Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CUF,Mh. Machano Khamis Ally ambaye ni Kiongozi wa Ujumbe na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofika Ikulu jijini Dar es salaam leo Kuonana na kuzungumza na Rais Kikwete juu ya Sheria ya kuanza kwa mchakato wa kutafuta Katiba Mpya. 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Ntatilo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Mh. Mnyaa Mohamed Habib
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Ismail Jusa.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa kwenye Mazungumzo na Ujumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofika Ikulu jijini Dar es salaam leo kuzungumzia Sheria ya kuanza kwa mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa serikali yake umekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Machano Khamis Ally kuhusu namna ya kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mkutano huo umefanyika asubuhi ya leo, Ijumaa, Desemba 2, 2011, Ikulu, mjini Dar es Salaam na ujumbe wa CUF umemkabidhi Mheshimiwa Rais mapendekezo ya chama hicho kuhusu namna Sheria hiyo inavyoweza kuboreshwa.
Baada ya majadiliano ya saa mbili, pande hizo mbili zimekubaliana kujipa nafasi ya kutafakari zaidi na zitakutana tena jioni ya leo.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
02 Desemba, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Hivi huyu wasira sikuizi ofisi yake ipo Ikulu eeh...maanake kila siku namuona pale sebuleni kwa Kikwete.

    ReplyDelete
  2. Watu wengine bwana! Unaalikwa na rais unaenda na raba na fulana kama vile umekurupushwa!!!!

    ReplyDelete
  3. HEKO MDAU WA PILI...YAANI KUNATAKIWA ELIMU YA KUVAA SANA..RABA NA JEANS WAPI NA WAPI?SHAME ON YOU

    ReplyDelete
  4. kwani laba na fulana siyo nguo,
    au wee ulitaka avae nini?
    Haya ndo mambo yale yale ya mzungu kuvaa ndala anasikia joto na akivaa mswaili basi anafangasi

    ReplyDelete
  5. Kweli ikulu pashakuwa mahali pa ovyoovyo kweli basi hata kuvaa shati na suruali nzuri ukachomekea na kiatu cha ngozi walau uonekane nadhifu jamani hao waliomruhusu huyu bwana kuingia hivo lazima wachukuliwe hatua. Au ndio kutuma ujumbe kwamba aliyemadarakani si lolote wala chochote. Mwatia haibu atii!

    ReplyDelete
  6. Hali halisi ya mtanzania, maisha bora yamegoma.

    ReplyDelete
  7. hii tabia ya vijana wadogo unakuta anamwita huyu fulani, huyu wasira inatoka wapi? mbona maadili yanatokomea kila siku jamaniiii!!!!!

    ReplyDelete
  8. Wadau kila vazi lina sehemu yake...hii ni Ki bongo bongo, mavazi kama raba na jeans sio ya kiofisi ni mavasi mepesi kwa shughuli kama michezo za hapa na pale mfano shughuli za kijamii!

    ReplyDelete
  9. CUF mlishaolewa pika pakua na CCM kitambo!...nyie ni kama CCM-B sasa kama tayari mpo ktk ndoa mnaweza kutafuta mwaliko ili kumuona mume wenu?

    ReplyDelete
  10. Jamaa huyu wa CUF na maraba maraba yake anatia aibu...angalia kwanza kikao kizima yupo peke yake, hivi aliambiwa viwanja vya ikulu baada ya kikao kutakuwa na mazoezi ya viungo?...bora angeazima hata suti ya dereva au kondakta wa basi alilojia kutokea kwake Buguruni ajisitiri kuwa anaenda onana na Raisi!

    ReplyDelete
  11. CCM B oh sorry wandugu, CUF nao wamekwenda kufanya nini IKILU? si waliunga mkono Katiba kujadiliwa na hata wakati walipobaki ndani hawakusena lolote kuhusu marekebisho! sasa wanataka nini? au kwa kuwa Dume la mbegu CHADEMA wamekwenda IKULU! CUF sio chama tena labda kwa Pemba

    ReplyDelete
  12. Maadili yamepotea wa kulaumiwa nani kama siyo nyie wazazi. Huyu kijana amejifunza toka kwa wakubwa (wewe unayemlaumu).

    ReplyDelete
  13. Kwa vile ni mtindo, basi kila mtu, chama, kikundi watakwenda Ikulu!!

    Mimi simaanishi haki isitumike, lakini, kwani CUF na CCM si waliukubali mapema wa katiba? Sasa wanakwenda kumwona Rais walisahau nini? Au kuiga tu?

    Wiki ijayo utasikia nao CCM wanataka kwenda kuonana na Rais!!
    Siyo nia yangu kuwakataza, hapana, mimi nadhani mnamchosha tu mheshimiwa Rais!

