| Mkongwe wa muziki wa injili Afrika Mzee Cosmas Chidumule pamoja na mwalimu maarufu wa Muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani,Wamegusa mioyo ya maelfu ya waumini walioshiriki ibada katika kanisa la mlima wa moto (Mountain of fire) la Mikocheni B Assemblies of God linaongozwa na Dr, Rv. Getrude Rwakatare. Kibao cha Kwa Yesu kuna raha chake john Shabani alichomshirikisha Chidumule ndicho kilicho tifua maelfu ya waumini hao. Wimbo huo umo ndani ya album mpya yakwake John shabani alioshirikisha waimbaji nyota wa nyimbo za injili Tanzania, Congo na Uganada. Album hiyo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu kwa mfumo Audio na video na inasimamiwa na kusambazwa na Kampuni ya Msama Promotions |
Home
Unlabelled
COSMAS CHIDUMULE NA JOHN SHABANI WAKONGA MIOYO YA MAELFU YA WATU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




michuzi turushie hapo walau kawimbo kamoja tuburudike ndani ya Yesu!!!
ReplyDelete