Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Magari ya Scania Nchini,Mark Cameron (katikati) akifungua mlango wa basi jipya la Kampuni hiyo lililopewa jina la Dar Coach wakati wa uzinduzi wa basi hilo uliofanyika leo kwenye stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo,Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Magari ya Scania Nchini,Mark Cameron akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa basi jipya la abiria ambalo limetengenezwa maalum kwa ajili ya waTanzania,leo kwenye stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo,jijini Dar.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania,Godwin Rwegasira akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Magari ya Scania Nchini,Mark Cameron akionyesha namna ya kuliendesha basi hilo kwenye uzinduzi wa basi hilo uliofanyika leo kwenye stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Scania Tanzania,Mark Cameron (kulia) akimabidhi funguo ya basi hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi ya Dar Express,Yudika Mremi ambaye alitangaza kulinunua basi hilo na mengine manne leo hii.
Sehemu ya Ndani ya Basi hilo.
Linavyoonekana Basi hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. ningependa kuona picha za basi zaidi kuliko watu, hata ukiniwekea picha ya marketing manager yeye siyo product.

    ungetupigia picha kwa ndani na nje linaonekanaje, lakini hapo umeuza sura tu.hata hivyo sisi mashabiki wa scania tunasema asante.

    naona scania wanafanya counter-attack kwa yutong za kichina.....nani alikwambia ushindani wa kibiashara siyo jambo zuri?

    ReplyDelete
  2. fix tupu hizo mara uje sikia ni mradi wa mwanafulani.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa MaguDecember 13, 2011

    Tujifunze watu wanapotaka habari wanataka waone taswira za subject. yaani basi. Sio mtangazaji au kama hapo huyo mzungu na Mr. dar express. Kifupi hawa ma Afisa habari huwa wana poteza maana ukiwaendekeza. Pia maelezo mengi mno kuliko subject. Tuone taswira ya subject.
    Michu wewe mwandishi mzuri, how come these.

    ReplyDelete
  4. Je hilo basi la ghorofa?

    ReplyDelete
  5. safi sana scania,jee bei yake mbona hujasema uncle.........

    ReplyDelete
  6. Tunaomba picha zaidi za mabasi haya

    ReplyDelete
  7. wangetueleza lina kitu gani tofauti na mabasi mengine kwa upande wa usalama na comfort ya abiria

    ReplyDelete
  8. ndani kuna choo, hakuna haja ya kondakta au utingo wala mpiga debe hahitajiki. sensors za wachafua hewa na kadhalika.

    ReplyDelete
  9. Kaka nakubaliana na wadau kadhaa hapo juu.

    Mtueleze lina FICHAZ gani mpya tofauti na ya zamani waliyokuwa wakitengeneza kama MAKO POLO, hilo ndio la muhimu, sio kutuambia tu scania wametoa basi jipya.

    HAITUSAIDII. Tujifunze MAKETING na BRANDING. Hata marketing ndogo tu hivi inatushinda? Halafu tumekalia kulalamika tu ooo "Watani wetu wa Jadi" wanatufanya hivui, mara vile, kumbe tunajilegeza wenyewe.

    ReplyDelete
  10. watu mnamambo he nanyie si mnunue yenu mkapige nayo picha??picha zote mlizowekewa bado hamjaridhika basi kama vipi mi nadhani nendeni ubungo mkalione live ikibidi mpande kidogo.

    ReplyDelete
  11. Ili biashara ieleweke vizuri ingefaa mtujulishe litafanya safari zake njia gani. Mikoa ipi na gharama zake.

    ReplyDelete
  12. yani bongo kila kitu kuzindua, kuzindua huh! mtu akitunga wimbo au movie anazindua sijui nini tabu kweli.

    ReplyDelete
  13. ... ndiyo basi jipya, kwahiyo????????

    ReplyDelete
  14. Ahhh makubwa basi jipya lina choo ndani na sensors za wachafua hewa ndani?...sawa litafaa maana pana wale ktk safari wanajisahau wanauchapa usingizi halafu wanaachia upepo pyuuu, duh tatizo limepata ufumbuzi kwa hiyo hatatafutwa mchawi au nani kaachia bomu kwa kuangalia viti vya nyuma au labda mbele....enhh haya mapya!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2012

    kama tunaweza nunua magari yakisasa namna hiyo kwanini tusinunue ambles kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kwani ni maskini wengi wanafia njiani wakielekea hospitalini kwa baisikeli au nikutaka ufahari watanzania tuamke na tuangalie mbele

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 26, 2013

    Naona scania mmejitahidi ila tu bei ya gari mjitahidi kupunguza il I tuachane Na malori

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...