Hili ni moja ya magari ya kubeba takataka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar,ambalo halina kibao cha nambari za usajiri kama ilivyo kwa magari mengine,sasa sijui kiko wapi na wanausalama barabarani sijui hawayaoni magari ya namna hii??maana yako mengi sana jijini hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Gari ya dola hiyo. Acha kelele, unafikiri mwanajeshi wa USA akija TZ anakuja na passport?

    ReplyDelete
  2. Usijali dereva amekariri kichwani haina haja ya kukiweka.

    ReplyDelete
  3. Kiko mbele, kiangalie vizuri. How can you ask us such question while you are the one who saw it. You might ask the driver/ owner not us.

    ReplyDelete
  4. Gari lenyewe pia ni takataka.. sasa namba za nini?

    ReplyDelete
  5. Gari lenyewe unaona kazi yake, michuruziko hadi mwekye matairi. Nimeona hata mataifa yaliyotupita kwa maendeleo magari kama haya hayana plate number hapo nyuma kwa vile yanatambuliwa kazi yake, kuna sehemu plate namba ipo.

    Jaribu kuwauliza wahusika watakueleza vinginevyo wasingeacha gari liwe linatembea kila siku. wakati mwingu tuko wavivu kufikiri.

    ReplyDelete
  6. Kwani tatizo nini? Kama namba ya gari kwanini hukumuuliza dereva?

    ReplyDelete
  7. Plate number ni takataka zaidi, imeshatangulia kinyamwezi "ukweni kwangu".

    ReplyDelete
  8. we mwenyewe hujasajiriwa ndio maana unataka kuona kibao ja usajiri badala ya usajili lol wapi babu kifimbo cheza mchafuzi wa lugha wewe halafu eti unajidai kuuliza upuuzi.

    ReplyDelete
  9. Magari haya yaundiwe kampeni kama ile ya wakati ule RPC Tibaigana aliposema breakdown zote lazima ziwe road worthy. Hapa napo kamanda Mpinga achangamke asisubiri kuambiwa

    ReplyDelete
  10. Usajiri mmmmmhhh hii itakuwa imesajiriwa geshini. Michuzi ni USAJILI sio usajiri.

    ReplyDelete
  11. Wewe yaelekea u mgeni katika mji/nchi hii. Hapa kwetu plate number haina maana yeyote kwa wenye nchi yao. Ina maana weye ndio mwenye macho makali ya kuona haya? Tuache sie tumeshajizoelea.

    ReplyDelete
  12. Watu mmeona hilo Gari tu mnapenda kulalamikia Serikali na Almashauri za jiji je hao wapita njia je kupita hapo haki au nauliza tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...