Hayati Alfred Ngotezi
Habari iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Afisa Uhusiano Mwanzamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na aliekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Serikali la Kila siku (Daily News), Mpiganaji Alfred Ngotezi amefariki Dunia ghafla  usiku wa kuamkia leo  Jijini Arusha ambako alikuwepo kwa maandalizi ya Mkutano wa Mashirika ya Afrika ya Hifadhi za Jamii unayotarajia kuanza rasmi kesho kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha - AICC.

Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa hii,  Hayati Ngotezi kabla ya kuaga Dunia alikuwa katika meza ya chakula na baada ya muda kidogo akanyanyuka kwa nia ya kwenda kujisaidia na hapo ndipo alipoanguka ghafla na kupoteza maisha.

Globu ya Jamii inaungana na wadau wote walioguswa na msiba huu mzito wakiwemo Ndugu,Jamaa na Marafiki katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mpiganaji 
Alfred Ngotezi mahala pema peponi

-Amin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimepokea kwa mstuko na huzuni taarifa hii. Natoa pole kwa wafiwa na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya rafiki yetu Alfred. Amin. Ahmed, Arusha.

    ReplyDelete
  2. kifo cha rafiki yetu mpendwa Alfred siyo tu kimenistua bali kimeacha pengo kubwa katika safu ya wanahabari hodari ambao daima walifanya kazi kwa umahiri na uadilifu mkubwa.Nilimfahamu marehemu tangu tukisoma pamoja kidato cha sita katika sekondari ya Mzumbe mwaka 1977. Mwenyezi Mungu ndiye muweza wa yote. Yatosha kumuomba ailaze peponi roho ya rafiki yetu mpendwa Alfred. Brig. General Maganga, Washington DC.

    ReplyDelete
  3. Ni mshtuko kwangu na wanaomfahamu. Ni kazi ya Mungu sote tutapita njia hiyo. Natoa pole kwa familia yake Mungu awape subira na tumuombee yaliyo mema mbele yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...