    Mswada umeshakuwa sheria sasa leteni kwa wananchi tuchangie. Tusubiri kuchangia namna gani Katiba iwe. Siyo kwenda kwenda Ikulu kila kukicha!!! Ndiyo maana hata wengine wanakwenda na Tshirts na kandambili, hawajui hata heshima ya Ikulu.

    Wasira ni jina lake. Ila kwa vile ana wadhifa, inafaa pia kutanguliza kutaja wadhifa wake. Ndiyo utamaduni wetu watanzania, kuheshimiana. Ingawa wengine wanatumia vibawa nyadhifa zao kwa kuwanyanyasa wanyonge.

    ReplyDelete
  14. ningependa kujua hayo mapendekezo waliyopeleka yana tofauti gani na yale waliyopigia makofi bungeni wakapitisha? crap!

    ReplyDelete
  15. Jamani kuvaa nako ni WITO huwezi jua jamaa hapo ndo kavunja kabati!na akajipiga na RABA MTONI.

    ReplyDelete
  16. Hivi CUF mlisubiri Chadema wawape mawazo/ umuhimu wa kukutana na raisi wetu au nmnataka kuonekana kua na nyie mna cha kuchangia. Kuweni wabunifu wa vitu vyenu bana, kuna mambo megi ya kufanya kuchangia maendeleo ya nchi. Au kama mnaona Chadema wana mawazo mazuri zaidi basi jiungeni nao ili upinzani uwe na nguvu kuliko wapinzani kuanza kugombana wenyewe. Ni mawazo tu nashauri.

    ReplyDelete
  17. Hv Prof. Ibrahim H. Lipumba yupo wapi siku hz? Naona kama timu imepwaya bila ya mwenyekiti!

    ReplyDelete
  18. Me naona wote mmekosa kazi jaribuni kujadili ya msingi na sio hayo mnayo jadili mtalala mika mpaka lini me nafurahi sana kwa jinsi wa Tanzania wana vyo lalamika coz wanasahau kufanya kazi alafu nauhakika Tuna wapiga gape ya ukweli

    ReplyDelete
  19. Wewe mdau unaelalama kwa huyu kijana kumuita wasila ulitaka amuite baba au? Viongozi wanachefua roho za wananchi mpaka wanashindwa kupata haki ya heshima.....mwananchi njaa kali kiongozi anatumia mamilioni na familia yake bado unataka tuwaite majina gani zaidi ya hayo wasila au orasa

    ReplyDelete
  20. hebu acheni ushamba, kwani raba ndio zinafanya kazi au kichwa cha mtu, nendeni uingereza mkaangalie madaktari wanavaa vipi hospitali! mmekaririshwa na filamu za kikoloni! Amkeni. Mzee Nelson Mandela mbona hamkupigia kelele wakati alipokua anavaa shati tu na sio suti?

    ReplyDelete
  21. Sasa haya ndio mazungumzo ya katiba?! Hakuna agenda wa adidu yaani kama vile mmeenda kumtembelea mjomba wenu tajiri... Raba si tatizo kubwa kama maswala yanazungumzwa hakuna hata anaerekodi ....Nafikiri hhapo wanasubiri chai waondoke...Wote walioko hapo hawapo siriazi kabisa

    ReplyDelete
  22. Je, nini maana ya vazi nadhifu? Je, ni suti na viatu vilivyochongeka kwa mbele? Kwa kuwa siyo lazima kila mtu kuvaa sare, au vazi maalum pale anapoenda ofisini, basi kila mtu anaweza kuvaa anavyojisikia, ilimradi awe 'comfortable' na vazi lake. Hakuna ubaya kuvaa tisheti na raba.

    Hapa hasa hasa tujadili, je kulikuwepo na umuhimu wa CUF kwenda ikulu? Maana waliujadili mswada na kuupitisha! Pia tunajua kuwa CCM ni mume wa CUF. Kwa utamaduni wa mtanzania, Mume ana KURA ya TURUFU. Kwa hiyo CUF haina ubavu wa kubadili matakwa ya CCM

    ReplyDelete
  23. Nyie wote munaomulalamikia kijana mdogo aliyemuita Mh. Wasila, Wasila: kwanza munajua vipi kuwa ni kijana mdogo? Yaani kwa kuwa munaona picha hapo munadhani hiyo ni picha yake! Kweli TZ critical thinking ni zero. Kama nyinyi hamuwezi kuweka majina yenu baada ya kutoa maoni yenu kwa nini munadhani huyo anaejiita Kelkaf anaujasili wa kuweka picha yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...