Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Cleopa David Msuya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkoa wa Kilimanjaro na uendelezaji wa fursa zilizopo kwa maendeleo ya mkoa huo na taifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Arnold Kilewo.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Na. Aron Msigwa -MAELEZO.

Wananchi wa mkoa Kilimanjaro wametakiwa kutumia fursa zilizopo katika mkoa huo zikiwemo mlima Kilimanjaro, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kujiletea maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Cleopa David Msuya amesema wananchi wana jukumu la kushirikiana na serikali katika kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo

Amesema kuwa kwa sasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo licha ya kuwepo fursa nyingi za maendeleo huku akisisitiza kuwa iwapo fursa hizo zitaendelea kutumika ipasavyo wananchi watanufaika na umaskini utapungua.

Amefafanua kuwa maendeleo ya mkoa huo yapo wazi kutokana na mkoa huo kuwa na maeneo mazuri ya uwekezaji katika shughuli za kilimo, nguvu kazi na miundombinu mizuri ya kurahisisha ufanyaji kazi.

“Ni dhahiri mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikoa yenye shule nyingi katika Tanzania, hivyo tuna nafasi nzuri ya kupata maendeleo pamoja na mlima Kilimanjaro tulionao ambao ni kivutio kizuri ndani na nje ya nchi yetu” Amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa mlima Kilimanjaro bado haujatumika ipasavyo katika kukuongeza pato la Taifa licha ya mlima huo kuwa na fursa nyingi za kuwainua kiuchumi wananchi hasa katika sekta ya utalii.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo wanaoishi maeneo ya mlima Kilimanjaro kuendelea kutunza mazingira yam lima huo ili uendelelee kuwa kivutio cha watalii na kuongeza pato la taifa.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa jukwaa hilo Bw. Arnold Kilewo amefafanua kuwa kwa sasa jukwaa hilo linaandaa utaratibu wa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wa mkoa wa Kilimanjaro ili kutathmini na kujadili changamoto mbalimbali za kimaendeleo za mkoa huo na namna ya kuendelea kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ndio tumeseme imeshindikana kuongelea maendeleo kitaifa sasa tunaanza kuangalia kimkoa. Japo lengo ni zuri lakini naona ni hatari na ni dalili ya serikali kuu kushindwa kuweka mikakati madhubuti kwa maendeleo ya Taifa zima.Ni angalizo kwa jinsi nionavyo.

    ReplyDelete
  2. Sina habari,hivyo Ndg cleopa D. Msuya aliwahi kuwa Makamo wa Rais wa Tanzania.

    ReplyDelete
  3. mulivyo kuwa kwenye system muliyafumbia macho hamupo mulalama. saizi wako wengi vile vile wakali kujifariji kuota misada ya matrector mawili miaka kumi ujinga mtu tanzania viongozi wanakalia kuiba tuuuuuuuuuuuu basi.

    ReplyDelete
  4. Malengo mazuri lakini, ni hatari kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu.Ikumbukwe, Mbali na fursa za kimaumbire ambazo mkoa huu umejaliwa, na zire za kiserikali pia zimeelekezwa huko, wether for fair or foul means..sasa tunakwenda wapi?

    ReplyDelete
  5. Kweli mkoa wa kilimanjaro una furusa tele, ili siasa ndiyo kikwazo cha maendeleo tunakwamisha kwa sababu za kisiasa

    ReplyDelete
  6. Mchangiaji wa kwanza hujawahi kusikia regional development?. Hujawahi kusikia zonal/area/reginal economic clusters?. Hujawahi kusikia reginal entrepreneuership?.

    Kila eneo lina "competitive advantage" zake na pia "comperative advantage". Mwanza/Shinyanga wanaweza kujipanga na kuzungumza sana kuhusu MADINI, PAMBA, MIFUGO, SAMAKI ZIWA VICTORIA. Arusha/Kilimanjaro wanaweza kujipanga kuzungumzia KAHAWA, UTALII, TANZANITE. Mtwara/Lindi/Ruvuma wanaweza wakajipanga kwenye UVUVI, KOROSHO, MAKAA YA MAWE, MAFUTA NA GESI.

    Kuzungumzia maendelea ya kimkoa ni sawa. Kuzungumzia ya wilaya ni sawa. Ya kata ni sawa. Yakijiji ni sawa. Ya mtaa ni sawa.Ya kwako binafsi ni sawa!. Ukiyajumlisha yote utagundua kumbe ujumla wake ni Taifa.

    DMK

    ReplyDelete
  7. ila hawa wazee walianzisha mambo mazuri na nyerere kwa sasa sidhani watakuwa na jipya la kuleta maendeleo, wakae pembeni watoe ushauri ukihitajika tu basi! kasi ya sasa hawaiwezi, kwanza viwnda vya nmkoa huu vimefia mikononi mwao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...