Hayati Alfred Ngotezi |
Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa hii, Hayati Ngotezi kabla ya kuaga Dunia alikuwa katika meza ya chakula na baada ya muda kidogo akanyanyuka kwa nia ya kwenda kujisaidia na hapo ndipo alipoanguka ghafla na kupoteza maisha.
Globu ya Jamii inaungana na wadau wote walioguswa na msiba huu mzito wakiwemo Ndugu,Jamaa na Marafiki katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mpiganaji
Alfred Ngotezi mahala pema peponi
Alfred Ngotezi mahala pema peponi
-Amin.
Nimepokea kwa mstuko na huzuni taarifa hii. Natoa pole kwa wafiwa na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya rafiki yetu Alfred. Amin. Ahmed, Arusha.
ReplyDeletekifo cha rafiki yetu mpendwa Alfred siyo tu kimenistua bali kimeacha pengo kubwa katika safu ya wanahabari hodari ambao daima walifanya kazi kwa umahiri na uadilifu mkubwa.Nilimfahamu marehemu tangu tukisoma pamoja kidato cha sita katika sekondari ya Mzumbe mwaka 1977. Mwenyezi Mungu ndiye muweza wa yote. Yatosha kumuomba ailaze peponi roho ya rafiki yetu mpendwa Alfred. Brig. General Maganga, Washington DC.
ReplyDeleteNi mshtuko kwangu na wanaomfahamu. Ni kazi ya Mungu sote tutapita njia hiyo. Natoa pole kwa familia yake Mungu awape subira na tumuombee yaliyo mema mbele yake.
ReplyDelete