Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa kampuni ya simu mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mwanyoka (wa kwanza kushoto) wakati akitoa maelezo ya namna shirika hilo linavyokabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo, wizi wa nyaza za simu, wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Chiku Gallawa akiwasikiliza wataalamu wa kampuni ya simu mkoa wa Tanga, ambao walimtembeza kwenye mitambo kuona namna wanavyorusha mawasiliano kwa wateja wao. nyuma ya RC ni msaidizi wake Bw. Joseph Sura.
Katibu Muhtasi wa meneja wa kampuni ya simu mkoani Tanga, Bibi Roselia Mpaka akimvalia kitenge Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja ya kutembelea kampuni ya simu mkoa wa Tanga TTCL.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa Akisalimia na Injinia Yohana Amosi ambaye ni menejea wa kitengo cha ufundi cha kampuni ya simu nchini (TTCL) mkoa wa Tanga, alipotembelea kuona shughuli zao.

Na Mashaka Mhando,Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Kampuni ya simu nchini (TTCL) mkoani Tanga, kutangaza kwa wananchi bidhaa zake ikiwemo kutoa elimu ya matuminzi hasa vijijini faida na umuhimu wa kuzinduliwa kwa mkonga wa Taifa wa mawasiliano.

Akizungumza jana, alipotembelea ofisi za kampuni hiyo zilizopo Jijini Tanga, Mkuu wa mkoa alisema wapo baadhi ya viongozi wakiwemo wananchi hawajui faida na matuminzi ya mkonga wa mawasiliano baada ya kuzinduliwa na Rais Jijini Dar es salaam miezi miwili iliyopita.

Alisema mkonga huo ambao utakuwa na faida kubwa katika mawasiliano ya bei rahisi na upatikanaji wa data na Interneti katika ofisi za serikali na kwa matumizni ya wananchi hatua ambayo sasa kampuni hiyo inatakiwa kueleza matunzi hayo na faida ambazo watumiaji wanaweza kunufaika nazo hasa baada ya kufungiwa.

“Mkonga wa Taifa watu wengi na hata baadhi ya viongozi hawajui umuhimu wake wemeona tu Rais amezindua na kuelezea kidogo…Ni vema sasa wenzetu wa TTCL wakaelezea faida na umuhimu wake kwa Taifa baada ya upatikanaji wake, najua kila kitu kitakuwa rahisi katika mawasiliano waambieni wajue” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa changamoto kwa kampuni hiyo kuweza kwenda katika maeneo ya vijijini kutoa elimu kwa viongozi wa serikali za vijiji wakatambua umuhimu wa kuunganisha mitandao katika ofisi za umma ikiwemo shule za sekondari za kata kuwa wezesha wanafunzi kuweka kuwa karibu na mawasiliano duniani.

Awali akimpa taarifa mkuu huyo wa mkoa Meneja wa TTCL mkoani Tanga, Bw. Rashid Mwanyoka alisema kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi wa mkonga huo wa taifa ambao unapita vijijini hivyo wanajipanga kuweza kutoa elimu kwa serikali za vijiji kuona umuhimu wa kuulinda kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema pamoja na changamoto hiyo, pia wanakabiliwa na madeni hasa ofisi za serikali ikiwemo suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme ambapo pindi unapokatika wanalazimika kutumia kiasi cha shilingi milioni 16 kwa mwezi kutokana na kununua mafuta katika mitambo yao ya kuendeshea mitambo hiyo.

“Changamoto nyingine ni wizi wa nyaya za simu lakini katika kipindi hiki tumeweza kudhibiti na tunalala usingizi baada ya kushirikiana na wenzetu wa polisi kwa kuunda kamati ambayo imekuwa na mafanikio makubwa ya kudhibiti tatizo hili,” alisema Bw. Mwanyoka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. je ni kweli mkonga wa mawasiliano ukimalizika kujengwa makampuni ya simu yatashusha zaidi bei za mawasiliano?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...