Mwakilishi wa Tanzania katika kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Zitto Kabwe ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CPA Tawi la Tanzania na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni akichangia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kinachoendelea mjini Arusha. Wengine pichani ni wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Moeng Pheto kutoka Botswana (pili kushoto), Mhe. Seneta Winnie Magagula kutoka Swaziland ambae pia ni Waziri wa Teknohama nchini humo, na Mhe. Elijah Okupa, Mbunge kutoka Uganda. Kikao hicho hukutana Tanzania mara mbili kwa mwaka kupitia bajeti ya chama hicho na kusimamia masuala mengine ya kifedha ambapo mwaka huu wamekutana pamoja na mambo mengine kuangalia namna bora ya kuwekeza fedha za michango ya wananchama ambapo Tanzania itakuwa ndio kituo kikuu cha uwekekezaji wa michango hiyo ya nchi wanachama za jumuiya ya madola zipatazo 19 barani Afrika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Request Muntanga akipata ufafanuzi kutoka kwa Katibu wa Afrika wa Chama hicho ambae pia ni Katibu wa Bunge la Afrika, Dr. Thomas Kashililah wakati wa kikao cha Kamati hiyo kinachofanyika Arusha. Bunge la Tanzania ndio Makao Makuu ya Sekretarieti ya Chama hicho na Katibu wa Bunge moja kwa moja anakuwa Katibu Mkuu wa Bara la Afrika wa chama hicho. Wengine pichani kutoka kulia ni Nd. George Seni (kwanza kulia) ambae ni Mhasibu Mkuu wa Bunge na Mhasibu wa Chama hicho barani Afrika, Nd. Demetrius Mgalami (pili kulia), Mkuu wa Itifaki wa Bunge na Katibu Msaidizi wa Afrika. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Elijah Okupa kutoka Uganda na wa tatu kushoto ni Mhe. Moeng Pheto kutoka Botswana
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola katika kanda ya Afrika pamoja na wajumbe wa Sekretarieti. Walioketi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Chama hicho, Mhe. Request Muntanga kutoka Zambia, Mhe. Seneta Winnie Magagula kutoka Swaziland, Bi Amina Magina kutoka Idara ya Uhasibu ya Ofisi ya Bunge, kutoka kushoto ni Katibu wa Kanda ya Afrika na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, Mhe. Moeng Pheto kutoka Botswana, Nd. Demetrius Mgalami (Mkuu wa Itifaki Ofisi ya Bunge na Katibu Msaidizi wa CPA Kanda ya Afrika), Mhe. Elijah Okupa kutoka Uganda, Bi. Elsie Simpamba kutoka Zambia ambae ni Afisa Mipango wa Chama hicho, Nd. Cossian Opata kutoka Uganda, na Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge na Mhasibu wa Kanda, Nd. George Seni. PICHA ZOTE NA SAIDI YAKUBU WA SEKRETARIETI YA CPA, OFISI YA BUNGE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...