazi kwamba chama cha CUF baada ya kuungana na CCM kimepoteza upinzani kwa kuwa wanalazimika kukubaliana kwa kila jambo. Maalimu Seif ndiye anayefaidika zaidi binafsi kutokana na makubaliano hayo kwa hiyo Mhe. Hamadi anataka CUF irudi ktk upinzani wa kweli.
ReplyDeleteHawakuliona hilo wakati wanasaini muafaka?!!
ReplyDeletenini wewe hujui kama hamadi zoea madaraka sasa sio kiongozi tena wa upinzani bungeni ni kiongozi wa upizani katika chama chake huree Mungu ijalie cuf ife tupumzike na roho zetu. haki sawa kwa hamadi Rashid
ReplyDeleteCuf ni toto ya sisiemu, hilo liko wazi, hawana sauti tena (mtoto kwa baba hakui). Juhudi za Mh. Hamad naziunga mkono kurudisha heshima ya Cuf. Sharifu kawapiga chenga ya mwili(sikumtegemea kama angebadilika hivi). Sasa Cuf iko wapi kwenye upinzani au utawala (mmdanganywa mmedanganyika).
ReplyDeletehaya shime wana Cuf rudisheni upinzani wenu.
mi kwa upande wangu, haya mambo ya hamadi kung'ang'ánia uongozi nilishayaona toka bungeni alipokua anapingana na mbowe kwenye kukabidhi uongozi. cuf wameshachelewa huyo kishaunda makundi, ndo waosababisha vurugu wakipata madaraka wanatulia,
ReplyDeleteKwanza unaposema serikari mbili imefanya watu zanziber wasimwage damu cha kujiuliza, ni nani chanzo! chanzo ni watu wanaotaka madaraka, watanzania lazima tupime tusikubari kuingizwa matatizoni kwaajiri ya faida binafsi za watu. seif alikua ndo chanzo zanziber amepata madaraka mnamsikia tena je amekuja kuwagawia pesa anazopata! sana sana tuamke tufanye kazi hakuna hata mmoja ataekuja kutulete welfare kweny kaya zetu kila mtu anataka kwa manufaa yake na familia yake. take care
Anonimous 10.00am
ReplyDeleteWewe ni mshabiki tu. Jaribu kuwa objective. Kama hupendi upinzani then sema hupendi upinzani, na siyo Cuf tu. Mbona huongelei Chadema wanaosababisha watu wafe ovyo eti kwa kutafuta umeya Arusha? Mbona wamekuwa kimya wakati mafuta ya taa yanapandishwa bei eti kwa kisingizio cha kumtetea mwenye pesa (gari)?
Nampenda sana comedian Mhe. Hamad Rashid. Miaka kadhaa huko nyuma CUF ilipokuwa na wabunge wengi bungeni na kuunda kambi ya upinzani, aliomba bunge liwatambue kama Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, na bunge likaridhia. Alisahau kwamba kuna siku CUF itapoteza viti bara kama ilivyo sasa. Mwaka jana, nafasi ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ikachukuliwa na Chadema. Ni Hamad huyu huyu aliyeungana na CCM kubatilisha jina alilopendekeza mwenyewe miaka kadhaa nyuma, akalazimisha Chadema watambuliwe kama kambi ya upinzani bungeni na si Kambi Rasmi ya Upinzani. Hii ni baada ya CUF kukosa sifa za kuunda kambi rasmi ya upinzani bungen na baada Hamad kukosa nafasi ya kuongoza mojawapo ya kamati za bunge. Leo hii akiwa kakosa mwana na maji ya moto, anataka kumpoka u-Katibu maalim Seif. Sasa mpaka hapa kwa nini tumchukulie kwamba ni COMEDIAN? Mimi sijasema ni mroho wa madaraka, NO, ni COMEDIAN.
ReplyDeleteMichuzi Usiibanie hii, wadau wajue historia ya mbunge huyu kwa undani.
Mimi naona Seif Hamadi ni mwanasiasa maarufu na mkongwe hali kadhalika Hamadi Rashid.Kama majina yao yanavyo shabihiana wote ni wanasiasa wanayoijua vyema siasa ya ndani na nje ya tanzania.kwa ujumla katika upinzani huwezi ukaongelea siasa za tanzania bila kuwataja watu hawa.Hebu wakae chini watafakari kwanza maana wapiganapo mafahali wawili ziumiazo ni nyasi.
ReplyDeleteMgogoro wa cuf unaweza kuisaidia sana cdm kuimarisha upinzani wa kweli nchini! kuwepo kwa cuf imara kumeivuruga sana cdm kiasi kwamba badala ya kujikita ktk malengo, tuliojiwekea, wanatumia muda mwingi kubishana na cuf huku ccm wanachanja mbuga!
ReplyDeleteHawa jamaa huenda wanatumia nguvu za giza kujipatia influence huku bara. Yaani chama cha watu chini ya 1 million kinatawala siasa za watu zaidi ya 40 mil. wanapewa publicity kubwa kwenye media! huku tukisahau matatizo makubwa yanayolikabili taifa letu kwa wakati huu!
ReplyDeleteWaarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba.......malizia wewe mwenyewe hapo. Nyi mnapiga kelele tuu.
ReplyDelete