Habari kaka michuzi
Naomba unitolee dukuduku langu katika blog yako. Mimi ni mhitimu katika chuo cha mipango Dodoma (Institute of Rural Development Planning).
Tatizo ni kwamba toka tumemaliza masomo yetu mwezi wa sita (2011) mpaka sasa tunazungushwa sana kupata Transcript zetu. Yaani tulitegemea zingekua tayari mara tu baada ya graduation ambayo ilifanyika tarehe 25 November mwaka 2011, lakini kila siku wanatupiga danadana.
Walisema zingekuwa tayari kuanzia tarehe 15 mwezi December 2011 lakini ghafla wakabadilisha tena na kusema kuwa wataanza kuzitoa kuanzia tarehe 10 mwezi Januari 2012.
Kwakweli kitendo cha kushindwa kupewa vyetu vyetu kinatusababishia kushindwa kupata ajira na ukizingatia waajiri hawahitaji provision results. Hili ni tatizo kubwa na linatukosesha kazi.
Ninaomba uongozi wa chuo ushughulikie swala hili kwa umakini. Hiki chuo kimekuwa kikiendeshwa kiholela mno na hakiendi na wakati. Tunaomba wajifunze kutoka vyuo vingine ambavyo mwanafunzi anapomaliza tu anapewa na vyeti vyake wakati huo huo.
Hiki chuo kinatuharibia. Tunahitaji vyeti vyetu tutafute kazi.
Asante.
Kila kitu ktk maisha kina Faida na Hasara zake.
ReplyDeleteSiasa ya Ujamaa kwetu wa Tanzania imetusaidia kwa upande wa FAIDA (Umoja wa Kitaifa,Ushirikiano,Undugu,Uzalendo,Uvumilivu na mengineyo)isipokuwa kwa upande wa HASARA (Uduni ktk ufanisi wa mambo,Kutokuwa Wachumi,Kuwa Butu ktk ushindani,Kuwa butu ktk maamuzi sahihi,Kutojali Vipaumbele,Uzembe ktk Uendeshaji-Uendeshaji chini ya kiwango, namengineyo)
SASA BASI WADAU WA CHUO BADO WANA YALE MAPUNGUFU YA UJAMAA!
Kwa vile PRIMARY VISION YA CHUO BADO IPO KTK MFUMO WA KIUJAMAA KAMA KIPINDI CHUO KILIPO ASISIWA HUKO MIAKA YA NYUMA!
Sidhani kama kuna kitu kama hicho Mipango. Nilihitimu pale miaka zaidi ya mitano iliyopita, pamoja na mapungufu yaliyokuwepo lakini hili la TRANSCRIPT mmmmhhhh...halijawahi kuwepo. Kama kuna chuo Tanzania ambacho kinakuwa kwa kasi ya ajabu basi MIPANGO kinaongoza. Ningekushauri tu rekebisha au shughulika na hicho kikwazo kinachowafanya wahusika wasikupe cheti, yamkini hujamaliza ada au mambo memngine kama hayo ila TRANS.. ni kitu kidogo sana.
ReplyDeleteAnonymous wa pili,mchango wako waonekana thahiri ni kuweka utetezi mbele pasipo kuangalia uzito wa hilo swala na muathirika ndiyo kaweka bayana yanayomsibu kwa sasa,iweje ww usiamini eti kisa ulisoma hapo na ulipata vyeti vyako kwa wakati!? tatizo letu watanzania kila jambo twaweka siasa mbele, tubadilike jamani,msaidie mtu kwa ushauri kutokana na aliyosema lakni siyo kujifanya mtu unajua zaidi.
ReplyDeleteJambo la msingi ni kurekebisha taratibu ili wahusika wapate vyeti ontime.haina uhakika kama ulipata mapema(msemaji wa 2 hapo juu) basi uweke assumption kuwa hadi sasa hali ni hiyo.mi nimemaliza pale mwaka juzi..frankly speaking kuna usumbufu.hivyo si lazima ukaleta literature ya 5 yrs ago.unadhani mtoa hoja anahaja gani ya kuleta hoja kama anajua yeye ndo ana tatizo....?no data no right to speak
ReplyDelete