Umoja wa nchi za Ulaya umetoa kiasi cha Sh bilioni 11 kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda ch kutengeneza madawa ya binadamu cha TPI kilichopo njiro Mkoani Arusha, ambapo kitaanza kutengeneza dawa za kurefusha maisha kwa waathirika kwa ugonjwa wa ukimwi .

Hayo yalisemwa na Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya, Timoth Clarke wakati alipokuwa akielezea nchi za umoja wa ulaya zinavyojitahidi kutoa misaada mbalimbali ya kimaendeleo hususan katika sekta ya afya, elimu ,vifo vya kinamama na watoto .

Alisema katika kiwanda hicho kumeanzishwa kitengo cha kutengeneza dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa VVU na kwamba kiwanda hicho kama hakitafunguliwa ,Taifa linaweza kupoteza nguvu kazi ambazo zinatokana na wale wagonjwa waliokumbwa na maambukizi hayo na kuongeza kuwa kupatikana kwa dawa hizo nchini kutawezesha wale walioathirika na ugonjwa huo kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zinaweza kuinua uchumi wan chi.

Alisema si busara kwa nchi kuwatenga waathirika wa ukimwi sehemu mbalimbali bali jamii inatakiwa kuwapa TANZANIA ni nchi mojawapo inayojitahidi kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kutumia kampeni mbalimbali ikiwemo kupunguza vifo vya kinamama na watoto vinavyotokana na ugonjwa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...