JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari na baadhi ya Wabunge kuwa posho ya Vikao vya Bunge imeongezeka kutoka Sh.70,000/= hadi 200,000/=.
Suala la mabadiliko ya Posho ya Vikao vya Bunge lilijitokeza katika Mkutano wa Wabunge, tarehe 8 Novemba, 2011 walipoiomba Serikali iangalie upya suala hili kwa lengo la kuboresha. Hadi tunapotoa tangazo hili, Serikali haijatoa taarifa iwapo Posho hiyo imeongezeka kutoka Sh.70,000/= hadi 200,000/=.
Tunasikitika na kushangaa sana kwa kauli hii kwani ina lengo la kujenga chuki baina ya Wabunge na Wananchi wao waliowapigia kura.
Kwa mujibu wa Waraka wa Rais kuhusu Masharti ya Mbunge uliotolewa tarehe 25 Oktoba, 2010 wenye Kumb. Na. CAB111/338/01/83 na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, pamoja na stahili zingine, Mbunge anastahili kulipwa Posho ya Kikao ambayo ni sawa na Sh.70, 000/= kwa kila kikao na masharti hayo hayajafanyiwa marekebisho wala kufutwa.
Kwa hiyo, taarifa hiyo iliyotolewa siyo sahihi na imelenga kuleta chuki baina ya Wabunge na Wananchi. Endapo itatokea mwenye mamlaka kupitisha kiwango kipya cha Posho ya Vikao vya Bunge, itakuwa ni uamuzi kama uamuzi mwingine anaoutoa wa kuwaongezea Watumishi wa umma mishahara, posho, marupurupu na mafao mengine.
Ofisi ya Bunge inahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Vyombo vya Habari kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri na kujenga mahusiano mazuri ya kuaminiana kati ya Wabunge, Vyombo vya Habari na Wananchi.
Imetolewa na:
Dr. Thomas D. Kashililah
KATIBU WA BUNGE
Mimi nafikri msemaji wa Bunge ana matatizo either ya Kitaaluma au hajui anchosema na amelazimishwa kutoa taarifa.Aposema ni ya posho ya 200,000/- ni kuleta chuki kati ya wanachi na wabunge na wakati huo anakubali kwamba wabunge wameomba posho iongezwe na kufika laki 2.Ila sasa Serikali haijakubali Ombi hilo.Je kuna kosa gani tukisema tayari anajua wanachokiomba ni kinyume na tunachotaka watufanyie wananchi na kwa kuwa wamekubaliana Bungeni waombe posho ya laki 2,tayari kwetu sisi wananchi hiyo inatosha kuona hawana uchungu na wananchi wao,angesema bunge lilikataa hapo tungemuelewa?Ila Serikali ndiyo haijapitisha HAPO KUNA TOFAUTI GANI NA ANACHOKITETEA?Kwa hiyo amejua kulipwa laki mbiloi ni WIZI NA NDIYO MAANA ANA WASIWASI KUWA WANANCHI WATAWACHUKIA WABUNGE WAO.
ReplyDeleteNCHI YETU BILA KUTOKE KIZAZI CHA KUKUBALI KUTESEKA KWA AJILI YA KIZAZI KIJACHO HATUWEZI KUENDELEA HADI SIKU YESU ANARUDI,Hakuna mwenye uchungu hata Bungeni wala Serilini kila mtu anajiangalia yeye na watoto wake hasa inapokuja kwenye kugawana keki ya Taifa.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Africa.
what defference does it make. Kumbe ni kweli mmeomba posho iongezwe hadi laki mbili. Sasa sioni upotoshwaji. Wabunge mnataka laki mbili kama posho au hamtaki?
ReplyDeleteacheni kujikanyaga bana..kama mmejiongezea maulaji mmejiongezea tu sa mnajistukia nini si tutapiga kelele tusahau tu kama kawaida!!
ReplyDeleteYawezekana si taarifa sahihi, ila mbona jibu limechelewa? mbona hakujibiwa mwandishi alipouliza kabla ya kuchapishwa?
ReplyDeleteAsili haina kawaida ya kuacha hombwe, hivyo kwa kuchelewa kujibu ama kujiumauma tayari watu washajazia kile wakijuacho.
Mungu Ibariki Tanzania.
