Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Taifa,Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kuwapa pole baadhi ya ndugu wa Marehemu Halima Mchuka,leo wakati alipofika kutoa heshima za mwisho.
Rais Jakaya Kikwete akiungana na viongozi wa msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakazi wa jiji la Dar es salaam kuuombea dua mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka wakiongozwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Fennela Mukangara (wa kwanza kulia) katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakiwa na majonzi mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu Halima Mchuka aliyekuwa mtangazaji wa shirika hilo kwa takribani miaka 19 leo jijini Dar es salaam.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiingizwa ndani ya msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya Ibada maalum kabla ya kupelekwa katika makaburi ya Msasani kwa ajili ya Mazishi.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiwekwa katika makao ya kudumu katika makaburi ya Msasani leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa TBC marehemu Halima Mchuka leo jijini Dar es salaam katika makaburi ya Msasani.

Picha ya Marehemu ikiwa Juu ya Jeneza.
Mkurugenzi wa Zamani wa TBC,Bw. Tido Mhando akiwa kajumuika na waombolezaji wengine kwenye msiba wa Halima Mchuka.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO na IKULU.
Mungu ilaze mahala pema roho ya Dada yangu huyu, tuliishi naye miaka ya nyuma pale ilala shariff shamba kabla hajahama
ReplyDeleteEe Bwana Yesu utusaidie, kifo kimekuwa tishio hasa kwa watu maarufu Tanzania. Tutakukumbuka daima kwa yote uliyotutendea. Poleni ndugu na jamaa kwa msiba huu
ReplyDeleteKumbe hata waislam sasa nao wanaaza kuga kama wakiristo?
ReplyDeletePoleni sana wafiwa
POLENI SANA TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU
ReplyDeleteMdau wa Dec 31, waislamu wanaruhusiwa kuaga mwili wa marehemu, lakini hapo awali ilikuwa ni familia na ndugu wa karibu tu (ndani ya chumba).
ReplyDeletePili maiti haifunguliwi uso labda kwa wale waliokufa vitani (tunasema wamekufa shahid). Ni kama hivyo ulivyoona kwa Marehemu Halima kiwiliwili chake hakionekani.
Wewe unayesma kumbe na wasilimu wameanza kuaga maiti unanishanganza, siku zote tunaaga maiti ile sisi hautuwaachi wazi watu waka wafeli, maisha yote tunapita kwenye janaiza au mkakeka na kubusu kwa hiyo usirukie hoja. Nyie mna desturi ya kumuaga mtu alie lala, mnapita kumfeli mkitoka hapo ooh mdomo wake ulikuwa wazi, oohh anatoka damu.......sisi sio hivyo
ReplyDeletekwani imekuwa vita jamaa alikuwa anauliza tuu
ReplyDeleteHao ndio wabongo anony Sat Dec 31, 10:24:00 PM 2011, wabongo hawana kasumba ya kuelewesha au kueleweshwa (si wote lakini), lao ubishi tu na kuanzisha mijadala isyo na tija. Mbona anony wa Sat Dec 31, 03:18:00 PM 2011 alitoa maelezo bila jazba! Safari yetu ndefu wandugu!
ReplyDeleteALSHABABU WAMEANZA TEH ETI JANAIZA,ALIKUWA ANAULIZA TU
ReplyDeleterip halima. and my heart is with the family.
ReplyDeletenatoa maoni kuwa katika issues kama mtu kafariki ingekuwa vizuri kuweka pivha yake ili na sisi wengine tumuone. michuzi...
Ooh Mola tunusuru sisi waja wako. Poleni sana wafiwa kwa msiba wa mpendwa Dada Halima.
ReplyDeleteHakuna kitakachobaki duniani kwani sisi sote tupo safarini.