Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya Ufunguzi wa jiwe la Msingi la Barabara, wakati wa ufunguzi wa Barabara hiyo ya Mandela uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 2.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya Enrico Strampeli, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Nelson Mandela, iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Desemba 2, Temeke jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli , wakikata upete kwa pamoja ikiwa ni ishala ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na (kulia) kwa Balozi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, baada ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela uliofanyika leo Desemba 2, Temeke jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliowezesha ujenzi wa Barabara hiyo.
Picha ya Pamoja.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Ankal
ReplyDeleteBarabara hii mbona bado sana, ina mapungufu mengi jamani, hivi Dr. Magufuli anakubali kuwa barabara hii imefikia kiwango kweli, hapana nakataa kabisa. Kama hali imefikia hivi basi kazi iliyoko mbele yetu ni kubwa kuliko tunavyodhani wengi wetu.
wamezindua kitugani wakati hata taa za trafic hazifanyi kazi pale junction ya serengeti na ajili njingi zishatokea!
ReplyDeleteHaya tena tumefunguliwa barabara iliyotengenezwa basi vurugu tena .... kutanua, spidi kali kali na accidents kwa wingi.
ReplyDeleteHata sijui tutaendelea lini sisi!
Barabara inapita karibu na kwetu taa hakuna, alama za usalama kwa ajili ya watembeaji miguu hakuna !!
ReplyDeleteJamani huyu makamu wa raisi nae haoni hili? Kweli cheo cake yeye ni kusherehekea tuu kibaya haya, hakijamalizika haya!!