Sidhani kama katibu wa Bunge ulistahili kuandika hiyo sentensi hapo chini inayosomeka "Ofisi ya bunge inaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya habari kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri na kujenga mahusiano mazuri ya kuaminika kati ya Wabunge na Vyombo vya Habari" .Badal yake maneno hayo yangeandikwa kwa kuvitaka vyombo vyote vya habari vilivyopotosha umma kuomba radhi kupitia front page za maggazeti yao ili wananchi waelewe kwamba tatizo ni vyombo vya habari ambavyo daima huandikahabari za uchochezi kwa lengo la kunufaisha bishara yao. Katibu wa Bunge waambie wasaidizi wako wawe wanakuandikia maneno yenye mpango na sio ili mradi kuandika kujaza karatasi "madokezo"
ReplyDelete2. Kanushi hii imekuja imechelewa inaonesha mlikuwa mnajiandaa kutafuta majibu. next time toeni kanushi zenu mapema.
3. Nategemea kesho utaandika kuvitaka vyombo vya habari kukanusha la sivyo muwachukulie hatua za kisheria. si unawanasheria Ofisini kwako?>>>
Mdau
Kadunchi
UK
watu walioleta hii taarifa kwa wananchi si vyombo vya habari bali ni baadhi ya wabunge ambao hawakutaka hiyo posho ipitishwe kwa sababu wanajua kuwa wananchi hawataridhika. Nadhani sentensi iliyotumika ni ( wananchi watatupiga mawe) Binafsi nilipata hii habari kutoka kwa wabunge wawili waliyoiandika kupitia mtandao wa twitter. Siku hizi nadhani kuvilaumu vyombo vya habari kumepitwa na wakati. siku hizi habari zinapatikana kutoka kwawakereketwa kupitia mitandao ya kijamii ( social network) kama twitter na facebook.
ReplyDeleteJe, wabunge walioshiriki kupotosha umma kwa taarifa ya UONGO watachukuliwa hatua gani?
ReplyDeleteWabunge wameshalipwa posho za shs 200,000.00 ndio maana wanapitisha kila utumbo unaoletwa na serikali.
ReplyDeleteKama Katibu wa bunge anabisha ajaribu kukichukulia hatua za kisheria chombo kilichoripori habari hiyo au kukitaka kikanushe habari hiyo kama hajaumbuka.
Sasa hii inakuwa kazi...hawa Waheshimiwa mshahara wao ni wa kupanda tu,,,tena safari hii umepanda kwa zaidi ya 100% tena kimya kimya!,,,taafrifa kama hii Dr.Kashillah anaitoa baada ya mabadiliko, kwa nini isitoke kabla ili tuipinge?.
ReplyDeleteOngezeko la posho za kujikimu kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu inakuwa mbinde lakini posho kwa Wabunge inakuwa shwari,,,tutafika kweli?
Acheni mambo ya kale bwana, elfu sabini kwa mbunge ndo nini? Kashfa kabisa!! Hata hiyo Sh. 200,000 waliyoomba ni posho ndogo sana, wananchi tusiwatese wabunge wetu. Kikubwa wachape kazi na mafao waongezewe. Mbona hamjahoji posho za mawaziri au kwa kuwa hamkuwaajiri? Wabongo elimu hakuna kabisa!!
ReplyDeleteLisemwalo lipo, kama halipo laja.
ReplyDelete"Wabunge wameomba posho toka 70,000 hadi 200,000" Hili lipo. Linalokuja bila mashaka ni kukubaliwa, wao si wanaotunga sheria bwana na kupitisha, watashindwa kupitisha maslahi yao? Kwa itikadi ya Tanzania haiwezekeni kutopitisha. Hata kama hamtatangaza, lakini piga ua watapitisha tu.
Mambo mengine yanatushangaza wananchi. Yaani 70,000/= ya kukaa tu mle ndani mnaiona ndogo!!! Ama kweli Nyerere amekufa na umaskini kwa kuipenda nchi, na kuwaacha walafi wasioaibu!!! Wengi wenu mlisoma enzi ya shule bure, safari kwenda shule kwa warrant, leo 70,000 mnaona ndogo!!! Mnataka 200,000 kwa kikao cha siku; kiasi ambacho ni zaidi ya kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa mwezi wa Mtanzania. Ama kweli wapo wasiothamini watu wengine.
Hivi maendeleo ya nchi hii yatasimamiwa na nani hasa? Kwa hali hii yupo mtetezi wa kweli wa nchi hii?
Eeeehhh! Napata kigugumizi. Hakuna wawakilishi wa kweli wa wananchi bali wanamaslahi tu!